
Azam FC ikiwa na pointi 31 itakuwa na wakati mzuri wa kushinda mchezo huo ili kukaa vyema katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi, huku Simba wakiwa na salio la pointi mbili kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi hiyo wanaitaji ushindi wa hali na mali.
Kocha wa Azam FC Itamar Amorin amesema kikosi chake kipo sawa kuikabili Simba SC na kutoipa nafasi ya kuwa mabingwa kupitia Azam FC.
Amesema "Simba ni timu ngumu na nzuri natarajia kikosi changu kitaleta upinzani mkubwa na kuondoka na ushindi katika mechi hiyo".

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Azam FC walipoteza mchezo huo kwa kukubali kufungwa goli 1-0 katik amchezo wa tisa wa ligi uliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo klabu ya Simba ambayo ilikuwa imeweka kambi visiwani Zanzibar imerejea leo jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo huo hapo kesho.
Golikipa nambari moja wa Simba Juma Kaseja amesema kwa maandalizi waliyoyafanya wanaamini kesho wanaingia uwanjani kwa lengo moja tu la kutaka kutawazwa mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kuizaba Azam FC."kaka unakumbuka katika mzunguko wa kwanza tulitokea Zanzibar kula marashi ya karafuu tukawafunga Azam na kesho watake wasitake lazima walowe tusherehekee ubingwa bwana" anasema kaseja.
Simba ambayo inaongoza ligi kuu Tanzania Bara ikiwa na jumla ya Pointi 53 inahitaji poitni mbili tu iweze kutangaza ubingwa.
No comments :
Post a Comment