Wachezaji bora wa Afrika, Didier Drogba wa Ivory Cost, Michael Essien wa Ghana na Mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto’o Fils ndiyo wanao waniwa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika mwaka 2009.
Kati ya wachezaji hawa watatu, Essien ndiyo mchezaji pekee ambaye hajawahi kutwaa tuzo hiyo, huku Eto’o akiitwa mara tatu tuzo hiyo mwaka 2003, 2004 na 2005, na Drogba mwaka 2006.
Tuzo hizo ambazo zitatolewa siku ya Alhamisi, March 11 mjini Accra, Ghana katika Banquet Hall, mchezaji mmoja kati ya hawa watatu ndiyo atakayerithi mikoba ya mshambuliaji wa kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor.
DIDIER DROGBAJina kamili: Didier Drogba
Tarehe ya kuzaliwa: March 11, 1978
Sehemu aliyozaliwa: Abidjan, Côte d'Ivoire
nafasi anayocheza: Ushambuliaji
Klabu ya sasa: Chelsea
Klabu alizowahi kucheza: Le Mans (Ufaransa), Guingamp (Ufaransa), Marseille (Ufaransa)
Timu ya taiafa amejitokeza mara66 na kufunga magoli 43.Drogba alizaliwa mjini Abidjan mwezi March 11, 1978 na kwa sasa anaichezea klabu ya Uingereza ya Chelsea.
Akiwa mdogo Drogba alihamia Ufaransa, na kuishi na ndugu wa familia, baada ya soka la vijana, Drogba alijitokeza kwa mara ya kwanza katika soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 18 katika Ligue 2 akiwa na klabu ya Le Mans.
Alisaini mkataba wake wa kwanza akiwa mchezaji wa kulipwa akiwa na umri wa miaka 21 lakini aliweza kufanya hivyo hadi msimu wa 2002/2003 ndipo alipoweza kuanza kung`ara, baada ya kufnga magoli 17 katika michezo 34 aliyojitokeza katika Ligue 1 akiwa na klabu ya Guingamp.
Msimu huo ndiyo kwa mara ya kwanza aliweza kujitokeza katika timu ya taifa ya Ivory Cost, ikiwa ni mwezi September na kufunga goli kwa mara ya kwanza akiwa na timu ya taifa mwezi Februari.Alihamia Olympique de Marseille mwaka 2003 na aliendeleza upachikaji mabao katika safu ya ushambuliaji, akimaliza ligi akiwa nafasi ya tatu kwa upachikaji magoli, akiwa na jumla ya magoli 19 na kufanikiwa kujitokeza katika fainali za mwaka 2004 katika UEFA Cup.
Drogba alijiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2004 na amejitengenezea mazingira mazuri na kuwa ndiye mchezaji hatari katika dimba la Stamford Bridge.
Hata hivyo amekuwa akitiliwa mashaka katika upande wa uwajibikaji wake katika timu ya taifa ya Ivory Cost hasa baada ya kushindwa kutamba katika michuano ya 18 ya mataifa ya Afrika iliyofanyika nchini Angola, ambapo walitolewa walitolewa katika hatua ya robo fainali wakati wanatarajiwa kutinga fainali za kombe la Dunia.
Mshambuliaji huyo hatari, alitwaa tuzo ya mwanasoka bora Afrika mwaka 2006 katika sherehe ambazo zilifanyika mjini Accra, Ghana.
MICHAEL ESSIEN
Jina kamili: Michael Essien
tarehe ya kuzaliwa: December 3, 1982
Sehemu aliyozaliwa: Accra, Ghana
Nafasi anayocheza: Kiungo
Klabu ya sasa: Chelsea
Klabu alizowahi kucheza: Liberty Professionals (Ghana), Bastia SC (Ufaransa), Olympique Lyon (Ufaransa)
Amejitokeza timu ya taifa mara 51 amefunga magoli 9.Essien alizaliwa December 3, 1982 mjini Accra na wazazi wake ni wa Ghana, mama anaitwa Aba Gyandoh na mzee James Essien, na alianza safari yake ya soka kama ilivyo kwa wa Ghana wengi akicheza soka la mtaani.
Alizoma masomo ya Sekondari katika shule ya St. Augustine’s College iliyopo Cape Coast, moja ya shule na chuo ambacho kinaheshimika sana nchini Ghana, Kabla ya kujiunga na Liberty Professionals.
Kiungo alianza safari yake vema katika klabu ya national juvenile, Black Starlets akiwa chini ya kocha mkongwe Cecil Jones Attuquayefio na alikuwa chachu ya kuiwezesha timu ya taifa ua vijana chini ya umri wa miaka 17 kutwaa medali ya fedha katika fainali za Dunia za vijana chni ya umri wa miaka 17, michuano iliyofanyika New Zealand.
