SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu nchini TBF katika kuhakikisha linahamasisha na kuibua vipaji vya mchezo wa mpira wa kikapu kwa watoto imeamua kushirikiana kwa karibu na vyombo vya habari nchini.
Akizungumza jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Kamisheni ya watoto Selemani Semunyu alisema wamefikia hatua hiyo ikiwa ni kuibua ari kwa watoto na wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki Kikapu.
“ Hatutapata wachezaji wachanga kama hawatahamasishwa kwa kuangalia ligi mbalimbali Sheria na mafanikio ya ,mchezo huo kitu ambacho kinahitaji msaada mkubwa kutoka kwa waandishi wa Habari na vyombo vya habari kwa ujumla,” alisema Semunyu.
Aliongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuwaonyesha wachezaji ligi mbalimbali za mpira wa kikapu Duniani ikiwemo Ligi ngumu Duniani ya kikapu ya marekani National Basketball Association NBA na mbinu na hatua mbalimbali za uchezaji pamoja na mafanikio ya wachezaji mbali mbali kupitia makala zao.
Alisema miongoni mwa vyombo vya habari ambavyo tayari vimeridhia kushirikiana na TBF ni pamoja na TBC ambao wameahidi kuonyesha ligi ya NBA kwa siku ya Jumamosi au jumapili.
“ kwa mujibu wa Mazungumzo ya Makamu wa rais wa TBF Phares Magesa na Mkurugenzi wa TBC Tido Mhando kilichobaki kwetu ni kumuandaa mchambuzi ambaye atakuwa akifafanua mambo mbalimbali katika mchezo husika,”alisema Semunyu.
Semunyu alisema Mchakato unaendelea kwa vyombo vingine na pia kutafuta uwezekano wa Ligi za ndani kuonyeshwa hata kwa baadhi ya michezo.
Pia alisema anavishukuru vyombo mbalimbali vya habari nchini ambavyo viko mstari wa mbele kutangaza masuala ya kikapu hali ambayo yanaongeza chachu kwa vijana kutaka kupata mafanikio kama yaliyofikiwa kwa Hasheem Thabeet.
Aliongeza kuwa Tanzani kuna vijana wengi wenye sifa ya uchezaji kikapu kinachotakiwa sasa ni mchango wa wadau wa habari ambao tayari wengine wameonyesha ili kliniki mbalimbali za kuwabaini wachezaji zinapofanyika kutoa mwamko kwa watoto na Vijana kujitokeza.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment