Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola imekabidhi vifaa vitakavyotumika kwenye mashindano ya Copa Coca Cola ngazi ya wilaya yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 16 mwezi huu wa Machi, 2010.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo menejea masoko wa Coca Cola Tanzania Herieti Mutayoba, amesema vifaa hivyo tayari wamekwisahaanza kuvisambaza katika mikoa mbali mbali nchini kupitia TFF.
Vifaa hivyo ni pamoja na Fulana, mipira na Bibs kwa ajili ya mazoezi.
"Hivi sasa zoezi la kusajili vijana watakaounda timu za Copa Coca Cola ngazi ya Wilaya linaendelea nchi nzima na ni matumaini yetu kuwa vijana wengi zaidi watajitokeza mwaka huu ili kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na hatimaye kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji bora na kufanikiwa katika maisha kupitia mchezo wa mpira miguu" anasema Herieti Mutayoba, Meneja masoko Tanzania, Coca Cola.
Amesema tayari matunda ya Copa Coca Cola tayari yamekwishaanza kuonekana kufuatia baadhi ya wachezaji kuanza kuonekana katika vilabu vya ligi kuu Tanzania bara na visiwani Zanzibar.Kutoka kulia ni Herieti Mutayoba, katikati Afisa habari wa TFF Florian Kaijage na kushoto ni Salum Madadi Afisa maendeleo wa vijana wa TFF akipokea jezi na vifaa ambavyo vimetolewa na Coca Cola.
Amesema timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 sasa inaundwa na wachezaji toka Copa Coca Cola na kituo cha michezo cha Tanzania Soccer Academy pia kinaundwa na wachezaji toka katika michuano hiyo ya vijana.
"katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kampuni ya Coca Cola imeweza kupeleka vijana kwenye kambi ya kimataifa ya mafunzo ya soka huko Brazil, mwaka 2007 na 2008, na mwaka jana vijana 16 wa Copa Coca Cola walikwenda nchini Afrika Kusini kushiriki michuano ya Copa Coca Cola Afrika" anasema Herieti Mutayoba.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment