TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 8, 2011
VPL KUCHEZWA UWANJA WA TAIFA
Serikali
imeruhusu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutumika kwa mechi za Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) zinazohusu timu za Simba na Yanga. Hata hivyo ruhusa
hiyo ni ya mechi mbili kwa wiki.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za VPL zenye maskani yake Dar
es Salaam waliwasilisha tena maombi Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo ili kutumia uwanja huo kwa mechi za ligi.
Kutokana
na uamuzi huo wa Serikali mechi ambazo sasa zitachezwa kwenye uwanja
huo ni Ruvu Shooting vs Yanga (Septemba 10), Azam vs Simba (Septemba
11), Simba vs Polisi Dodoma (Septemba 14), African Lyon v Yanga
(Septemba 15), Azam vs Yanga (Septemba 18), Yanga vs Villa Squad
(Septemba 21).
Nyingine
ni Yanga vs Coastal Union (Septemba 24), Simba vs Mtibwa Sugar
(Septemba 25), Yanga vs Kagera Sugar (Oktoba 14), Simba vs African Lyon
(Oktoba 16), Simba vs Ruvu Shooting (Oktoba 19), Yanga vs Toto Africans
(Oktoba 20), Simba vs JKT Ruvu (Oktoba 22), Yanga vs Oljoro (Oktoba 23),
Yanga vs Simba (Oktoba 29) na Moro United vs Simba (Novemba 5).
TWIGA STARS, BANYANA BANYANA 2-2
Timu
ya Taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) imetoka sare ya mabao
2-2 na Afrika Kusini (Banyana Banyana) katika mechi ya michezo ya All
Africa Games (AAG) iliyochezwa leo Uwanja wa Machava jijini Maputo,
Msumbiji.
Banyana
Banyana ndiyo iliyoanza kupata bao kabla ya Twiga Stars kusawazisha
dakika ya 25 kupitia kwa Mwanahamisi Shuruwa. Banyana Banyana ilianza
kipindi cha pili kwa nguvu na kupata bao la pili. Zena Khamis
aliisawazishia Twiga Stars dakika 60.
Twiga
Stars itacheza mechi yake ya mwisho hatua ya makundi Septemba 11 mwaka
huu dhidi ya Zimbabwe kwenye uwanja huo huo. Katika mechi yake ya kwanza
Zimbabwe ilifungwa na Banyana Banyana mabao 4-1.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments :
Post a Comment