1. MAREKEBISHO YA KATIBA ZA WANACHAMA
Kama inavyofahamika TFF iliagiza wanachama wake wote kukamilisha marekebisho ya katiba zao kulingana na maelezo yaliyotolewa na TFF. Wanachama wote wa TFF(Vyama vya mpira wa miguu vya Mikoa, klabu za ligi kuu na vyama shiriki).TFF iliweka tarehe 15 februari 2010 kuwa mwisho wa wanachama wote kuwasilisha marekebisho ya katiba zao ili TFF iweze kuyapitia marekebisho hayo na haomaye kukamilisha zoezi zima ifikapo februari 28, 2010.Hata hivyo kazi ya wanachama kuwasilisha marekebisho ya katiba zao imekuwa si nzuri na kwahiyo TFF imeona ni vema kuongeza muda wa juma moja (siku saba (7) hadi tarehe 22 Februari 2010.
Kwa nyongeza hii ya muda wa kuwasilisha marekebisho ya katiba inamaana kuwa mwanachama yeyote ambaye hata kamilisha ndani ya muda huo, hataweza kuhudhuria mkutano mkuu wa TFF utakaofanyika Februari 27 na 28, 2010.
wanachama waliyowasilisha hadi sasa ni kama ifuatavyo:
Mkoa: Mwanza, Mara, Morogoro na Tanga.
KLabu za ligi kuu: Tanzania Prisons, Simba SC, Azam FC, Majimaji, Ruvu Stars JKT.
Vyama shiriki: Hakuna.
2. TIMU YA TAIFA - TWIGA STARS
Timu ya taifa - Twiga Stars inakabiliwa na mashindano ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wanawake zitakazofanyika Afrika Kusini baadae mwaka huu.
Twiga Stars imepangwa kuanza kampeni yake ya kufuzu kwa fainali hizo za Afrika kwa kupambana na Ethiopia kati ya tarehe 5-7 Machi 2010, katika mchezo utakaochezwa huko Ethiopia na baadaye kurudiana majuma mawili baadaye. Iwapo itafaulu kuitoa Ethiopia, Twiga Stars itacheza na mshindi kati ya Kenya na Eritrea baadaye Mei 2010.
Twiga Stars imeingia kambini siku ya Jumatatu Februari 15, 2010. Twiga Stars itakuwa chini ya kocha Charles Boniface na Adolf Rishard na kambi imeweka katika hoteli ya Lamada, Ilala Dar es Salaam huku mazoezi wakifanya katika uwanja wa KArume.
Gharama zote za Kambi na safari ni zaidi ya shilingi milioni 70. Kama inavyofahamika Twiga Stars haina mdhamini. Kwa hali hiyo TFF inajitahidi kutafuta fedha kutoka sehemu mbali mbali ikiwemo kwa wadau na jamii kwa ujumla.
Tunapenda kutumia Fursa hii kwa jamii nzima ya mpira wa miguu kuisaidia Twiga Stars ili iweze kushiriki kikamilifu katika michezo ya kufuzu.
Kutokana na majukumu ya Twiga Stars mashindano ya timu za mikoa za wanawake yaliyokuwa yafanyike kuanzia katikati mwa Februari yameahirishwa hadi itakapotangazwa tena.
3. MTIHANI WA UWAKALA WA WACHEZAJI
Mtihani wa uwakala wa wachezaji uttafanyika Alhamisi April 15, 2010 saa nne Asubuhi.
waombaji wa mtihani huo wanapaswa:
Kuwasilisha barua ya maombi TFF
Kuwa na elimu isiyopungua kidato cha nne
Aeleze ushiriki wake katika masuala ya Mpira
Ada ya Dola za marekani 50.
4. TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA 2010 AFRIKA KUSINI
TFF imekwishawasilisha maombi ya tiketi kwenye ofisi inayoshughulikia tiketi za kombe la Dunia.
Jumla ya tiketi ambazo Tanzania imepangiwa kama moja ya nchi ambazo timu zake hazishiriki ni 290.
Hata hivyo maombi ya tiketi yanazidi idadi ya tiketi ambayo Tanzania imepangiwa. Kwa hiyo TFF imewasilisha maombi kwa FIFA kwa ajili ya kupata nyongeza ya tiketi.
Kwa upande wa tiketi 290, kinachosubiriwa sasa ni invoice ya FIFA ili waliyoomba waweze kulipia tiketi zao. Kulingana na utaratibu wa FIFA ni kwamba waombaji wote watatakiwa kulipia tiketi zao ndani ya siku 10 tangu siku TFF itakapopokea invoice.
Fredrick Mwakalebela
KATIBU MKUU - TFF
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment