Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, September 3, 2011

DENZEL MUSUMBA AKAMILISHA SALAMU ZA EID MUBARAK KUPITIA EAST AFRICA RADIO USA



Mtangazaji wa East African Redio US Anko Denzel Musumba, aliembeba dogo Hudhaifa Shatry akiwa na mzee wa swahilivilla editor, juu ya mpangilio mzima wa kuandaa kipindi cha salamu na pongezi, kilichoandaliwa rasmi na Abou Shatry, Mtangazaji wetu wa East African Redio US, Anko Danzel Musumba, pamoja na mzee wa changa moto yetu, Mubelwa Bandio, ndani ya East African Redio US.

Juzi ilikuwa ni Sikukuu kubwa ya waislamu Duniani kote siku ya Eid El Fitr, kwa furaha ya kuadhimisha siku hii adhimu ya kupongezana, kutoleana salamu na kutakiana kila la kheri katika mfungo mzima wa mwenzi mtukufu wa Ramadhani, uliomalizika siku ya jumatatu kumkia jumanne ya Aug,30/2011,

Baadhi ya waumini wa Jumuiya ya Kiislamu Tanzanian Muslim Community Washington Metropoli (TAMCO). wanaoishi hapa DVM hawana budi, kumpongeza ndugu yetu, mtangazaji wetu wa East African Redio US, Bwana Denzel Musumba kwa kazi nzuri aliyo ifanya jana katika kipindi cha salamu za kupongezana na kutakiana edi jeema, kupitia East Africa radio LIVE siku ya jumanne Aug 30, 2011 mida ya saa 6: PM hadi 10:PM

Mtangaziji wa Redio hiyo Bwana Denzel Musumba, aliweza kuunganisha waumini wa dini ya kislamu na wasiokuwa waislamu kutoa pongezi zao mbali mbali na kuwatakia sikuku ya jeema ya Eid El Fitr kupitia kwa njia ya mtandao na simu ya East Africa radio USA, ambayo pia unaweza kusikiliza kwa simu ya mkononi redio hiyo kwa njia ya simu, nambari (347)857-1206 juu ya maada yoyote inayoongelewa LIVE ikitaka kuchangia maoni yako na kuongea na mtangazaji wetu ndugu, Denzel Musumba unabofya numbari (1),yeye atakutajia number zako za mwisho ili kukujulisha ndio wewe atakaeongea nawee na kukupa uwanjaa wakutoa maoni yako. kwa mada iliokuwa hewani.

Siku zote sitochoka kusema hivi, Jamii iliyostaarabika ni yenye kuheshimu Mawazo na mitazamo ya wengine. Mchango wako katika kazi yoyote ile, hujenga jamii yenye kujitambua, Kujithamini na Kujiwajibisha. Pale panapo mahitaji kuhusu jamii yetu kwa jumla. Hii ni kuonyesha amani, maelewana, upendo, na ustahi wajamii yetu hii tuipendayo katika kipindi hiki kigumu kilichotukabili. Chuki ni sumu ya mapenzi.

No comments :

Post a Comment