Deidre Lorenz akimkabidhi picha ya Ground
Zero (New York) Rais wa Mt. Kili Marathon 1991 Onesmo Ngowi baada ya
kukimbia mbio hizo.
Deidre Lorenz akiwa anahojiwa na waandishi wa Habari mjini Moshi.
---
Na Grace Soka, Afisa Uhusiano
MT. KILIMANJARO MARATHON 1991
Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre
Lorenz ameahidi kuleta wacheza sinema wenzake na kushiriki kwenye mbio
za mwaka kesho za mt. Kilimanjaro Marathon zitakazokuwa zinatimiza miaka
23 tangu zianzishwe mwaka 1991.
Lorenz aliyekimbia mbio za mwaka huu
ambazo zilipewa jina la “mbio za kutimiza miaka 50 ya uhuru wa
Tanganyika” na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) amesema kuwa atakuja na
timu yake ya wapiga picha ili kupiga picha vivutio kadhaa vya Tanzania
ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro. Qwiji hili la sinema za Santorini
Blue, The Great Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi ameelezea
kuipenda sana Tanzania.
“Sikutegemea kuikuta nchi nzuri kama hii”
alisema mcheza sinema huyo ambaye ameshawahi kuchaguliwa zaidi ya mara 4
kugombea tuzo maarufu za Oscar. “Sasa nimeamini kuwa mlima Kilimanjaro
ni mali ya Tanzania na nitautangaza katika sinema zangu zote” aliendelea
kusema Deidre Lorenz.
Mcheza sinema huyu ambaye ameingia kwenye
mkataba na kampuni kubwa ya Google hivi karibuni ili kuuza sinema zake
katika mtandao aliielezea Tanzania kama nchi nzuri na yenye watu
wakarimu sana.
Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon
zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances anayetoka katika jiji la
matajiri la Bethesda nchini Marekani baada ya kuombwa na balozi wa
zamani wa Tanzania nchini Misri. Tangu kuanzishwa kwake mbio hizi
zimekuwa zinaleta watalii matajiri katika mji wa Moshi kupanda mlima
Kilimanjaro na kukimbia mbio hizi zinazojulikana kama Seven Continental
Races.
Hakuna masharti yote ya kukimbia mbio hizi na watanzania wanaoshiriki katika mbio hizi huwa hawatozwi pesa za kiingilio.
Kwa kutambua mchango wake katika uchumi
wake Manispaa ya Moshi iliibadilisha jina barabara ya zamani ya Bustani
Ale na kuiita Marie Frances Boulevard ili kumuenzi mama huyu
aliyejitolea maisha yake kuutangaza mlima Kilimanjaro.
“Kila siku napokea ujumbe kutoka nchi
mbalimbali niende huko kuanzisha mbio za marathon lakini kwa sasa basi”
alisema mama huyo aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi vya televisheni ya
ABC kabla ya kunzisha Mt. Kilimanjaro Marathon.
Alisema kuwa mwaka jana yeye na Rais wa
klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon mtanzania Onesmo Ngowi walifanya
makubaliano ya Ethiopia Airlines (ET) jijini Addis Ababa kuzifanya mbio
hizo kuwa za kimataifa zaidi. “ET walikubali kutoa ufadhili kwetu na pia
kugharamia kushiriki kwetu katika mbio za New York Marathon, Boston
Marathon na Los Angelos Maratthon ili kuitangaza vyema Tanznaia”
alibainisha Frances.
Katika makubaliano hayo, Ngowi na Frances
pia wataanzisha mbio za “King Solomon Marathon” zitakazofanyika katika
jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.
Deidee Lorenz amefungua pazia kwa watu
mashuhuri kushiriki katika mbio za marathon nchini Tanzania na ni jukumu
la Watanzania kuchangamkia fursa zinazoletwa na ujio wao.