BARAZA la wadhamini wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam limeulima barua uongozi wa klabu hiyo, likiuagiza kufanya mambo mbalimbali ili kuboresha klabu hiyo ukiwemo Mkutano Mkuu ndani ya siku 14 tangu Ijumaa iliyopita.
Kwa mujibu barua ambayo baraza hilo limemwandikia Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Imam Madega na kunaswa na vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na gazeti la majeri na Radio Times FM 100.5 hili kufanikiwa kunasa nakala yake, baraza hilo linamtaka kuitisha huo mkutano huo, ili kufanya marekebisho ndani ya Katiba kama inavyotakiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Baraza hilo limesema kuwa ni lazima mkutano huo ufanyike ndani ya siku 14 na mapendekezo ya mabadiliko ndani ya katiba ni lazima yatangazwe hadharani kwa muda wa wiki moja, kabla ya kuidhinisha, ili kuweza kuwashirikisha wanachama katika kuamua jambo hilo.
"Na baada ya marekebisho kupitishwa unapaswa kuyafuata na kuyaingiza ndani ya katiba haraka iwezekanavyo na inapaswa kufahamu kazi hii, inatakiwa isichukue muda zaidi ya wiki mbili," ilielza sehemu ya barua hiyo.
Mbali na Mkutano Mkuu na marekebisho ya katiba, baraza hilo limemwagiza Katibu Mkuu na Kamatai yake ya Sekeretarieti kuhakikisha inawakilisha ripoti ya kumbukumbu za mahesabu zilizohakikiwa katika kipindi chote cha uongozi wa mwenyekiti huyo.
Pia baraza hilo limemtaka Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Kostadin Papic kuandaa taarifa za kipindi atakachokuwa ameionoa klabu hiyo, ili kuepukana na tatizo kama la kocha aliyefundisha timu hiyo msimu uliopita na kisha kuondoka bila kuandika taarifa.
"Kwa uwezo wangu kama mdhamini, nitahitaji nakala ya ripoti zote kuwakilishwa katika Baraza la Wadhamini, pamoja na ajenda zake walau siku saba kabla, ili niweze kufanya tathimini kama mdhamini wa Yanga," ilieleza barua hiyo.
Barua hiyo ambayo ilisainiwa na mmoja wa wajumbe wa baraza hilo, ilieleza kuwa endapo mambo hayo yatakuwa yameenda kama inavyotakiwa, wanatarajia watakuwa wamepokea taarifa hizo Juampili ya Aprili 24, mwaka huu ambayo itakuwa ni muda wa wiki moja, baada ya mechi yao ya mwisho ya ligi.
Wadhamni hao pia wamemwagiza mwenyekiti, kuandaa taarifa muhimu katika magazeti na vyombo mbalimbali vya habari siku moja baada ya mkutano wa mabadiliko ya katiba kumalizika.
Katika barua hiyo wadhamini hao walisema endapo kutakuwepo masuala mengine yanayohitajika kupatiwa ufumbuzi, ili kuhakikisha Baraza la Wadhamni na Uchaguzi Mkuu unafanyika kama vile kuchagua kamati itakayoshughulikia uchaguzi itabidi yapatiwe ufumbuzi katika muda unaotakiwa.
Aidha michezo na Times FM ilifainikiwa kuzungumza na mwenyekiti wa Yanga Imani Madega ambaye amesema Baraza la wadhamini wa klabu hiyo halikuisoma vema katiba ya klabu hiyo na kusema kazi ya wadhamini katika klabu ni kusimamia masuala ya fedha.
Madega amesema hakuna chombo chochote katika klabu ya Yanga ambacho kitatoa maamuzi yeyote ya nini kifanyike kwa maana shughuli za kila ssiku za klabu ya Yanga zaidi ya mwenyekiti.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment