Mbunifu wa mavazi wa kimataifa nchini Afrika Kusini, David Tlale akiwa na Mwanamitindo wa Kimataifa kutoka Tanzania, Millen Magesa wakipita jukwaani stejini mara baada ya kuonesha ya kuonesha mavazi yake katika Tamasha la Mercedez Benz African Fashion Week, lililofanyika kwenye Stehsni ya Treni ya Ravos ya Mjini Tshwane, Pretoria, Afrika Kusini hivi karibuni
Thursday, October 31, 2013
MWANAMITINDO WA KIMATAIFA MTANZANIA MAGESSE AZIDI KUTESA

PHD AOMBA RADHI MASHABIKI

Na Elizabeth John
MSANII wa filamu na bongo fleva nchini, Hemed
Suleiman ‘PHD’ amewaomba radhi mashabiki wa muziki wake kwa kutoonekana msanii,
Heri Samir ‘Mr Blue’ katika video ya wimbo wake wa ‘Rest Of My Life’.
Katika video ya wimbo huo, sauti ya Mr Blue
unasika lakini yeye haonekani kitu ambacho kimewashangaza mashabiki wa msanii
huyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Hemed
alisema hiyo imetokana na msanii huyo kutokuwepo nchini wakati akifanya
‘shooting’ ya wimbo huo.
“Naomba sana radhi kwa mashabiki wangu kwa
kutoonekana Mr Blue katika video ya wimbo huo, wakati nafanya video ya wimbo
huo, hakuwepo nchini baada ya kuona audio imekaa kwa muda bila video
nikalazimika kuifanya pekeyangu,” alisema.
Msanii huyo alishawahi kutamba na kazi zake kama, ‘Mama Kimbo’, ‘Usiniache’, ‘Ninachotaka’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.
Wednesday, October 30, 2013
WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KONYAGI (TDL) WALIOKWENDA KUONA MECHI YA BARCELONA NA REAL MADRID,HISPANIA WAREJEA WAKIWA NA BASHASHA TELE
Mfanyakazi wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited
(TDL), Khadija Madawili ambaye alikuwa kiongozi wa msafara wa
wafanyakazi wa TDL waliokwenda kushuhudia pambano la Ligi ya La Liga ya
Hispania kati ya Barcelona na Rael Madrid, akirejea jana kwenye Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Wafanyakazi
watano wa TDL, waliteuliwa baada ya kampuni hiyo kushinda Tuzo ya
SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13)
Joseph Chibehe (kushoto) akilakiwa na mkewe baada ya kuwasili
Chibehe akiwa na furaha baada ya kulakiwa na mkewe
Bavon Ndumbati (kushoto), akilakiwa na ndugu yake. Katikati ni Michael Mrema
Bavon akiwa na furaha
Mwesiga Mchuruza.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (katikati), akiwa na mabosi wa kampuni mama ya SABMILLER AFRICA.wakiwa wameshikilia tuzo hiyo ya MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR (F 13).
KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd, (KONYAGI) ambayo ni miongoni mwa kampuni tanzu za Kampuni ya Sabmiller South Africa, imeshinda tuzo ya utendaji bora wa bidhaa (SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13). Sabmiller inamiliki zaidi ya viwanda 60 vya bia na vinywaji vingine duniani.
Baada ya ushindi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TDL, Mgwassa ambaye alipambana mpaka kupata ushindi huo, aliamua kuwazawadia baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, kwenda Hispania kushuhudia pambano la timu kubwa za Barcelona na Real Madrid lililofanyika mwishoni mwa wiki.
Wafanyakazi waliokwenda Hispania na kurejea jana usiku kwa ndege ya Afrika Kusini ni; Joseph Chibehe, Khadija Madawili, Bavon Ndumbati, Michael Mrema na Mwesiga Mchuruza.
Wafanyakazi hao, walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, walionekana kuwa na bashaha na kupokelewa na ndugu zao pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzao.
Akizungumza kwa niaba ya wenzie,Michael Mrema wa Kanda ya Kaskazini, alisema kuwa wanashukuru uongozi kuwapa zawadi hiyo, ambayo imewafanya kuwa na morari mpya wa kazi.
Pia anaseama walifurahi sana kushuhudia mechi hiyo kubwa ya timu za Barcelona na Real Madrid ambapo timu ya Barcelona waliyokuwa wanaishabikia kushinda mabao 2-1.

AIRTEL MONEY HAKATWI MTU INAWAPIGA TAFU WAFANYA BIADHARA YA SAMAKI MWALONI MUSOMA NA MWANZA.
kushoto ni Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando na kulia ni Ofisa
Masoko wa kanda ya ziwa Bw Ally Mashauri wakimkabidhi vitendea kazi
vya uwakala Bw, Innocent Godwin (kati) anaefanya uwakala ndani ya soko
la samaki la kimataifa Mwaloni Kirumba Mwanza leo wakati ambapo airtel
walitembelea sokoni hapo kujionea jinsi wauzaji na wanunuzi wa samaki
wanavyoitumia huduma yao ya kutuma na kutoa pesa bila makato
wanapokuwa kwenye biashara zao-hakatwi mtu hapa

Wakwanza mbele kushoto ni Meneja uhusiano wa Airtel jacksonm Mmbando
na ofisa masoko wa Airtel Mwanza Bw Ally Mashauri wakimsikiliza bw,
Rashid Moshi mmoja wa wauzaji na mvuvi wa samaki katika soko la
kimataifa la Samaki Mwaloni Kirumba Mwanza leo wakati ambapo Airtel
walitembelea sokoni hapo na kuzungumza na wateja wao jinsi huduma ya
Airtel Hakatwi mtu inavyowafaidisha kufanya biashara zao za kuuza na
kununua samaki kupitia airtel money bila makato- Hakatwi mtu hapa.

Biashara ya samaki kwenye Mwalo wa Musoma mkoani Mara na Kirumba
mkoani Mwanza imepata msukumo wa kipekee baada ya kuanzishwa kwa
kampeni ya hakatwi mtu, ambayo inawawezesha watumiaji wa mtandao wa
airtel kutuma na kupokea pesa bila makato.
Ikiwa inaingia katika mwezi wa tatu sasa kampeni ya hakatwi mtu
inayowawezesha wateja wa airtel money kufanya miamala yao bila makato,
wafanyabiashara na wachuuzi kwenye soko la samaki la Mara Mmusoma
wanatumia kampeni hiyo kama njia ya kupunguza kutembea na pesa muda
wote kwa ajili ya kununua ama kuuza samaki na dagaa
mwenyekiti wa soko la samaki na dagaa mwaloni Musoma Mara bw, Gideon
Dogori anasema airtel money hakatwi mtu ni sawa na kufanya biashara ya
malipo kamili yaani cash kutokana na falsafa yake ya hakatwi mtu.
Anasema wafanyabiashara sokoni hapo hufanya malipo kwa kutumia airtel
money na hawana tena ulazima wa kutembea na maburungutu ya fedha kwa
ajili ya kununulia dagaa ama samaki.
"Tangia hawa jamaa wa airtel waanzishe hii huduma yao ya hakatwi mtu
wafanyabiashara hapa wamekua hawatembei na lundo la hela kama
ilivyokua mwanzoni bali sasa wanauza na kununua bidhaa kwa kutumia
simu zao za mkononi",alisema Bw. Dogori.
"Kuna wengine wanaishi nje ya Musoma kwahiyo wanatuma tu pesa na
wanatumiwa bidhaa zao huko walipo bila kufika hapa sokoni kwasababu
huduma ya airtel money haina makato yoyote" aliendelea kueleza
mwenyekiti wa mwalo wa samaki na dagaa musoma bw. Dogoli.
Bw Dogori anasema faida kubwa inaonekana kwenye huduma hii hasa kuokoa
muda kwa wafanyabiashara, ambapo hawahitajiki kusafiri mwendo mrefu
kwenda sokoni hapo kufanya manunuzi kama ilivyokuwa zamani bali
wanatuma tu hela na kusubiria bidhaa zao huko walipo.
"Huduma hii ingekuwa ya kudumu ingesaidia sana wafanyabiashara kwani
ka muda huu mfupi imeweza kusaidia kuongeza hata miataji kwa
wafanaybiashara hapa mwaloni", alisisitiz Dogori.
Bi Mkami Magesa ni mfanyabiashara kwa zaidi ya miaka kumi sokoni hapo,
anasema wakati huu biashara imerahisishwa sana kwani kupitia huduma ya
hakatwi mtu amekuwa akifanyabiashara kubwa na anapata pesa yake bila
makato.
"Hii huduma ya airtel money ya hakatwi mtu ni mkombozi kwakweli kwani
mteja anaweza akawa shinyanga ama singida anatuma humu pesa na mimi
nampakilia mzigo wake anaupata bila ya yeye kufika hapa mwalini",
alisema bi Mkami.
Kwa upande wake John Anton mchuuzi wa dagaa na samaki katika soko la
samaki Mwaloni Mwanza Anasema anachofanya ni kutoa oda ya bidhaa
anazohitaji na kisha kutuma pesa bila makato kwenda kwa muuzaji na
kuokoa muda wa kusafiri kutoka sirali anapoishi na kufanyia biashara
zake.
"Kwasasa maisha na biashara imekuwa rahisi sana nawaomba airtel
kuifanay huduma hii kuwa endelevu maana inasaidia sana katika shughuli
za kibiashara", alisema Bw. Bundala.
Bw Dogori ambaye ni mwenyekiti wa mwaloni mjini Musoma alimalizia kwa
kusema elimu zaidi ya matumizi ya huduma za airtel money inahitajika
kwani zimeanza kuonesha dalili za kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara wa
soko lake.
TASWA WAPONGEZA UONGOZI MPYA WA TFF
CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kinatoa pongezi kwa uongozi
mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliochaguliwa Jumapili iliyopita.
Tunaungana
na wapenda michezo na Watanzania kwa ujumla kuitakia kila la heri Kamati ya
Utendaji ya TFF na shirikisho hilo kwa ujumla chini ya Rais mpya Jamal Malinzi
na Makamu wake, Wallace Karia.
TASWA
inaamini Malinzi, Karia na wajumbe wao ni wazoefu na ni watu wenye kujua mambo
mengi yanayohusu mpira wa miguu nchini, hivyo tunaamini watakuwa viongozi wazuri
kwa nafasi zao katika kuhakikisha shirikisho hilo linasonga mbele.
Tunawatakia
kila la heri Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji, huku tukiamini hawatawaangusha
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF waliowaamini kushika nafasi hizo.
TASWA
na waandishi wa habari za michezo kwa ujumla hapa nchini tunaahidi kuwapa
ushirikiano wa kutosha ili watekeleze majukumu yao ipasavyo.
Nawasilisha.
Amir
Mhando
Katibu
Mkuu TASWA
30/10/2013
DK.Shein atoa salamu za Mwisho Marehemu Balozi Sepetu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akimpa pole Mjane wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,Mama Miriam
Sepetu,alipofika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi
mmoja Mjini Unguja,kuuaga mwili wa Marehemu leo Asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein, akitia saini kitabu cha maombolezo ya Marehemu Balozi Isaac
Sepetu,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja
Mjini Unguja leo asubuhi,Marehemu alifariki juzi Jijini Dae es Salaam,na
atazikwa Kijiji kwao Mbuzini Wilaya Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein, alipokuwa akiuwaga Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,katika
ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la
zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja leo asubuhi,Marehemu alifariki juzi Jijini Dae es Salaam,na atazikwa Kijiji kwao Mbuzini Wilaya Magharibi.
zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja leo asubuhi,Marehemu alifariki juzi Jijini Dae es Salaam,na atazikwa Kijiji kwao Mbuzini Wilaya Magharibi.
Baadhi
ya Wananchi mbali mbali wakiwa katika sehemu maalum nje ya ukumbi wa
Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja,wakisubiri
kuuaga mwili wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,leo asubuhi ambapo utazikwa
Kijiji kwao Mbuzini Wilaya Magharibi.{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}
KAMPUNI YA BRAVO YAWAPATIA KAZI DUBAI WATANZANIA WENGINE WAWILI
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bravo Job Centre, Jaffar Kingwande (kulia),
akimkabidhi tiketi Amisa Ally (22), ya kwenda Dubai kufanya kazi ya
ndani aliyotafutiwa na kampuni hiyo. Anayeshudia hafla hiyo iliyofanyika
Dar es Salaam jana, ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Mohamed Omar.
(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Jazira Rashid akipatiwa tiketi ya ndege na nyaraka zingine kwa ajili ya safari ya kwenda Dubai kufanya kazi aliyotafutiwa na kampuni hiyo.
Amisa na Jazira wakiwa na baadhi ya maofisa wa Bravo pamoja na wadhamini wao
Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Omar akifafanua jambo wakati wa kuwaaga wafanyakazi hao

BABU SEYA NA MWANAYE WAANZA KUSIKILIZWA RUFAA YAO NA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA
Nguza Vicking akipunia watu mahakamani |
RAIS WA CAF AMPONGEZA MALINZI

