Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, April 24, 2012

MSHINDI WA DROO YA M-PESA AKABIDHIWA SHILINGI MILIONI 10



Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania  Bw. Rene Meza (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika hafla fupi ya kukabidhi fedha kwa mshindi wa pili wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya  M-pesa  Bw. Revocatus Mkama (kulia) anaejishughulisha na ufundi wa magari jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza (kushoto) akimkabidhi mshindi wa pili wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya M-pesa Bw. Revocatus Mkama (kulia) fedha taslimu shilingi milioni kumi  katika hafla fupi iliyofanyika katika Makao makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini dar es salaam.
Mshindi wa pili wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya M-pesa Bw. Revocatus Mkama ambaye pia ni mkazi wa Mwanza anayejishughulisha na ufundi wa magari akifurahia kitita cha shilingi milioni kumi alizoshinda kupitia promosheni ya M-pesa mara baada ya kukabidhiwa fedha hizo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza.


Mshindi wa pili wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya M-Pesa Bw. Revocatus Mkama leo amekabidhiwa kitita chake cha Shilingi 10 Milioni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza amempongeza mshindi huyo wakati akikambidhi kitita chake hicho kufuatia kuibuka mshindi katika droo ya Aprili iliyochezeshwa hivi karibuni. “Ninajisikia furaha kubwa kukukabidhi fedha hizi ulizoshinda ikiwa ni matunda ya kutumia hudiuma ya ”Alismea Bw. Rene.
“Wewe ni mteja mwenye bahati kubwa miongoni mwa mamilioni ya wateja wa Vodacom M-Pesa, nakupongeza sana na tunaimani kwamba fedha hizi zitakusaidia kubadili maisha yako kiuchumi.” “Azma yetu, tunataka kuona kwamba kila mmoja ana mudu kutumia huduma hii na huku wateja wetu wakiwezeshwa kadri watumiavyo huduma waipendayo ya M-Pesa”Aliongeza Bw. Rene
Hadi kufikia leo, zaidi ya wateja 7000 wameshajishindia jumla ya shilingi Milioni 370 wakiwemo washindi wawili wa droo ya mwezi. “Matumizi ya M-Pesa yameongezeka sana tangu kuanza kwa promosheni hii, tumeshusha gharama za huduyma hiyo na watu waendelee kutumia huduma hii bora na wawezeshwe.”Aliongeza Bw. Rene
Huduma ya Vodacom M-Pesa ndio huduma inayoongoza soko katika huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi ikiwa na mtandao mpana zaidi wa mawakala zaidi ya 20,000 nchi nzima. “Udhati wetu katika kuhakikisha huduma hii inaendelea kuwa bora, salama, ya uhakika na zaidi yenye gharama nafuu kwa watu wote bila kujali uwezo wa kiuchumi bado ipo pale pale.”Amesisitiza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene.
Kwa upande wake Bw. Mkama ambae ni mkazi wa Mwanza anaejishughulisha na ufundi wa magari jijini humo pamoja na kuishukuru Vodacom pia ameipongeza kwa kuleta huduma bora inayowawezesha watanzania kufanya miamala kupitia simu za mkononi.
“Hakuna shaka yoyote kwamba huduma ya Vodacom M-Pesa inaongoza soko na inatumiwa na wananchi walio wengi kama sio kutuma basi kupokea fedha, na hii imeipeleka nchi mbele katika matumizi ya teknolojia ya simu ya mkononi.”Alisem,a Bw. Mkama
Bw. Mkama ni mshindi wa pili droo hiyo, wa kwanza alikuwa Konstebo wa Polisi James Peter Mlalo, aliyeibuka mshindi katika droo ya Machi mwaka huu.
Ili kuwa katika nafasi ya kushinda shilingi 50,000 kila siku , mteja wa Vodacom anatakiwa kutumia huduma ya M-Pesa. Kadri mteja anavyoitumia huduma hiyo ndivyo anavyojiweka katika nafasi ya kushinda zawadi ya kila siku na ile ya mwezi.
Kupitia huduma ya M-Pesa mtu huweza kutuma na kupokea pesa, kulipia na kununua gharama mbalimbali ikiwemo LUKU, DAWASCO,DSTV, Pia huduma ya M-Pesa hutumika kutoa na kuweka fedha katika akaunti ya mteja iliyo katika benki ya CRDB, kununua tiketi za safari za ndege za Precision Air, Coastal n.k

No comments :

Post a Comment