Mkurugenzi wa Andika Afrika Publishers, Neema Kambona akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya Tamasha la wasanii wenye vipaji na ubunifu litakalofanyika jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 20,2010 katika ukumbi wa Nafasi Art Space Mikocheni . Tamasha hilo limedhaminiwa na kampuni ya Simu za mkononi ya Zain Tanzania.
Sauda Simba kutoka Trinity Promotion (katikati) akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam juu ya Tamasha la wasanii wenye vipaji na ubunifu litakalofanyika Jumamosi Machi 20, 2010 katika ukumbi wa Nafasi Art Space Mikocheni Dar es Salaam. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya Simu za mkononi ya Zain Tanzania. Kulia ni Meneja uhusiano wa Zain Muganyizi Mutta na kushoto ni Fred Halala kutoka Nafasi Art Space.
Mratibu wa Tamasha la wasanii wenye vipaji na ubunifu litakalofanyika jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 20, 2010 katika ukumbi wa Nafasi Art Space Mikocheni jijini Evans Bukuku (kushoto) akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi ya Tamasha hilo ambalo limedhaminiwa na kampouni ya Zain Tanzania. Wengine ni Muganyizi Mutta wa Zain na Sauda Simba wa Trinity Promotion.
Mtaalam wa kuchonga vinyago Mwandale Wakwenya akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya kazi zake atazoonyesha wakati wa Tamasha la Wasanii wenye vipaji na ubunifu litakalofanyika Jumamosi Machi 20,2010 katika ukumbi wa Nafasi Art Space Mikocheni Dar es Salaam. Tamasha hilo limedhaminiwa na kampuni ya Zain Tanzania. Kushoto ni Neema Kambona kutoka Andika Africa Publishers.
Kampuni ya simu za mikononi Zain kudhamini maonyesho ya wasanii wenye vipaji na ubunifu.
Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania inadhamini maonyesho ya wasanii wenye vipaji mbali mbali kama vile muziki, uchoraji, utunzi na vipaji vinginevyo, yatakjayofanyika jumamosi machi 20 katika ukumbi wa Nafasi Art Space Mikocheni nyuma na Fiesta Pub jijini Dar es Salaam.
Maonyesho hayo yatawapa nafasi wasanii kuonyesha vipaji vyao na pia kuonyesha kazi zao mbali mbali za kisanaa.
Washiriki katika maonyesho hayo ni wahitimu wa kozi mbali mbali za kisanaa waliomaliza mafunzo mwaka 2009. Jumla ya wasanii 60 walishiriki kozi hiyo chini ya udhamini wa Balozi wa Denmark na British Council, kama sehemu yao ya kusaidia sekta ya ubunifu.
Kati ya washiriki wa maonyesho hayo ni mwandale Mwanyekwa ambaye ni mchongaji maarufu wa vinyago anayefahamika kitaifa na kimataifa kwa ubunifu wake wa kipekee, Mwanamitindo Kemy Kalikawe, Mwanamitindo Chipukizi Naledi Label, pamoja na Sauda Simba ambaye atakuwa akizindua wimbo w ake wa "SAUTI YA SAUDA". Huu ni wimbo wa pili na unafuatia mafanikio ya Alkbamu yake ya kwanza maarufu ya "SIMPLY JAZZMIN".
Wengine ni mtayarishaji wa muziki maarufu Ambrose Akula Akwabi a.k.a DUNGA ambaye alishiriki katika kutengeneza nyimbo ambazo zimewahi kutamba sana kama vile ANITA wa MATONYA, Mr Politician ya NAKAAYA, NIpe Deal ya Ngwear na wengineo wengi.
Maonyesho yataanza saa nne Asubuhi. Watoto pia watakuwa na nafasi ya kufurahi na wanamuziki mbalimbali kama vile Daz, Ngoma Afrika, Sauda Simba na kuangalia picha mbali mbali zitakazoonyeshwa na wataalam wa picha wa World Pictures (WAPI) ambao wamekuwa waikishirikiana na British Council kuandaa tamasha kama hili ambalo kwa sasa ni tamasha la tatu.
Meneja mawasiliano wa Zain Tanzania Beatrice Singano amesema Zain Tanzania imefurahi kudhamini maonyesho haya ili kuwasaidia wasanii wa Tanzania kuonyesha vipaji vyao na kujitangaza, jambo ambalo litawasaidia kufahamika katika soko na kujiendeleza.
No comments :
Post a Comment