| ||
| Kila mmoja akitaka kushuhudia kila kitu kinachoendelea na hataki kuhadithiwa basi kubana nako ni sehemu ya burudani hivyo ndivyo ilivyokuwa kwenye tamasha hilo. |
Hapa maji yakazidi unga walianza kusukuma watu
wanyuuuma abisa hapa wimbi la msukumano ndio linaishia yani ilikuwa kama
maji baharini yanavyofanya mawimbi na watu walikuwa vivyo hivyo.
|
| Sasa baada ya watu kutulia hapa anafanya vitu vyake. |
| Lakini punde tu mkanyagano ukaanza tena. |
| Hapa Kijana wa TMK Juma Kassim Kiroboto AKA Juma Nature, akikamua vilivyo kwenye tamasha hilo na kusababisha mashabiki kumng'ang'ania asishuke aendelee kutumbuiza. |
| Farid Kubanda Fid Q, nae alikuwa semu ya burudani hiyo. |
| Profesa J, Wamitulinga Mchawi wa Rymes, nae hakujivunga ilimradi ni burudani na shwangwe mwanzo mwisho shoo ilianza saa 6:00 mchana hadi 12:00 jioni yani furahaaaaaaa teeeele. |
| Mzee wa kuongea na Mshua Eazy Busyness nae alipakua vitu vyake kwa mashabiki wake na hakuwaangusha kabisa aliwakilisha vilivyo tu. |
| Mzee wa kamua baba kamua baaaaaa, kamua baba usitumie iliziiiiii! |
| Mkanyagano ukaanza tena upyaaaaa. |
| Lakini pia walikuwepo waliopanda juu ya minazi ili washuhudie. |
| Roma Mkatoliki nae alikuwepo kwenye kimuhemuhe hiko na aliwakilisha vilivyo hakuwaangusha mashabiki wake. |
No comments :
Post a Comment