Semina ya soka la wanawake iliyokuwa ikiendelea kwenye makao makuu ya shirikisho la kandanda Tanzania TFF uwanja wa karume imefikia tamati hii leo chini ya mkufunzi wa shirikisho la soka Dunia FIFA.
Akizungumza mara baada ya semina hiyo mkufunzi huyo wa FIFA MONICA STARB amesema wanawake wanaweza wakafanya vizuri katika mchezo wa soka endapop wataendelezwa.
Amesema licha ya nchi nyingi zilizoendelea haziruhusu wanawake kufanya kile wanachokipenda lakini amedai kwa kuendelea wanawake kufanya vizuri kutaendelea kufungua milango.
Ameongeza kuwa ili wanawake milango yao ya mafanikio iweze kufanikiwa wanalazimika kuyatumia vema mafunzo hayo ambayo wameyapata kwa kuinua soka la wanawake Tanzania.
Amesisitiza ni muhimu kuwepo kwa makocha wazuri wanawake lakini pia ukapewa kipaumbele mashuleni na wazazi wakahusishwa katika kuhamisisha mchezo wa soka la wanawake Tanzania.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment