Mabondia wa klabu ya ngumi ya Simba wakijifua kwa ajili ya mpambano wao na Ashanti siku ya Ijumaa.Mabondia wa Klabu ya ngumi ya Ashanti ya Ilala Dar es Salaam wakifanya mazoezi ya tumbo kwa ajili ya mpambano wao na klabu nyingine siku ya Ijumaa.
Klabu mpya ya mchezo wa ngumi ya Ashanti siku ya Ijumaa inatarajiwa kutambulishwa kwa klabu zingine za mchezo huo katika ukumbi wa CCm Ilala.
Kocha wa timu ya Shanti Rajabu Mhamila ambaye pia ni mpiga picha wa viwanjani.blogspot.com amefahamisha kuwa klabu hiyo yenye mabondia tisa itatambulishwa kwa klabu zingine ili itambulike kuwa ni miongoni mwa klabu zinazoendeleza mchezo huo nchini.
Aidha Amesema, katika utambulisho huo atavikutanisha vilabu vya Simba, Amana, Vingunguti na wenyeji Ashanti ambapo kila klabu itatoa mabondia wa tatu kuzinyuka.
Katika pambano hilo linalotarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu, klabu ya Ashanti itatoa wachezaji tisa na kila bondia atacheza na klabu nyingine.
Lengo la kuanzishwa kwa klabu hiyo ni kukuza vipaji vya vijana pamoja na kuonyesha wachezaji wapya katika ulimwengu wa masumbwi katika uzito tofauti.
klabu ya Ashanti imeanzishwa hivi karibuni na inaundwa na mabondia Juma Salum, Yahaya Hamisi, Ramadhani Gumbo, Ramadhani Kasi na Abdujeri Kadir.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment