Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, October 17, 2013

MAHOJIANO NA WADAU WA DARASA LA KISWAHILI WASHNGTON DC



Mtangazaji wa Jamii Production Mubelwa Bandio akiwa na Wawakilishi wa wahusika wa mpango huo, Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) Idd Sandaly pamoja na walimu Asha Nyang'anyi na Bernadeta Kaiza 
Ikizungumzwa na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika. Na inaaminika kuwa lugha ya saba kwa watumiaji wengi duniani
Na matumizi yake kama lugha inayozungumzwa na wengi wenye lugha tofauti katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaifanya lugha hii kuwa muhimu zaidi kwa watu wengi walio na mahusiano na / ama wanaotaka kujishughulisha na biashara, kazi ama diplomasia katika ukanda huo.
Kiswahili sasa kinafunzwa katika vyuo visivyopungua 50 hapa nchini Marekani, lakini pia inafundishwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali Ulaya na hata bara Asia.
Kiswahili ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na hata usalama miongoni mwa mataifa na naamini ndio sababu hata jumuiya ya waTanzania hapa Washington DC wakaona ni jambo la busara kuanzisha darasa la kufunza Kiswahili kwa watoto hapa DMV.
    
Wawakilishi wa wahusika wa mpango huo, Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) Idd Sandaly pamoja na walimu Asha Nyang'anyi na Bernadeta Kaiza wamekuwa wakarimu sana kujiunga nami katika studio za JAMII PRODUCTION hapa Washington DC.
KARIBU UUNGANE NASI

No comments :

Post a Comment