Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, October 25, 2009

WATEJA WA VODACOM KUONGEA BURE KUPITIA CHEKA TIME

mkuu wa kitengo cha udhamini wa Vodacom George Rwehumbiza, mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa Boniface Emmanuel, mkuu wa mawasiliano Vodacom Mwamvita Makamba na Ofisa bidhaa wa Vodacom Elihuruma Ngowi wakiwa wameshikilia vipeperushi katika uzinduzi wa huduma ya CHEKA TIME ambapo mteja wa Vodacom atakatwa shilingi 500 na kuweza kupiga simu dakika 60.Ili mteja aweze kupata huduma hiyo atalazimika kujiunga kwa kupiga *147# na mteja anaweza kujisajili mara nyingi ili aweze kupata muda wa maengezi kadri atakavyo.
Huduma hii imezinduliwa jijini Dar es Salaam leo.Picha na Rajabu Mhamila a.k.a Super D

KOMBE LA DUNIA U-17 NIGERIA 3-3 UJERUMANI

Wenyeji na mabingwa watetezi Nigeria wamemaliza mchezo wao na mabingwa wa Ulaya Ujeruamni kwa kutoka sare ya goli 3-3 katika mchezo wa ufunguzi wa fainali za Dunia chini ya Umri wa miaka 17.
Ujerumani iliwachukua dakika 22 kupata goli kupitia kwa mchezaji Lennart Thy na kuwanyamazisha mashabiki wa Nigeria.
Kama haitoshi dakika 16 baadaye waliongeza goli la pili kupitia kwa mchezaji Shkodran Mustafi.
Timu zote zilirejea uwanjani kwa kasi, lakini ilikuwa ni Ujerumani ambayo ilipata nafasi tena ya kufunga goli la tatu kupitia kwa mchezaji Mario Goetze na kufanya matokeo kuwa 3-0 katika dakika ya 47.
Mpira ulianza kugeuka kwa mabingwa watetezi kunako dakika ya 53 wakati Robert Labus alipompenyezea mpira Omoh Ojabu katika eneo la penati, na kupata penati na kupata goli la kwanza, kupitia kwa mchezaji Stanley Okoro katika dakika 54 wakati mchezaji Kenneth Omeruo akifunga goli la pili dakika tano baadaye.
Mchezaji aliyeingia kipindi cha pili Edafe Egbedi alifunga goli la tatu katika dakika ya 61 na kuwalazimu kugawana popinti.
Argentina sasa inaongoza kundi A baada ya kuichapa Honduras 1-0.
na katika kundi B Switzerland iliichapa Mexico 2-0.

