Waandaji wa tuzo za CAF za mwaka wamewasili Mjini Accra, Ghana tayari kwa maandalizi ya tuzo za mwaka huu ambazo zitafanyika siku ya Alhamisi, March 11 huko Banquet Hall, mjini Accra.
Timu ya watu 115 toka Afrika Kusini ikiwa ni waandaaji wakiwa na kampuni ya True Colours Event tayari kuhakikisha sherehe hizo kubwa za kuwatunuku waliyotamba Afrika katika ulimwengu wa soka, wachezaji, makocha na wote wanaohusika mambo yankwenda safi.
Kampuni hiyo toka Afrika Kusini inarekodi nzuri ya kuandaa matamasha makubwa na yenye kufanya nsana takriban 48.
Bobby Scott, Mkurugenzi wa True Colour Events amesema wametua na vifaa mbali mbali kwa ajili ya hafla hiyo ikiwa ni pamoja na Jukwaa, Taa, Mziki, AV, trussing, furniture, draping, décor elements, Meza na viti, Bedouin tents, vifaa vya huduma ya kwanza, cabling, outboards, sound desks, monitors na generators.
Katika Burudani, kunatarajiwa kuhudhuriwa na wasanii mashuhuri katika kupamba utoaji wa tuzo hizo, miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na P-Square toka Nigeria, Ishmael Lo wa Senegal na Kwabena Kwabena wa Ghana.
Kiungo wa Ghana Michael Essien, mchezaji mwenzake wa Chelsea Didier Drogba wa Ivory Cost na mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto’o ndiyo ambao wanawania tuzo hiyo ya mwanasoka bora wa Afrika wa mwaka 2009 (CAF African Footballer Year 2009 award).
Essien ndiyo mchezaji pekee ambaye hajawahi kutwa tuzo hiyo, wakati Etto’o tayari amekwisha twa tuzo hiyo mwaka 2003, 2004 na 2005, na Drogba amewahi kutwaa tuzo hiyo mwaka 2006.
Kampuni ya simu za mkononi ya Globacom ndiyo wadhamini wa tuzo hizo.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment