Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, February 16, 2011

Iker Casillas bado alia na mwamuzi




MADRID,Hispania

MLINDA mlango wa timu ya Real Madrid, Iker Casillas amesema wazi kwamba hakustahili kutolewa nje ya mchezo kati ya timu yake dhidi ya Espanyol wa michuano ya Ligi Kuu ya Hispania uliofanyika Jumapili iliyopita jioni.

Mlinda mlango huyo wa timu ya Taifa alitolewa nje ya mchezo huo baada ya kuoneshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mchezaji Jose Callejon nje eneo la penalti zikiwa ni dakika mbili tangu mchezo huo uanze na picha za video zinaonesha kuwa hakukuwepo na kosa kubwa la kustahili adhabu hiyo.

Casillas anaamini kwamba hakustahili kupewa kadi hiyo na anapingana vikali na uamauzi wa mwamuzi wa pambano hilo.


"Kadi yangu nyekundu inatia shaka lakini kama mwamuzi aliona ni sahihi basi tunapaswa kuikubali,"alisema mlinda mlango huyo kupitia tovuti ya klabu.

“Jambo la muhimu ni kwamba timu ilicheza soka safi na ilistahili kuwa kati ya wachezaji 10 kwa 10.Kiwango chetu kilikuwa juu na sisi tukafanikiwa kuondoka napointi tatu muhimu kwetu,”aliongeza.

Mbali na kulalamikia kadi hiyo,mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 29 alimpongeza mchezaji aliyingia kuchukua nafasi yake Antonio Adan akisema kuwa Adan alicheza mechi ngumu na atakuwa na mafanikio siku za mbeleni.

No comments :

Post a Comment