Timu ya taiafa ya wanawake Tanzania Twiga Stars imefanikiwa kutinga hatua ya pili ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wanawake baada ya kutoka sare ya kufungana goli 1-1 katika mchezo wa marudiano uliyochezwa Jumamosi uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Twiga Stars inasonga mbele kwa jumla ya magoli 4-2 baada ya mchezo wa kwanza kushinda 3-1 walipokutana nchini Ethiopia majuma mawili yaliyopita.
Katika mchezo wa jana timu ya Twiga Stars licha ya kufanikiwa kusonga mbele lakini ilionekana kucheza mpira katika kiwango cha chini tofauti na Ethiopia ambao walikuwa wakionekana kucheza mpira wenye mipango ya kusaka ushindi.
Sasa Twiga Stars itakutana na Eritrea katika hatua ya pili ya kusaka nafasi ya kucheza mataifa ya Afrika soka la wanawake, fainali ambazo zitafanyika nchini Afrika Kusini mwaka huu.
No comments :
Post a Comment