Kenny Dalglish amtetea Andy Carroll
Meneja wa klabu ya soka ya
Liverpool, Kenny Dalglish, amemtetea mchezaji Andy Carroll, kufuatia
madai ya kocha wa timu ya taifa ya England, Fabio Capello, kuhusu
starehe za kibinafsi za mchezaji huyo.
Carroll alikuwa ni mchezaji wa zamu katika mechi ambayo England ilipata ushindi ilipocheza dhidi ya Wales.
Capello awali alikuwa amesema: "Ikiwa anataka kuwa mchezaji mzuri, basi ni lazima apunguze kinywaji zaidi wa wenzake".
Lakini Dalglish amesisitiza: "Hali yake ya afya ni bora zaidi kumshinda yeyote yule.
"Sidhani maisha na starehe zake za kibinafsi sio kama inavyofikiriwa katika kutafuta cha kuandika kumhusu".
Meneja wa Liverpool aliongezea: "Andy hakuwa katika hali nzuri msimu uliopita kutokana na jeraha la goti.
"Tunafurahia hali yake ya afya msimu huu kwa kwa jeraha hilo limetoweka".
Carroll, mwenye umri wa miaka 22, amecheza tangu
mwanzo katika mechi mbili, kati ya mechi nne za Liverpool, tangu
alipofika katika uwanja wa Anfield, kufuatia kuhama kutoka Newcastle
mwezi Januari.
Mchezaji huyo alifunga mara moja katika pambano
la Kombe la Carling dhidi ya Exeter, lakini msimu uliopita, aliweza
kutumbukiza magoli mawili katika lango la Manchester City, wakati timu
yake ilipopata ushindi wa magoli 3-0.
Dalglish aliongeza: "Nadhani Andy anapokea mawaidha vyema hasa kutoka kwa yeyote yule mwenye uzoefu katika mchezo wa soka".
"Nadhani amepokea vyema mawaidha ya Capello kwa
kuwa anamheshimu sana, na nadhani, Fabio Capello naye amheshimu sana
Andy Carroll".
No comments :
Post a Comment