Saturday, October 24, 2009

LIVERPOOL v/s MANCHESTER UTD

Majogoo wa Jiji la London Liverpool wanawaalika Mashetani Wekundu Manchester United huko Anfield katika mtanange uliona gumzo kubwa katika medani ya soka Duniani.
HABARI ZA TIMU
Fernando Torres wa Liverpool ana matumaini ya kurejea Dimbani.
Glen Johnson anataraji kurejea pia lakini Injini ya Liverpool Steven Gerrard inakimbizana na muda ili kuweza kuwa kamili kutokana na majeraha.
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amelalalma kuwa uenda akamkosa Wayne Rooney ambaye anakimbizana na Muda.
Rooney amekosa michezo miwili kutokana na kusumbuliwa na kifua, Darren Fletcher (Nyonga) yupo njiapanda huku Ryan Giggs na Patrice Evra watarejea Dimbani.
Liverpool imeifunga Manchester United nyumbani na ugenini katika msimu uliopita kwa mara ya kwanza tangu kupita miaka 7. Ushindi mkubwa ulikuwa wa 4-1 huko Old Trafford ulikuwa mzito kupewa United nyumbani kwao tangu mwaka mpya 1992.
Manchester United wameshinda mitanange 5 na suluhu 1 katika michezo 7 ya Ligi waliyocheza huko Anfield..
United wana rekodi nzuri kwa Liverpool kuliko timu yoyote ye Ligi kuu ya England wakiwa wameishinda michezo 18 na kupata pointi 61.
Liverpool
• Liverpool wamepoteza mitanange 4 muhimu katika mshindano makubwa dhidi ya Manchester United.
• Liverpool wamefunga magoli 15 kwa michezo 4 ya ligi waliyocheza Anfield kwa msimu huu.
Manchester United• katika michezo ya Ulaya na Ligi Manchester United wamechomoza mara 10 suluhu 1 katika michezo 11 waliyocheza.
• Ryan Giggs amefunga magoli 99 katika Ligi ya England huku Paul Scholes amefunga magoli 98 kwa Manchester United.
• Michael Carrick kama atateremka Dimbani atakuwa akicheza mchezo wake wa 100 wa Ligi kuu akiwa na Manchester United huku Patrice Evra na Dimitar Berbatov watakuwa wakicheza mchezo wa 100 tangu kucheza mechi za Premier League .
Fernando Torres wa Liverpool amefunga magoli 8 yote katika Ligi kuu ya England ,Kuyt amefunga magoli 4 huku mabao 3 wakiwa ni ya Ligi kuu ya England.
Kwa upande wa Manchester United Rooney ana Magoli 7 huku 6 yakiwa ni ya Ligi huku Berbatov ana magoli 3.
Katika mtanange wa hivi karibuni baaina ya Vigogo hao wawili March 14 mwaka huu Liverpool waliizaba Man Utd 4-1 magoli ya Liverpool yalifungwa na : Torres (28) Gerrard (44) kwa Tuta, Aurelio (77), Dossena (90), huku bao la kufutia machozi kwa Manchester United lilifungwa kwa njia ya Tuta na Christiano Ronaldo dakika ya 23.
Bolton Wanderer v Everton (13:30)
Hakuna majeruhi mpya katika kikosi cha Bolton ambacho kinanolewa na Gary Megson, ingawa Andy O'Brien (groin), Sean Davis (knee) na Johan Elmander (hamstring) wataendelea kukalia benchi.
Everton itamkaribisha tena uwanjani Steven Pienaar ambaye alikuwa akiuguza goti, lakini Phil Neville, Phil Jagielka, Victor Anichebe na Mikel Arteta wataendeleza kuwa nje. Leighton Baines (calf) anatiliwa mashaka, lakini Joseph Yobo atalazimika kurejea uwanjani.
Manchester City v Fulham
Robinho atakuwa tena nje kwa wiki mbili zaidi kufuatia kuumia Enka lakini Craig Bellamy atarejea. Kolo Toure anakimbizana na muda kuwa fit na Vincent Kompany atakuwapo kikosini Pablo Zabaleta yupo kolokoloni kufuatia kadi nyekundu aliyopewa wiki iliyopita.
Fulham watawakosa Danny Murphy(knee), Simon Davies (ankle), Dickson Etuhu (knee) and Andy Johnson (shoulder). Kagisho Dikgacoi anaendelea kutumikia adhabu ya kufungiwa.
West Ham United v Arsenal (16:15)
Wagonga Nyundo wa London West Ham wapo fit huku wakimkaribisha Kapteni wao Scott Parker aliyerejea kutoka korolokoloni ya soka.
Mshambulizi Eduardo anakimbizana na muda kuwa kamili Nicklas Bendtner yupo 50-50 katika kikosi cha Arsene Wenger. Theo Walcott ,Denilson na Johan Djourou wataendelea kusugua Benchi kutokana na majereha. Lukasz Fabianski na Samir Nasri watarejea uwanjani huku wakimkosa Tomas Rosicky watakapokuwa huko Upton Park.

YANGA NAE KUTUPA KARATA JUMAPILI HII

Ligi kuu Tanzania bara itaendelea jumapili kwa mchezo mmoja utakaopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kati ya mabingwa watetezi Yanga na Moro United.
Klabu ya Yanga imetamba kuhakikisha inaibuka na ushindi hapo kesho kufuatia kuongezewa mbinu mpya na kocha Kostadin Papic.
Afisa Habari wa Yanga Luis Sendeu amesema Yanga inakila sababu ya kuhakikisha inashinda mchezo wake wa kesho kwani wanautumia kuwa ni sehemu ya maandalizi ya kumzamisha mnyama Simba.
Yanga hadi hivi sasa imejikusanyia jumla ya pointi 15 ikishika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.
Naye kocha wa Moro United Juma Mwambusi ametamba kuibuka na ushindi dhidi ya klabu ya Yanga kwani wanahitaji pointi zaidi ili kuchumpa kileleni mwa msimamo wa ligi.
Mwambusi amesema anauhakika wataifunga Yanga kwani msimu huu haoni kama inatisha na kuifananisha na nyanya.

SIMBA MBELE KWA MBELE

Mnyama anaetisha mwituni pengine kuliko wanyama wote Simba ameendeleza makali ya makucha yake baada ya kuizaba klabu ya lambalamba wa Azam bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliyochezwa leo katika uwanja wa Uhuru.
Goli hilo la dhahabu lilipatikana katika dakika ya 24 ikiwa ni goli la kujifunga kufuatia mpira wa kona uliyopigwa na Hillary Echesa na kumgonga Henry Morris katika kipindi cha kwanza.
Hata hivyo klabu ya Simba imeondoka muda mchache baada ya kumalizika kwa ndege kurejea visiwani Zanzibar kuendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga hapo Oktoba 31, mchezo utakaochezwa uwanja wa Uhuru.
Simba sasa imefikisha pointi 27 ikiwa ndiyo inaongoza katika ligi kuu Tanzania Bara, ikifuatiwa na Mtibwa yenye Pointi 18.
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA UWANJANI
HUYU NI MGOSI AKIWAJIBIKAHUYU NI HARUNA MOSHI "BOBAN" AKIWATOKA MABEKI WA AZAM FCHEBU MDAU NAWEWE SEMA SASA HUYU ANAMSHIKA WAPI MWENZIYE?JAMAA BADO KANG`ANG`ANIA HAPO HAPO TU...!!!

IVO MAPUNDA AUAGA UKAPELA

Mchezaji wa Zamani wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars) Ivo Mapunda akimlisha kipande cha Keki mke wake Bi.Elizabeth Madale kwenye ukumbi wa Golden Resort Sinza Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumamosi.Harusi ilifungwa katika Kanisa Katoliki Kurasini.Mwanamuziki wa siku nyingi hapa nchini Ramadhani Massanja Banza Stone na mwimbaji Hasasani mabele wakiimba wakati wa harusi ya mwanamichezo Ivo Mapunda kwenye ukumbi wa Golden Resort Dar es Salaam.

TABLE TENNIS WAJIPANGA MASHINDANO YA KIMATAIFA

Katika kuhakikisha mchezo wa mpira wa Meza unakuwa hapa Nchini Chama cha mchezo huo TTTA kipo kwenye mchakato wa kujenga Meza kwa kutumia Saruji katika Shule za msingi za hapa Nchini ili kuukuza mchezo huo.
Akizungumza na kipindi cha michezo cha Radio Times fm Katibu Mkuu wa chama cha mpira wa Meza Tanzania Issa Mtaraso amesema mbali na jitihada hizo ambazo wanazo lakini wapo katika mikakati ya kushiriki mashindano mbalimbali Nje na ndani ya Nchi.

VINYOYA (BADMITON) WAHITAJI MSAADA KUUFUFUA NCHINI

Chama cha mpira wa Vinyoya Tanzania TBA kinawaomba wafadhili mbalimbali wajitokeze kusaidia mchezo huo ambao kwa sasa umeshaanza kupoteza ramani ili uweze kujulikana kama miaka ya nyuma.
Akizungumza na kipindi cha michezo cha Radio Times fm Katibu mkuu wa chama hicho Simon Maganga amesema wanashindwa kuandaa mashindano kutokana na kukosa fedha, na wakati mwingine kushindwa kupelekea hata mshiriki katika masdhindano ya Kimataifa yanayofanyika Nje ya Nchi.
Maganga ameongeza kuwa anatoa nafasi kwa watu wengine kugombea nafasi za kukiongoza chama hicho kwani tangu waanzishe hakuna uchaguzi wowote uliofanyika wa kuchagua Viongozi na anaamini wapo watu wenye uwezo zaidi yake.

Friday, October 23, 2009

SERENGETI YAITAKA TAIFA STARS KUIFUNGA MISRI

Wadhamini wakuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambao ni watengenezaji wa Kinywaji cha Bia ya Serengeti wamesema watashirikiana bega kwa bega kuhakikisha Timu hiyo inawabwaga mafarao wa Misri katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa Novemba 5 mwaka huu Cairo, Misri.
Akizungumza na kipindi cha michezo na burudani cha radio Times FM Afisa uhusiano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda amesema ijapokuwa taarifa ya mwaliko huo wameupata muda mfupi lakini watajitahidi kadri ya uwezo wao kuwapatia mahitaji muhimu wachezaji ili wapate ushindi kwenye mchezo huo.
Mapunda ameongeza kuwa atafurahishwa endapo Timu hiyo ya Misri itakubali mwaliko wa kuja Tanzania, kwani mbali na kuja kucheza lakini watawatembeza kwenye vivutio vyetu ili wajionee.

TENGA - WAAMUZI WALA RUSHWA HAWANA NAFASI

Shirikisho la soka Nchini Tff limesema kwa sasa watakuwa wakali kuhakikisha Waamuzi wanachezesha mpira kwa haki kutokana la suala hilo kuzidi kukithiri katika soka nchini Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Tff Rais wa Shirikisho la kandanda hapa nchini Leodga Chilla Tenga amesema Waamuzi ambao hawatachezesha mpira vizuri watawaondoa.
Aidha amewataka wachezaji kuwajibika uwanjani ili wapate nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Amesema ili mchezaji aweze kupata mafanikio ndani na nje ya nchi nidhamu, juhudi na kutambua wajibu wake katika klabu ndiyo jambo la muhimu.
Utovu wa nidhamu hauwezi kumfikisha mchezaji kokote zaidi kujenga chuki na mwalimu, viongozi na waamuzi uwanjani.

SIMBA VS AZAM FC, MAJIMAJI VS AFRICAN LYON KUKIPIGA JUMAMOSI HII

Ligi kuu Tanzania Bara inataraji kuendelea kesho katika viwanja viwili tofauti, katika uwanja wa Uhuru Mnyama Simba atakuwa mwenyeji wa Azam Fc wakati wanalizombe Majimaji watawaalika Simba wa Afrika, African Lyon katika uwanja wa Majimaji Songea mkoani Ruvuma.
Tukianza kunako uwanja wa Uhuru Mnyama Simba ambaye ameweka kambi huko visiwani Zanzibar anatarajiwa kuwasili jijini kesho asubuhi kwa ndege tayari kwa mchezo huo na kisha kurejea kuendelea na mawindo dhidi ya Yanga hapo Oktoba 31.
Akizungumza na michezo Afisa habari wa klabu ya Simba Cliford Mario Ndimbo amesema wamefikia hatua ya kukodi ndege kufuatia ratiba ya mazoezi ya mwalimu kwa vijana hao wa msimbazi ambao hawajapoteza hata mchezo mmoja tangu kuanza kwa ligi kuu.Kwa upande wa Azam FC katibu mkuu wa klabu hiyo Twalibu Chuma ametamba wao watakuwa wa kwanza kuisimamisha klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi.
Wakati mashabiki wengi wengi wa kandanda jicho lao likiwa katika mchezo wa Simba na Azam Fc, klabu ya African Lyon imekiri ligi kuwa ngumu na kutamba wanauhakika wa kushinda mchezo wao wa kesho dhidi ya Majimaji.

BOTSWANA KUUMANA NA ZIMBABWE

Botswana imetinga hatua ya Robo fainali ya kombe la cosafa baada ya kuinyuka Shelisheli 2-0 huko Bulawayo jana usiku.
Kwa mtaji huo Botswana watakwaana na Wenyeji Zimbabwe katika hatua ya mtoano.
Botswana ipo kileleni mwa kundi B wakiwa na pointi 7 kutokana na Michezo mitatu waliyocheza mbele ya Swaziland wenyhe pointi 6 na Comoro wenye pointi 4.
Swaziland waliianza michuano ya cosafa kwa kuinyuka Sheli sheli 3-0 lakini ushindi wa jana wa Botswana umewaweka kilelelni mwa kundi lao.
Mashujaa wa Zimbabwe waliwafunga Mauritius 3-0 katika mtanange wa ufunguzi kabla ya kwenda sanjari ya 2-2 na Lesotho.
Hatua ya robo fainali ya michuano ya cosafa itaendelea tena hapo kesho wakati Wavuvi wa Ziwa Nyasa(Malawi) watapambana uso kwa Uso na Mambas wa Msumbiji huku Namibia wakijaribu kuichimba Shaba ya Zambia.
Siku ya Jumatatu Waandaaji wa Kombe la Dunia Afrika Kusini Wataulizana na waandaaji wa Mataifa ya Afrika Angola wakati ambapo watoto wa Babu Mugabe (Zimbabwe) wataumana na vijana kutoka Jangwa la Kalahari Botswana.

MJINI MIPANGO....MGAMBO KAZINI... DUH!!!

Mgambo wa manspaa ya Ilala wakiwa wamemtia nguvuni mfanyabihashara aliyekuwa anafanya bihashara kinyume na taratibu za manspaa hiyo katika barabara ya Msimbazi Dar es salaam jana.(Picha na Rajabu Mhamila)

MALIASILI NA UTALII WAZURU CHUO CHA UTALII

WADAU WAKIPOZI KWA PICHA YA PICHA YA PAMOJAMtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Nchini Bi.Agnes Mziray wa (pili kulia) na Mkurugenzi wa utafiti na mafunzo kutoka wizara ya Maliasili na Utalii Bw.Ibrahim Mussa wa tatu (kulia) pamoja na wadau wa sekta ya utalii wakitembelea jengo linaloendelea kujengwa la chuo hicho
lililopo makutano ya mtaa wa Shaban Robert na Samora Dar es Salaam jana.(Picha na Rajabu Mhamila)Fundi akiwaelekeza wadau wa UtaliiAbderrazak Sedouga Mtaalamu wa Sekta ya utalii akitoa maelezo kwa wadau

Mafundi wakiendelea na ujenzi katika jengo la chuo cha Taifa cha Utalii lililopo makutano ya mtaa wa Samora na Shaban Robert Dar es salaam jana kushoto ni Chales Joel na Hamisi Pambe.(Picha na Rajabu Mhamila)

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA - CUF

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wanachi (CUF) Bw. Juma Duni Haji (kulia) akimnjosha mkono juu kumtambulisha kwa wananchi mgombea wa ujumbe wa Serikali ya mtaa wa Kunduchi Bw. Ally Mbawe, wakati wa kampeni zilizofanyika Tegeta Dar es salaam juzi.(Picha na Rajabu Mhamila)

Thursday, October 22, 2009

PERREIRA AKUTAMANI TENA SAUZI

Carlos Alberto Parreira amesema kuwa anaangalia uwezekano wa kupata ofa kurudi kuwa kocha wa Afrika ya Kusini.
Mkataba wa Afrika ya Kusini na kocha wa Raia wa Brazili Joel Santana umekwisha jumatatu iliyopita na Parreira anataka kupata ofa ya kurejea tena huko Bondeni.
"kuna nafasi kama kutakuwa na ofa, itakuwa makini kwangu kuangalia hiyo amesema Perreira.
"kuna viashiria kwa Wasauzi kubaki na shule ya Brazil itakayokaa katika soka la Afrika ya Kusini ameongeza Pereira.
Parreira aliiongoza Brazil kuutwaa ubingwa wa Dunia wa Mwaka 1994 alijiuzuru kama kocha wa Afriak ya Kusini mwaka uliopita mna kwenda kumhudumia mkewe aliyekuwa mgonjwa.
Ametanabaisha kuwa kazi huko Afrika Kusini itakuwa ngumu zaidi tangu nchi hiyo kutangazwa kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la 2010.
Bafana Bafana wamepoteza michezo michezo 8 kati ya 9 ya kimataifa iliyopita.

DUA YAISAIDIA ZIMBABWE KUTINGA ROBO FAINALI COSAFA

Wenyeji wa Kombe la COSAFA Zimbabwe wametinga Robo fainali ya michuano hiyo baada ya kusubiri Dua yao ikubaliwe kwa Lesotho kuifunga Mauritius 1-0 katika mchezo wa mwisho wa kundi A.
Zimbabwe iliizaba Mauritius 3-0 katika mchezo wa ufunguzi lakini walienda sanjari ya 2-2 na Lesotho.
Lesotho waliwakabili Mauritius huko Harare huku wakitakiwa kushinda 4 bila ili watinge hatua ya Robo Fainali lakini waliishia kuwazima Mauritius bao 1 kwa bila.
Mashabiki Lukuki wa Zimbabwe walijaa Dimbani kuishangilia Mauritius na walilipuka kwa furaha baada ya mtanange kwisha kwa nchi yao kufuzu hatua ya Robo fainali kwa Tofauti ya magoli.
Kundi B wanamaliza michezo yao hii leo huko Bulawayo wakati Botswana wakiikabili Sheli Sheli huku Wakomoro wataumana na Waswazi.
Comoro na Botswana wanaongoza kundi wakiwa na pointi 4 kila moja , Swaziland ni wa 3 huku Sheli Sheli wametolewa kwa kuzabwa michezo miwili.
Comoro walikwenda sululu ya 0-0 na Botswana na kuzabw a 2-1 na Sheli sheli.
Waswazi wanaofundishwa na kocha wa Zamani wa Afrika ya Kusini Ephraim "Shakes" Mashaba, walianza vyema kwa kuinyoa Sheli sheli 2-1, lakini walizimwa na Botswana 1-0.
Waliojuu kisoka kusini mwa Afrika wamenyoosha moja kwa moja katika Robo Fainali ya Michuano hiyo Jumapili Wanyasa (Malawi) watakumbana na Mamba wa Msumbiji huku Namibia watawaalika wachimba Shaba wa Zambia.
Jumatatu ijayo Bafana Bafana watawaalika Angola huku Wazimba wataumana na mshindi wa Kundi B kati ya Comoro na Botswana.

BINGO NENE MAJIMBO 8 KENYA

Washindi katika ligi ya timu za Majimbo 8 za soka watakuwa na sababu ya kufurahi baada ya ya wadhamini kuongeza Donge nono na kufikia shilingi Laki 3 za Kenya.
Waandaaji wa michuano hiyo Extreme Sports wamekutanisha timu kutoka Majimbo 8 zinazokutana jijini Nairobi wakiwa na nia ya kutambulisha na kukuza vipaji na kupandisha hali ya soka majimboni mwao.
Timu zitakazoibuka washindi katika kila eneo wa pili ataondoka na Elfu 60 shilingi ya Kenya na watatu ataondoka na Elfu 15 shilingi ya Kenya .
Waandaaji hao wamepokea cheki ya Ufadhili kutoka Moto Gari, Cellz Are Us na Lock 7 kampuni za mawasiliano shilingi za Kenya Laki 7 huku extreme sports ambao ni waandaaji wamesema kuwa wataeneza michuano hiyo katika sehemu nyingine za Nchi ya Kenya.
Michuano hiyo inayoibua vipaji mbali mbali imeanza kwa ju8mla ya timu 78 inatarajiwa kufikia fainali February mwakani.

MISS TANZANIA APOKEWA KAMA MALIKIA MWANZA


Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald,akiwapungia mkono wananchi wa jiji la Mwanza walipompokea leo jijini humo, aliyesimama kushoto ni mmoja wa waandaji wa Vodacom Miss Mwanza Anita Zimbire. Miriam anatarajiwa kufanyiwa sherehe kubwa kesho jioni jijini Mwanza katika kumkaribisha rasmi ambapo mgeni wa heshima atakuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro.Jinsi maandamano ya mapokezi ya Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald yalivyofana jiji Mwanza

Wednesday, October 21, 2009

MATOKEO YA LIGI KUU TANZANIA BARA OCTOBA 21, 2009

MTIBWA SUGER 2 - 1 TOTO AFRICAN
Wafungaji
OMARI MATUTA MAULIDI HANIU
SAIDI MKOPI

TANZANIA PRISON 1 - 0 KAGERA SUGER
Mfungaji
BENJAMIN ASUKILE dk 74

TANZANIA "TAIFA STARS" KUCHEZA NA MISRI

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo wake wa Kimataifa wa kirafiki na Mafarao wa Misri mchezo utakaochezwa nchini humo Novemba 5 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Tff Afisa habari nwa Shirikisho hilo Florian Kaijage, amesema baada ya kupata mwaliko huo kikosi cha Taifa Stars kitatangazwa Jumanne Ijayo kujiandaa na mpambano huo, ukuzingatia timu hiyo ni Mabingwa wa Afrika mara mbili.
Kaijage ameongeza kuwa kuwepo kwa mechi ya Kimataifa ya Kirafiki baadhi ya michezo ya Ligi kuu itasogezwa mbele kutokana na wachezaji kuchelewa kurudi katika timu zao.

YANGA - MAJIMAJI ISHUSHWE DARAJA KAMA JUVENTUS

Uongozi wa klabu ya Yanga unataraji kuwasilisha barua katika Shirikisho la Kandanda TFF, Kupinga maamuzi yaliyotolewa na kamati ya mashindano kuwafungia waamuzi wanne maisha na kuitaka klabu ya maji maji ya Songea kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi (10) kama faini kabla ya kuanza msimu wa pili wa Ligi kuu kutokana na tuhuma za rushwa zinazowakabili.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Imani Mahugira Madega amesema yawezekana hawakuangalia vizuri adhabu waliyoitoa kutokana na kosa lenyewe katika rushwa, kwani mtoaji na mpokeaji wanatakiwa wawe na adhabu sawa.
Ameongeza kuwa Viongozi wa Maji maji ya Songea nao wafungiwe maisha kama waamuzi na Majimaji ishushwe daraja kwa kuwa Sheria iko wazi hata kimataifa ndio maana Juventus ilishushwa daraja baada ya kubainika imefanya udanganyifu.
HATUA HIYO IMEKUJA KUFUATIA TAARIFA HII ILIYOTOLEWA JANA NA TFF
Kamati ya mashindano ya Shirikisho la soka Nchini Tff limewafungia Waamuzi wanne maisha, pia na kuitaka klabu ya Maji maji ya Songea kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi 10 kama faini kabla ya kuanza msimu wa pili wa Ligi kuu kutokana na tuhuma za rushwa zinazowakabili.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Tff Afisa habari wa Shirikisho hilo Frolian Kaijage amesema kamati hiyo ilikaa jana na kujadili masuala mbalimbali ya Ligi kuu ya Tanzania bara hususani katika mchezo namba 20 kati ya Maji maji na Mtibwa Sukari uliochezwa Septemba 9 mwaka huu.
Kaijage ameongeza kuwa katika kamati hiyo walibainisha mambo makuu manne kabla ya kutoa maamuzi hayo.
Miongoni mwa waamuzi waliyofungiwa maisha ni pamoja na Athumani Kazi.

SIMBA YA WATAKA YANGA WASITAFUTE MCHAWI

Klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam imewataka wapinzani wao wa jadi Yanga kutowatupia lawama pale wanapopata tatizo na waangalie vizuri walipojikwaa na si walipoangukia.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Simba Cliford Ndimbo baada ya kupata taarifa kutoka Yanga kuhusu kufungiwa kwa mchezaji Moses Odhiambo na Amiri Maftah kumesababishwa na Simba.
Ndimbo amesema Ligi Kuu ya Mwaka huu imeendeshwa vizuri na makosa ambayo yanafanyika katika michezo mbali mbali inafanyiwa kazi na kutolewa maamuzi, hivyo amepongeza Shirikisho la kandanda Tanzania kwa kazi nzuri waliyoifanya katika Ligi inayoendelea.
Somba hadi sasa imejikusanyia jumla ya pointi 24 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.

JAMANI HUKU KUSHANGILIA GANI...???

Hii ilikuwa siku ambayo Argentina ilifanikiwa kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani Afrika Kusini, sasa hawa ni mashabiki wakishangilia, mimi nilistaajabu nikasema si vibaya nikawauliza wadau, jamani huku ni kushangilia gani?

MASANJA AAGWA , JUMATANO KUPELEKWA URAMBO, TABORA

MAMIA ya wadau wa michezo nchini, wamejitokeza kuuaga mwili wa marehemu, Meneja wa Uwanja wa Taifa na Uhuru, Charles Massanja (52) aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumatatu nyumbani kwake Kimara, Dar es Salaam baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yake.
Katika kuuaga mwili wa marehemu Massanja, siku ya Jumanne, viongozi mbalimbali wa serikali, Vyama vya Michezo, viongozi wa Klabu mbalimbali na wadau wengine walihudhiria, ambapo mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda nyumbani kwao Urambo, Tabora kwa maziko.
Akiongoza mamia ya waombolezaji katika maombolezo yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera alizungumza kwa niaba ya serikali na kusema Massanja alikuwa ni kiongozi mwenye nidhamu asiyependa makuu.
Amesema kifo chake cha gafla kimewashtua wadau wengi wa michezo na pengo aliloacha halitaweza kuzibika kwani alikuwa ni miongoni mwa wataalam wachache katika michezo hapa nchini.(NAIBU WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO JOEL BENDERA AKIWEKA SHADA LA MAUA KATIKA JENEZA LA MASANJA)Amesema ninautambua uwezo wa Massanja tangu zamani ila Mwenyezi Mungu amempenda zaidi ndio maana amemchukua, hivyo hatuna budi kumuombea kwa mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, amina.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Leonard Thadeo amemzungumzia Massanja kwa kusema, alikuwa anajali kazi yake kwa kuipenda ambapo alikuwa akiitumikia bila kusukumwa na mtu ndicho kitu kilichosababisha kupendwa na wadau wa michezo.
Mbunge wa Ilala, Idd Azan naye alikuwepo katika kuuaga mwili wa Massanja ambapo amesema mpaka sasa hawajui ni nani atakayeweza kuziba pengo lililoachwa na Massanja kwani alikuwa mtu wa watu, itachukua muda kusahau mazuri yake.
Amesema wadau wa michezo hawana budi kumuombea kwa mungu aepukane na adhabu ya kaburi, kwa jinsi alivyokuwa akijitolea kwa wanamichezo mbalimbali hawana budi kumshukuru.
Pia Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, Idd Kipingu amemzungumzia Massanja kwa kusema, marehemu alikuwa akifanya kazi katika eneo nyeti na aliweza kulimudu bila matatizo yoyote kwa kuweza kushirikiana na watu vizuri bila malalamiko ya hapa na pale.
Amewaomba viongozi wa Vyama vya michezo wamuenzi Massanja kwa kuiga yale mazuri ambayo alikuwa akiyafanya likiwemo la nidhamu ambapo ndicho kitu kilichomfanya akubalike miongoni mwa wadau wa michezo.
Naye Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodgar Tenga amesema, wao ndio wadau wakubwa wa soka hapa nchini wamesikitishwa na kifo hicho cha gafla kwani alijitolea maisha yake katika soka na huwezi kuzungumzia maendeleo ya soka bila kulitaja jina lake.(Bi. Devotha, mke wa marehemu akiaga mwili wa mumewe kwenye uwanja huo)Nao Wenyeviti wa Klabu kongwe nchini za Simba na Yanga kwa nyakati tofauti walimzungumzia Massanja ambapo Hassan Dalali wa Simba amesema siku ya mchezo wa timu yao dhidi ya JKT Ruvu alitaniana na marehemu kwa kubishana kwamba marehemu alitaka Dalali akakae kwenye jukwaa kuu na Dalali alikataa kwa kusema huko wanakaa viongozi wa serikali tu.
Naye Iman Madega wa Yanga, amesema wamempoteza mwanachama wao hai kwani alikuwa akiwasaidia mambo mengi uwanjani na pia alifundisha soka timu mbalimbali hapa nchini.
Massanja alizaliwa miaka 52 iliyopita huko Urambo, Mkoani Tabora na kupata elimu ya sekondari katika shule za Itaga mjini Tabora na Minaki jijini Dar es Salaam kuanzia mwaka 1972 mpaka 1977 na baadaye kuendelea na elimu ya juu kwa kupata Shahada ya Uzamili wa Physical Education nchini Cuba mwaka 1988.
Enzi za uhai wake Massanja aliwahi kufanya kazi na miaka yake katika mabano za Ofisa Michezo Daraja la Kwanza(2007), Meneja wa Uwanja wa Taifa na Uhuru (2006 mpaka umauti unamkuta), Katibu Mkuu Msaidiu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania enzi hizo kikijulikana FAT (1995-96, 2002-04), Ofisa Michezo Idara ya Mendeleo na Michezo(1996-2001) na Kocha Mkuu wa timu ya African Sports ya Tanga (1990-1994).

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina

MAVAZI ASILIA KWA MTINDO WA KISASA YANAPENDEZA...?

VAZI LA KIAFRIKA LINAPOKARABATIWA KISASA HUPENDEZA SANA

ZAIN YAZINDUA PAMOJA+ (UHURU WA KUONGEA)

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Zain Tanzania Bw. Kelvin Twissa,(kushoto) Mkurugenzi Mkuu, Khalid Muktad na Ofisa Bihashara wa kampuni hiyo Bw. Chiruyi Walingo wakiwa wameshika vipeperushi wakati wa uzinduzi wa Pamoja+ iliyozinduliwa Dar es salaam jana ambapo mteja anauwezo wa kuchagua watu kum wa mtandao uho na mmoja kutoka mtandao wowote nchini kwa kuongea kwa garama nafuu.(Picha na Rajabu Mhamila)

KAMATI ZA BUNGE ZAENDELEA...

Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali Bw. Jonh Cheyo (kushotO) akizungumza na mwenyekiti wa mda wa Kamati hiyo Dar es salaam.Bw.Mudhiri wakati wa vikao vya kamati za bunge.(Picha na Rajabu Mhamila)Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini Bw. Victor Mwambalaswa (kulia) akizungumza na wahandishi wa habari kuhusu kutembelea mitambo ya SONGAS Dar es salaam jana kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw.William Shelukindo.(Picha na Rajabu Mhamila)

Monday, October 19, 2009

RAMBIRAMBI ZA MSIBA WA CHARLES CELESTIN MASANJA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

1. RAMBIRAMBI ZA MSIBA WA CHARLES CELESTIN MASANJA

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania limepokea kwa mshtuko mkubwa msiba wa Meneja wa Uwanja wa Uhuru, Charles Celestin Masanja uliotokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Oktoba 19, 2009 nyumbani kwake Kimara Dar es Salaam.

Kwa TFF jamii ya mpira imempoteza mtu muhimu ambaye alikuwa na ushirikiano mkubwa katika harakati za kusukuma mbele maendeleo ya soka la Tanzania hasa ikizingatiwa kuwa kifo hiki kimekuja ghafla na katika wakati ambao mchango wake ulikuwa bado unahitajika mno.

Kutokana na ushirikiano wake na watu mablimbali aliofanya nao kazi, Masanja amekuwa ni rafiki wa watu wengi na kwa hakika alikuwa mtu wa watu.

TFF inamtambua Masanja kama mtu aliyekuwa muhimu hasa kutokana na kutumikia vema nyadhifa mbalimbali alizowahi kuzipata katika mpira kama ifuatavyo:

1990 Kocha Mkuu wa klabu ya African Sports ya Tanga.
1993 - 1996 - Katibu Msaidizi wa FAT akiwa ameazimwa kutoka Wizarani
2002 – 2004 - Katibu Mkuu msaidizi wa FAT (wa kucaguliwa)
2005 – 2009 Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya TFF
2007 – 2009 Mkufunzi wa ukocha – Mkoa wa kimashindano wa Temeke
2004 – 2009 Mjumbe wa mkutano Mkuu wa TFF kupitia Chama cha Makocha
(TAFCA)

Mbali na nyadhifa hizo, Charles Masanja alikuwa mmoja wa makocha wa kiwango cha Juu hapa nchini kulingana na vigezo vya TAFCA.

TFF itashiriki kikamilifu katika msiba huu na inawatakia wanafamilia uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Mungu aiweke roho ya Marehemu Charles Celestin Masanja mahali pema peponi, Amen.


Florian Kaijage
AFISA HABARI

POOLTABLE KWENDA AFRIKA KUSINI KUSHIKRIKI MASHINDANI YA KIMATAIFA

Wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo wa pool wakiwa wameshika bendera ta Tanzania baada ya kukabidhiwa Dar es salaam leo(Picha na Rajabu Mhamila Super D Mnyamwezi)
Mchezaji wa Timu ya taifa ya pool table na nahodha wa timu hiyo Aliakber Akberal akijaandaa kupiga mpira wakati waiagwa kwenda kwenye mashindano Afrika ya kusini yanayoanza kesho.(Picha na Rajabu Mhamila Super D Mnyamwezi)Mwanamziki wa bendi ya msondo ngoma Rashidi Mwezingo akijataarisha kupiga mpira wakati aliposhiriki mchezo wa pool table.(Picha na Rajabu Mhamila Super D Mnyamwezi)