Arsene Wenger amesema wala hasumbuliwi na kelele zinazopigwa dhidi yake na anataka kuendelea kuingoza Arsenal kwa kipindi kirefu zaidi.
Wachambuzi wa soka wamekuwa wakihoji nafasi ya Wenger wakati huu Arsenal ikishikilia nafasi ya 17 ya msimamo wa Ligi Kuu ya England wakiwa wameuza wachezaji muhimu msimu huu.
Lakini baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Shrewsbury kuwania Kombe la Carling, Wenger amesema: "Sijali kabisa kutokana na uvumi uliopo dhid yangu kwamba nitatimuliwa.
"Nimekuwa katika klabu hii kwa miaka 14 na nimefanikiwa kuiweka katika kuwania ubingwa wa Ulaya kwa miaka hiyo 14. Natumai nitaendelea kuwepo miaka mingine 14."
Mtendaji mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis ameiambia BBC kwamba kumfukuza Wenger sio jambo wamalofikiria kulitekeleza.
Zaidi anachokiangazia zaidi Wenger ni kuimarisha kikosi chake baada ya nahodha wake Cesc Fabregas kuhamia Barcelona na kiungo mwenzake Samir Nasri kujiunga na Manchester City mwezi wa Aprili.
Katika siku ya mwisho ya usajili, kiungo wa Everton Mikel Arteta, mshambuliaji Park Chu Young, beki wa kushoto Andre Santos na mlinzi wa kati Per Mertesacker walijiunga na Arsenal, wakati Wenger pia alimchukua kwa mkopo Yossi Benayoun kutoka klabu ya Chelsea.
Lakini mabadiliko hayo yamekuwa makubwa kuyazoea uwanjani, wakati Arsenal imeshinda mechi moja tu ya Ligi kati ya mechi tano huku ikiwa imefungwa mabao mengi hadi sasa.
Wenger amesema:"Naelewa watu hawana furaha na wanalaumu, lakini najua mnafahamu kama ninavyofahamu kwamba watu wanakuwa wepesi sana kufikia hatua ya kulaumu".
"Tunapofanya vizuri tunashangiliwa na kupongezwa, kwa hiyo tunawajibika kukubali lawama iwapo mambo yanapokwenda kombo - lakini kwa pande zote mbili pia tunatakiwa kuwa na subira.
No comments :
Post a Comment