Tanzania imeendelea kulala katika nafasi ya 108 katika viwango vya soka Duniani huku barani Afrika ikishika nafasi ya 26.
Tanzania imelazimika kubaki katika nafasi hiyo bila kupanda wala kushuka kufuatia kutokuwa na michezo ya kimataifa kwa timu za Taifa mwezi Februari.
Hata hivyo kushuka kwa Tanzania kulitokana na kutoshiriki michuano yeyote ya kimataifa kwa muda mrefu tangu itolewe katika michuano ya kuwania nafasi ya kufuzu kucheza mataifa ya Afrika na kombe la Dunia.
Uganda ndiyo nchi pekee ya ukanda wa Afrika Mashariki ikiendelea kung`ara nafasi za juu katika viwango vya soka kufuatia kushika nafasi ya 74 Duniani huku Afrika ikiwa nafasi ya 15, Rwanda ikkishika nafasi ya 105 Duniani huku Afrika ikishika nafasi ya 25, Kenya nafasi ya 113 Duniani wakati Afrika ikishika nafasi ya 30.
Mabingwa wa Afrika, Misri ambao katika msimamo uliyopita walikuwa katika kumi bora ya viwango vya soka Duniani, safari hii imeondolewa.
Mafarao hao wa Misri wameshuka kwa nafasi saba hadi nafasi ya 17 Duniani, ikimaanisha hakuna taifa lolote Afrika ambalo linatamba katika mataifa 15 Duniani katika viwango vya FIFA.Hata hivyo Misri inaeendelea kuwa kinara kwa kandanda barani Afrika katika viwango vya soka.
Cameroon sasa inashika nafasi ya 20 Dunia, ikifuatiwa na Nigeria nafasi ya 21 na Ivory Coast ikishika nafasi ya 22.
Mabadiliko makubwa katika viwango vya soka Duniani yametokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana mwishoni mwa mwaka jana, na utakumbuka mchezo wa fainali ya mataifa ya Afrika mwaka 2006 ilichezwa mwezi Februari na si januari kama ilivyokuwa mwaka huu.
Mabadiliko makubwa yanatarajiwa kujitokeza mwezi ujao, kufuatia kuwa na michezo mingi ya kimataifa kwa mujibu wa kalenda ya FIFA.
Itakuwa ni nafasi ya timu nyingi za mataifa mbali mbali kuweza kutengeneza mazingira ya kupanda katika viwango vya FIFA, siyo tu kwa wale ambao wamefuzu tu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2010.
Afrika Kusini, ndiyo taifa pekee la Afrika ambalo linashiriki fainali za Dunia huku ikiwa nje ya kumi bora katika viwango vya soka Afrika na Dunia, Afrika inashika nafasi ya 16 huku katika viwango vya soka Duniani ikishika nafasi ya 81.
Hispania inaendelea kushika nambari moja katika viwango vya soka Duniani, ikiwa mbele ya Brazilin a Uholanzi.
Top ten in Africa - world rankings in brackets:
1. Egypt (17)
2. Cameroon (20)
3. Nigeria (21)
4. Ivory Coast (22)
5. Ghana (28)
6. Algeria (32)
7. Gabon (43)
8. Burkina Faso (51)
9. Mali (54)
10. Tunisia (55)
Jana Taifa Stars ilifungwa na timu ya taifa ya Uganda 3-2 katika mchezo uliyochezwa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kufungwa katika mchezo huo huenda kukapelekea ikashuka tena katika viwango vya soka Duniani pindi watakapotoa mwezi Ujao.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment