Dar es Salaam Young African ama Yanga imesema kwamba inafanya mikakati kabambe ya kuhakikisha wanamsajili tena kipa wao nambari mbili Yew Berko.
Hayo yamesemwa na msemaji wa klabu hiyo Luis Sendeu baada ya Shirikisho la kandanda Tanzania kumpiga stop golikipa huyo kucheza mechi zilizobaki katika michuano ya ligi Kuu ya Tanzania bara.
Wakati huo huo Sendeu amesema wamejiandaa vema katika mchezo wa kesho wa ligi kuu Tanzania Bara siku ya Jumapili dhidi ya Azam na kutamba watahakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi ili kujiweka mazingira mazuri.Amesema licha ya kuwa matumaini madogo ya kuweza kutetea ubingwa kufuatia Simba kuwaacha mbali kwa kuwa na pointi nyingi, amesema wao wanachohitaji sasa ni ushindi katika kila mchezo wanaoshuka dimbani.
Wakati huo, Katika maandalizi ya kukutana na Yanga siku ya Jumapili katika uwanja wa Uhuru kikosi cha Azam FC kipo katika maandalizi makali ya kuweza kukikabili kikosi hicho kutoka Jangwani.
Azam ilikutwa na mwandishi wa tovuti hii ikiwa katika mazoezi ya kiwango cha juu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwani muda mrefu wa mazoezi hayo ya masaa mazili ulitumika kwa kuwapa mbinu tofauti tofauti za ufungaji kwa washambuliaji wa kikosi hicho pamoja na magolikipa.
"mazoezi haya maalumu yanawajenga washambuliji kuongeza mbinu za kufunga magoli pindi wawapo uwanja, nimewafundisha kufanya mashambulizi ya kushtukiza 'counter attack', mashambulizi ya kawaida ili kuwaweka sawa" amesema kocha mkuu wa Azam FC Itamar Amorin.
Mazoezi hayo hayakuwa kwa washambuliji tu bali pia kwa magolikipa wamepata mazoezi kudaka mashambulizi ya kushitukiza na ya kawaida. Mazoezi hayo yaliwahusisha magolikipa wote, Vladmir, Ben Kalama na Maridadi Haule.
Wakifanya mazoezi kwa nguvu zaidi washambuliaji wa Azam FC waliweza kufunga magoli kulingana na nafasi wanazozipata huku mchezaji Saidi Swedi akiwa ndiye anayeongoza kwa kuwafunga magolikipa wake akifuatiwa na Shaaban Kisiga, Ally Manzi, Nsa Job na Yahya Tumbo.
Washambuliaji wengine waliokuwa wakipata mazoezi ni Luckson Kakolaki, Tumba Swed, Selemani Kassim 'Selembe', Philip Alandu, Jamal Mnyate na Salum Machaku. washambuliaji hao walikuwa wakipokea mipira iliyokuwa ikipigwa na viungo na mabeki wa timu hiyo wakiongozwa na Ibrahim Shikanda, Malika Ndeule, Dan Wagaluka, Jukumu Kibanda, Salum Aboubakari na Mau Ally.
Upande wa magolikipa, golikipa namba moja wa Azam FC Vladimir ndiye alikuwa mtaalam wa kupangua mashambulizi aina yoyote na kuweza kufungwa magoli matatu yakiwa ni machache zaidi kuliko magolikipa wenzie Kalama na Maridadi ambao walifungwa magoli zaidi ya matano kila mmoja.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment