NYON, Switzerland
Klabu ya Arsenal itaikabili Barcelona katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya katika hatua ya robo fainali, ikiwa historia ya inajirudia tena kwani walikwishawahi kukutana mwaka 2006 ambayo Barca alifanikiwa kuibuka mbabe.Manchester United, ambayo ilichapwa na Barcelona katika mchezo wa fainali mwaka jana, sasa Man itacheza na Bayern Munich, wakati Inter Milan yenyewe itacheza na CSKA Moscow na Lyon imepangwa kucheza Mfaransa mwenzao klabu ya Bordeaux katika ratiba ambayo leo Ijumaa.
Michezo wa kwanza umepangwa kuchezwa March 30/31 huku mchezo wa marudiano ukichezwa April 6/7.
Ratiba ya nusu fainali pia imepangwa tayari, ambapo mshindi katika mchezo kati ya Man United na Bayern Munich atakutana na Lyon au Bordeaux, na mshindi kati ya Inter au CSKA atacheza na mshindi kati ya Arsenal au Barca.
Katika michezo ya robo fainali tayari Ufaransa imekwishajihakikishia kuwa na timu moja katika hatua ya Nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu klabu ya Monaco ifanikiwe kutinga hatua hiyo mwaka 2004.
Kwa klabu ya Arsenal ratiba imempa nafasi ya kulipa kisasi cha kutolewa na vijana hao wa Hispania, Barcelona 2-1 walipokutana katika dimba la Stade de France jijini Paris miaka minne iliyopita.
The Gunners wamefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali wakiwa na rekodi ya kumchapa Porto nagoli 5-0 na kusonga mbele kwa jumla ya magoli 6-2, utakumbuka mdau wa viwanjani, Porto iliwahi kutwaa ubingwa huo mwaka 2004.
Kikosi cha Mzee Arsene Wenger, kitakuwa kikisaka ushindi wake wa kwanza barani Ulaya.
Mabingwa mara tatu wa michuano hii, Manchester United kwa mujibu wa ratiba sasa wanatakiwa kunoa upya mapanga yao, kwani wanakutana na Bayern, utakumbuka waliwahi kukutana huko Camp Nou na Man kukfanikiwa kutwaa ubingwa mwaka 1999.
Lakini miaka miwili baadae, Bayern iliichapa Man United katika hatua ya robo fainali na kufanikuiwa kulitwaa kombe.
Msimu huu fainali zitapigwa katika uwanaja wa Real Madrid, Dimba la Santiago Bernabeu hapo May 22, itakuwa ni mara ya kwanza fainali za ligi ya mabingwa kuchezwa siku ya Jumamosi.
Ratiba ya hatua robo fainali.
Lyon (FRA) v Bordeaux (FRA)
Bayern Munich (GER) v Manchester United (ENG)
Arsenal (ENG) v Barcelona (ESP)
Inter Milan (ITA) v CSKA Moscow (RUS)
Mchezo wa kwanza utapigwa March 30/31
michezo ya marudiano itapigwa April 6/7
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment