Shirikisho la kandanda Duniani FIFA inatarajiwa kusikiliza madai ya shambulio lililofanywa nchin Misri wakati Algeria kabla ya mchezo wao wa kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia mjini Cairo tarehe 15 April.
FIFA imesema kwamba kamati ya nidhamu itasikiliza kesi hiyo watakapokutana Zurich.
kwa mujibu wa sheria za kinidhamu za FIFA zinaitaka nchi mwenyeji kuhakikisha usalama wa wageni.
Chama cha soka cha Misri kinaweza kutozwa fainali, ama wanaweza kupewa adhabu ya kutochezewa michezo ya kimataifa nchini mwao.
wachezaji wa Algeria na viongozi wao walijeruhiwa na vioo vilivyopasuliwa kwa kushambuliwa na mawe na mashabiki wa Misri kabla ya mchezo mwaka jana mwezi Novemba.
Misri ilishinda mchezo huo kwa magoli 2-0 na kulazimisha kuchezwa mchezo wa mtoano nchini Sudan, ambapo Algeria ilishinda 1-0 na kufanikiwa kutinga fainali za kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.
No comments :
Post a Comment