Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, September 3, 2011

JITOKEZE NA UONYESHE UWEZO WAKO JIJINI DAR ES SALAAM WAKATI GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ IKISAMBAA KIMATAIFA


Wapenzi wa kinywaji mahiri cha Guinness na mashabiki wakubwa wa mpira wa miguu nchini Tanzania, kwa mara ya kwanza GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ itazinduliwa SEPTEMBA 4 katika viwanja vya Leaders Club. Usikose kujionea maajabu ya mpira wa miguu katika kipindi hiki kabambe cha Televisheni ambacho kinaangaliwa na kuwavutia watu wengi barani Afrika, ambapo kitawapatia mashabiki nchini Tanzania nafasi ya kujitokeza na kuonyesha mapenzi yao ya dhati katika mpira wa miguu na kushindana na mashabiki wakubwa wa mpira wa miguu kutoka Kenya na Uganda na kujishindia mamilioni ya fedha.

Timu ya majaji itakuwepo kwenye viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kufanya usaili kutafuta mashabiki wenye mapenzi na vipaji kwa mpira wa miguu watakaoiwakilisha Tanzania katika kipindi cha Televisheni cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE

Kipindi cha Televisheni cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ ni cha kimataifa, Timu ya Majaji imeshafanya usaili katika miji mikubwa ya Kampala, Nairobi na itakuwa Dar es Salaama tarehe 4 Septemba 2011 kwa ajili ya kutafuta mashabiki wenye mapenzi na vipaji kwa mpira wa miguu kutoka nchi za Uganda, Kenya na Tanzania ambao watashindana ili kupata nafasi ya kujishindia zawadi nono.

Mashabiki watakaotaka kushiriki wanatakiwa waje na rafiki na wawe tayari kuonyesha uwezo wao. Washiriki ni lazima wawe wawili wawili, mmoja kati yao inabidi awe tayari kuonyesha kipaji na ujuzi wake wa mpira wa miguu na mwingine kuoyesha ufahamu wake wa mpira wa miguu. Majaji wataangalia uwezo wako wa kuchezea mpira kupitia mifumo ya mazoezi ya mpira wa miguu kuona ili kuona kama una uwezo na kipaji cha kuingia katika kipindi cha televisheni cha Gunness Football Challenge.

Itakuwa ni siku nzuri kwa kila mtu, kutakuwa na shughuli nyingi za mpira wa miguu, muziki na burudani, Usikose nafasi hii ya kuwa mshiriki na kushuhudia maajabu ya mpira wa miguu ambayo yatainyanyua nchi yetu. Njoo leaders tarehe nne mwezi wa tisa viwanja vya Leaders Club kuanzia saa nne asubuhi. Watakaoruhusiwa kuingia ni wale wenye miaka zaidi ya kumi na nane. Hakuna Kiingilio.

Kipindi cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ kinakuja Tanzania, jitokeze na uonyeshe uwezo wako ili upate nafasi ya kushinda hadi dola za kimarekani Elfu Hamsini kila wiki kwa wiki nane kwenye kipindi cha television. Huu ni wakati muafaka wa kuonyesha jirani zetu Kenya na Uganda kuwa mashabiki wakubwa na mahiri wa mpira wa miguu wanatokea Tanzania.

Tafadhali kumbuka, usinywe pombe kupita kiasi. Guiness haiuzwi kwa walio chini ya miaka 18

No comments :

Post a Comment