Baada ya kumalizika michuano hiyo ya Dunia ya vijana, Alitajwa kuwa ndiye mchezaji ambaye alikuwa akiwindwa na vilabu vingi barani Ulaya, lakini klabu ya Bastia SC ya Ufaransa ilifanikiwa kumnasa na kudumu nae kwa misimu mitatu kabla ya kununuliwa na Olympique Lyon.
Alipewa jina la Utani la “The Bison” kufuatia kuwa na nguvu, anayetoa upinzani mkali na kuweza kuwachezesha wenzake.
Uwezo huo ndiyo uliyomshawishi kocha mzaliwa wa Ureno, Jose Mourinho, ambaye alilazimika kutoa kiasi cha pauni milioni 24.4 ambazo ni sawa na Euro milioni 38, na kuwa ndiyo mchezaji ghalli wa Afrika kununuliwa na klabu ya Chelsea mwaka 2005.
Essien alijitokeza kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya Ghana mwaka 2002 katika michuano ya mataifa ya Afrika, michuano iliyofanyika Mali lakini alipata maumivu ambayo yalimlazimu kuondolewa baada ya kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Morocco.
Miaka minne baadae, alikuwa ndiyo chachu ya kuiwezesha Ghana kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia ambazo zilifanyika nchini Ujerumani kabla ya kutolewa na Brazili kwa kuchapwa 0-3.
Katika fainali za mataifa ya Afirka ambazo zilifanyika nchini Ghana mwaka 2008, alipata umaarufu mkubwa kwa staili yake ya ushangiliaji iliyopewa jina la “Kangaroo Dance” kila mara walipofunga goli.
Anatajwa kuwa ndiye kiungo ambaye anauwezo mkubwa kuwahi kutokea katika kikosi cha Ghana.
Tangu mwaka 2006, amekuwa akijitokeza katika tuzo za mwanasoka bora wa Afrika, lakini amekuwa akitoka mikono mitupu.
SAMUEL ETO’O FILS
Jina kamili: Samuel Eto'o Fils
Tarehe ya kuzaliwa: March 10, 1981
Sehemu ya Kuzaliwa: Nkon, Cameroon
Nafasi: Mshambuliaji
Klabu yake ya sasa: Inter Milan
Klabu alizocheza: Real Madrid (Hispania), Leganes (Hispania), Espanyol (Hispania), Mallorca (Hispania), Barcelona (Hispania)
Katika timu ya taifa amejitokeza mara 94 na kufunga magoli 44.Samuel Eto'o Fils alianza safari ya kusakata kandanad katika shule maarufu ya michezp nchini Cameroon ya Kandji Sports Academy kabla ya kuhamia nchini Hispania na kujiunga na klabu ya Real Madrid mwaka 1997.
Akiwa na umri mdogo aliuzwa kwa mkopo katika klabu ya ligi daraja la pili ya Leganes kabla ya kununuliwa na klabu ya Mallorca sehemu ambayo alifunga magoli 48 katika michezo 120 aliyojitokeza katika kipindi cha miaka minne.
Eto’o alijiunga na Barcelona mwaka 2004 na ndipo alipoanza kung`ara na vijana hao wa Catalans.
Alifunga magoli 100 katika kipindi cha miaka misimu mitano akiwa na FC Barcelona, na anashikilia rekodi ya kuwa ndiye mchezaji mwenye asili ya Afrika kujitokeza michezo mingi katika La Liga.
Ni mchezaji wa pili kufunga katika fainali za ligi ya mabingwa barani Ulaya mara mbili, ikiwa ni mwaka 2005 na 2008.Akiwa na timu ya taifa ya Cameroon, alikuwa ni moja ya wachezaji ambao walitwaa uchampion wa michuano ya Olimpiki katika soka iliyofanyika Sydney, Australia mwaka 2000.
Amefanikiwa kutinga katika fainali mbili za Dunia na kujitokeza mara sita katika fainali za mataifa ya Afrika huku akishuhudia wakilibeba mara mbili, na anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote katika michuano ya mataifa ya Afrika, akiwa na rekodi ya kufunga magoli 18.
Eto`o kwa sasa ndiye kapteni aliyechaguliwa na kocha wa Cameroon Paul Le Guen na alikuwa chachu ya kufuzu kucheza fainali za Dunia na mataifa ya Afrika licha ya kutolewa katika robo fainali.
Eto’o amefanikiwa kutajwa kuwa mwanasoka bora wa Afrika mara tatu mfululizo, ikiwa ni mwaka 2003, 2004 na 2005.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment