Wekundu wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliyochezwa katika uwanja w Uhuru.
Simba ndiyo ilikuw aya kwanza kupata goli kupitia kwa mchezaji Mohammed Banka kwa shuti kali kabla ya mchezaji Bruno Adolf wa JKT Ruvu aliyefunga kwa mkwaju wa Penati kabla ya kwenda mapumziko.
KAtika dakika za lala salama Mussa Hassan Mgosi alifunga goli la pili kabla ya mchezaji Uhuru Suleimani kufunga goli la tatu na kuwafanya kuibuka na ushindi wa magoli 3-1.
Hata hivyo mchezaji Mwinyi kazimoto alijikuta akitolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuzozana na mwamuzi jambo ambalo litamfanya mchezaji huyo tegemeo wa JKT Ruvu kukosa michezo mitatu iliyosalia katika ligi kuu Tanzania Bara.
Kufuatia ushindi huo, Simba sasa imefikisha Jumla ya pointi 53 huku wakiwa wamesaliwa na pointi mbili kuweza kutangaza ubingwa.
katika mchezo mwingine uliyochezwa mjini Morogoro Mtibwa Suger imefanikiwa kuifunga timu ya Moro United jumla ya magoli 2-0, na kuwafanya sasa kufikisha jumla ya pointi 30.
Huko Kaitaba, timu ya Kagera Suger imelazimishwa sare ya bila kufungana na klabu ya Afrika Lyon.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment