MSHAMBULIAJI wa kulipwa wa timu ya Simba, Mganda, Emmanuel Okwi na beki wa kutumainiwa Juma Nyoso wameachwa katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza na Lengthens FC Machi 19 jijini Harare.
Simba imeondoka leo alfariji kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya ikiwa na msafara wa watu 25, ambapo wachezaji ni 19 na viongozi sita kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho CAF dhidi ya Wazambabwe hao.
Akizungumza Dar es Salaam, Ofisa Habari wa timu hiyo, Cliford Ndimbo alisema Okwi ameachwa kutokana na kuwa mgonjwa lakini Nyoso hayumo katika orodha hiyo kutokana na nafasi.
"Wachezaji walioachwa si Nyoso na Okwi pekee kwani wapo wachezaji wengine wameachwa kutokana na idadi ya watu ambao wanahudumiwa na wapinzani wetu," alisema Ndimbo.
Ndimbo aliwataja wachezaji wanaokuwa katika msafara huo ni Juma Kaseja, Haruna Shamte, Juma Jabu, Nicco Nyagawa, Kelvin Yondani, Mohamed Banka, Hilary Echessa na Ramadhani Chombo.
Wengine ni Mussa Hassan Mgosi, Mike Barasa, Ulimboka Mwakingwe, Ali Mustapha, Salumu Kanoni, david Naftar, Uhuru Selemani, Jerry Santos, Mohamed Kujuso, Jabir Aziz na Joseph Owino.
Kwa upande wa viongozi watakaoambatana na timu hiyo ni Mwenyekiti Hassan Dalali, Kocha Patrick Phiri na Msaidizi wake Amri Said, Meneja Innocent Njovu, Daktari Cosmas Kapinga, Kassimu Dewji na Mulamu Ng'ambi.
Ndimbo alisema kikosi hicho kinaondoka kikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri kutokana na kufanya maandalizi ya kutosha wa ajili ya michuano hiyo.
Simba wanatarajia kurudi nchini mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo au JUmapili wakitegemea na ratiba ya ndege wanayosafiri nayo.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment