Ligi kuu ya Vodacom imeingia katika raundi ya 19 kwa kumalizia mchezo wa mwisho kati ya Azam FC na Yanga ambapo umeshuhudia Yanga ikiibuka na ushindi ya 2-1 na hivyo kuizuia Simba kutangaza ubingwa mapema
Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa uhuru, Yanga walianza kupata bao la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa mchezaji Mrisho Ngasa.
Dakika ya 26 Yanga walipata goli la pili kutoka kwa Jerryson Tegete baada ya mabeki wa Azam FC kufanya uzembe golini.
Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco alifunga goli la pili kwa njia ya penalt iliyopatikana baada ya beki wa Yanga George Owino kumwangusha mchezaji wa Azam FC Yahya Tumbo katika eneo la hatari.
Mchezo huo uliojaza mashabiki wengi hadi mapumziko matokeo yalikua 2-1, Kipindi cha pili Azam walibadilisha mchezo na kutoa mashambuliz mengi, Bocco na Tumbo walikosa nafasi nyingi za wazi.
Azam FC, Vladmir Niyonkuru, Ibrahim Shikanda, malika ndeule, aggrey Morris, erasto nyoni/Luckson Kakolaki, Ibrahim Mwaipopo, Danny Wagaluka, salum aboubakar, Seleman Kassim,/Shaban Kisiga, John Bocco, yahya tumbo
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment