Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, April 22, 2012

ZIARA YA KATIBU MKUU KIONGOZI ALIPOTEMBELEA JENGO LA BUNGE MJINI DODOMA JANA


 Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah, (wa pili kushoto) akimuongoza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, wakati akiingia mjengoni Bungeni kwa Waheshimiwa Wabunge. Balozi Sefue jana alifanya ziara ya kutembelea jengo hilo la Bunge.
 Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah akimuonesha katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue sehemu za kukaa maofisa wa Serikali ndani ya Ukumbi wa Bunge kipindi wawapo ndani ya ukumbi huo kusikiliza hoja mbalimbali zinazohusu Wizara zao.
  Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah akimuonesha katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue mtambo wa kudhibiti vipaza sauti pamoja na picha za video Bungeni.
 Mtaalamu wa mitambo ya Sauti na Picha kutoka Ofisi ya Bunge, Lemo Toluwe, akimpa maelezo Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ya namna mitambo hiyo inavyofanya kazi Bungeni.
  Mhandisi wa umeme kutoka Wakala wa Majengo wa Seriikali, Hijja Mrutu, akitoa maelezo juu ya namna mitambo ya kufua Umeme Bungeni inavyofanya kazi.
 . Patson Sobha 'MCHUNGAJI' kutoka Idara ya Hansard, Bungeni akitoa maelezo kwa Balozi Sefue ya namna Hansard inavyoandaliwa baada ya kunasa sauti za majadiliano Bungeni.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akifurahia mitambo ya kisasa ya kunasa picha za matukio yote katika viwanja vya Bunge.
Naibu waziri wa Miundombinu Mhe. Harrison Mwakyembe, akimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue walipo kutana Bungeni juzi.

No comments :

Post a Comment