BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini Msondo Music bendi inatarajia kufanya ziara ya utambulisho wa albam yao mpya ya huna shukrani Mkoani Tanga mapema mwezi huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema sambamba na kutambulisha albamu hiyo pia ziara hiyo ni maalum kwa ajili ya kutakiana kheri ya mwaka mpya ikiwa ni pamoja na kusheherekea sikukuu ya wapendanao na wakazi wa Jiji hilo.
Alisema katika sherehe hizo mashabiki watapata nyimbo mpya ambazo wamezitunga kwa ajili ya alabamu yao mpya ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na zile zilizopo katika albamu hiyo ya Hunashukurani huku ikisindikizwa na nyimbo zilizotamba katika miaka ya nyuma.
Alizitaja nyimbo hizo mbili mpya kuwa ni Lipi jema uliotungwa na Eddo Sanga na Dawa ya deni kulipa uliotungwa na Isihaka Katima 'dj papa upanga' ambao umefanyiwa kazi na kukamilika ambapo itakuwa ni zawadi kwa wakazi wa mkoa huo.
Aidha aliwataja wanenguaji watakaokuwa wanatoa burudani katika safu hiyo kuwa ni Amina Said 'quen Emmy' Nacho Mpendu 'mama Nzawisa' na Amiri Saidi 'Dongo' aidha rapa wa bendi hiyo Romani Mng'ande 'Romario' atawachenguwa mashabiki watakaofika katika onesho hilo wakiongonzwa na mkurugenzi wa bendi hiyo Muhidini Gurumo,na kiongozi wa bendi hiyo Saidi Mabela.
No comments :
Post a Comment