
Timu ya taifa ya Argentina ambayo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 walipocheza na Ujerumani, sasa kocha Carlos Alberto Parreira atakuwa na kibarua kuwakabili wa Argentina hao ambao wananolewa na nyota wa zamani wa kandanda Dunia Diego Armando Maradona.

Parreira amedai amekuwa akifurahishwa na maendeleo mazuri ya vijana wanaounda timu ya taifa ya Afrika Kusini.
Kocha huyo amesema alikwishamwambia CEO Leslie Sedibe kwamba anahitaji timu ngumu kama vile Denmark na Argentina, na siyo timu ndogo ambazo haziwezi kumsaidia kubaini mapungufu.

Argentina imepangwa kundi moja na Nigeria, Jamhuri ya Korea na Ugiriki katika kundi B na itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Nigeria June 12.
Bafana Bafana pia imepanga kucheza mchezo miwngine wa kirafiki dhidi ya Denmark hapo June 5 – siku tano kabla kushuka dimbani katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa fainali za Dunia ambapo watafungua na Mexico katika dimba la Soccer City hapo June 11.
No comments :
Post a Comment