
Luisi Sendeu ni Afisa Habari wa Yanga, amekiri kocha huyo anawadai mshahara wa mwezi mmoja lakini amewataka mashabiki kusubiri makubaliano watakayoyafikia na uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imechapipshwa na magazeti leo, Papic amebainisha kwamba amechoshwa na vitendo anavyofanyiwa na Uongozi wa klabu ya Yanga ikiwa ni pamoja na kutompatia malipo yake kwa wakati, jambo ambalo limekuwa likimfanya atumiwe fedha toka Serbia badala ya mshahara ambao anastahili kupata.
Aidha Papic amesema hapewi heshima anayostahili na viongozi wa klabu ya Yanga jambo ambalo anahisi kama wanamdharau na ndiyo maana wanamnyanyasa licha ya kuibadili Yanga na kucheza soka bora.
No comments :
Post a Comment