Timu ya taifa ya Tanzania inataraji kuingia kambini siku ya jumanne jioni na kuanza mazoezi siku ya jumatano tayari kuanza maandalizi ya mchezo wa kwanza wa kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezjai wa ndani CHAN dhidi ya Somalia.
Akizungumza na waandishi wa habari kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania taifa Stars Marcio Maximo amesema mchezo dhidi ya Somalia anataraji utakuwa mgumu kwasababu watacheza mchezo mmoja tu hapa nyumbani Tanzania hivyo anaamini fika watakuja kutaka kushinda.
Amesema licha ya Somalia kutoa upinzani mara kwa mara kwa Taifa Stars lakni sasa wakati umefika wa kuithibitishia kwamba Tanzania ya sasa katika soka siyo ile ambayo walikutana nayo mwaka mmoja au miwili iliyopita.
Maximo amewataka wachezaji kujituma katika mazoezi na kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo badala ya kushinda mchezo magazetini.
Aidha Maximo amewataka wa Tanzania kuiunga mkono timu ya taifa ya Tanzania, kwani inapofungwa siyo taifa Stars wala kocha Maximo, bali ni Taifa la Tanzania.
WACHEZAJI WA TAIFA STARS WATAKAOINGIA KAMBINI SIKU YA JUMANNE
GOALKEEPERS
Shaban Kado - Mtibwa
jacksona Chove - JKT Ruvu
Fullbacks
Shadrack Nsajigwa - Yanga
Salum Kanoni - Simba
Juma jabu - Simba
Stephano Mwasika - Moro United
CENTER BACKS
Nadir Haroub - Yanga
Kevin Yondani - Simba
Aggrey Morris - Azam
David naftal - Simba
MIDFIELDERSDS
Abdull-halim Humoud - Mtibwa
Erasto Nyoni - Azam
Shaban Nditi - Mtibwa
Juma Nyoso - Simba
Abdi Kassim - Yanga
Mbwana Samatta - Afrcan Lyon (U-20 National Team)
Nurdin bakari - Yanga
jabir Aziz - Simba
Kigi Makasi - Yanga
Hamid Thabit - African Lyon (U-20 national Team)
Seleman Kassim - Azam
FORWADS
Mussa Hassan "Mgosi" - Simba
Mrisho Khalfani Ngassa - Yanga
John Bocco - Azam
Jerson Tegete - yanga
Thomas Emanuel - Moro United/ National team U-20
Yusuf Abbas Soka - African Lyon/national team U-20
Uhuru Suleima - Simba
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
5 days ago
No comments :
Post a Comment