Jamal Malinzi
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza
Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Katika
salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira
wa miguu Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi
fursa ya kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.
Amesema
CAF ina imani uwezo wake katika uongozi, uzoefu na ujuzi katika mpira
wa miguu havitausaidia mpira wa miguu Tanzania pekee bali Afrika kwa
ujumla, na kuongeza kuwa ataendeleza ushirikiano uliopo ili kuwanufaisha
zaidi vijana wa bara hili.
Rais
Hayatou amemtakia Rais Malinzi kila la kheri katika kipindi chake cha
uongozi na kumhakikishia kuwa CAF iko pamoja naye katika kusukuma mbele
gurudumu la kuendeleza mpira wa miguu.
PAMBANO LA YANGA, MGAMBO SHOOTING LAINGIZA MIL 37/-
Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mgambo Shooting lililochezwa
jana (Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh.
37,915,000.
Washabiki
waliohudhuria mechi hiyo namba 46 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na
ushindi wa mabao 3-0 walikuwa 6,515 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000,
sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) sh. 5,783,644.07, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,145,790 wakati
kila klabu ilipata sh. 8,550,741.95.
Wamiliki
wa uwanja walipata sh. 4,347,834.89, gharama za mchezo sh.
2,608,700.93, Bodi ya Ligi sh. 2,608,700.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 1,304,350.47, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) sh. 1,014,494.81.
SIMBA, KAGERA SUGAR KUUMANA KESHO
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 kesho (Oktoba 31 mwaka huu
kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Viingilio
katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1
vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.
Nayo
Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya
ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Novemba
2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union
(Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa
Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na
Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi
hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City
itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7
mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs
Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania
Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Tuesday, October 29, 2013
TAMASHA LA WAJASILIA MALI NA WAKULIMA KUFANYIKA BAGAMOYO
TAMASHA HILI LITAFANYIKA MKOA WA PWANI WILAYA YA BAGAMOYO
CHRIS BROWN AMVUNJA MTU PUA BAADA YA KUMTWANGA NGUMI
MWANAMUZIKI Chris Brown bado anaendelea kuvunja
sheria za huko Marekani. Sources mbalimbali kutoka kwenye mitandao ya uhakika
huko zinasema kwamba Chris amekamatwa pamoja na bodygurd wake baada ya Chris
mwenyewe kumpiga ngumi ya uso na kumvunja pua jamaa mmoja waliyekutana kwenye
hotel.
Habari juu ya tukio hilo linasema kwamba wasichana wawili
walikuwa wanapiga picha na Chris Brown na wakati huohuo jamaa huyo alijaribu
kwenda kwa nyuma na kuharibu picha hiyo (Photoboom). Chris Brown alivyomuona
ndio hasira zake zikamfanya amrushie ngumi ya uso na kumpata puani.
VIONGOZI, WASANII NA WANANCHI WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU BALOZI ISAAC ABRAHAM SEPETU(BABA MZAZI WA WEMA SEPETU) NYUMBANI KWAKE SINZA
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu enzi za uhai wake
Mh.
Jaji Warioba akisaini kitabu cha Maombolezo leo mchana nyumbani kwa
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akisaini kitabu cha maombolezo leo October 29, 2013 nyumbani kwa marehemu Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akisaini kitabu cha maombolezo leo October 29, 2013 nyumbani kwa marehemu Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Mama
Gertrude Mongella akisaini kitabu cha maombolezo kwenye msiba wa
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu nyumbani kwake Sinza Mori leo
October 29, 2013
Mh.
Jaji Warioba na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh.
Bernard Membe wakibadilishana mawazo kwenye msiba wa Marehemu Balozi
Isaac Abraham Sepetu leo October 29,2013
Baadhi ya viongozi waliofika msibani kwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Watu
wa karibu na marehemu waliokuwa wanaishi naye huko Zanzibar
wakizungumza jambo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
leo nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam
Mtoto mkubwa wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu, Aman Isaac Sepetu akizungumza jambo na mwandishi wa habari, Mkwaia wa Kuhenga leo October 29, 2013 nyumbani kwa Marehemu
Mtoto wa marehemu akimsalimia mama baada ya kufika msibani hapo leo mchana
Mama akiwa na mwanae baada ya kufika msibani
Wema Sepetu (katikati) akiongea na Dada yake (wa kwanza Kushoto) na (kulia) ni mama yake mama yake mzazi
Kajala alishindwa kujizuia na kuanza kulia na kupelekea watu wengine kuanza kulia kwa majonzi
Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu ukifikishwa nyumbani kwake
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu likibebwa na kupelekwa ndani
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu likibebwa na kupelekwa ndani ya nyumba
Aman Isaac Sepetu ambaye ni mtoto mkubwa wa marehemu akitoka ndani na msalaba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu likitolewa ndani ya nyumba kwa ajili ya kufanyiwa maobi na kuagwa ili kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya mazishi
Wema Sepetu akiwa ameshikiliwa baada ya kuona mwili wa baba yake mzazi Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu ukiwa kwenye jeneza
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)