Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, October 11, 2013

MAMA SALMA KIKWETE AKIZINDUA MRADI WA MAFUNZO YA GESI NA MAFUTA YA PETROLI VETA LINDI



 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono  wanafuzi wa  Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA) , Lindi kabla ya kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana mkoani Lindi.Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah  Moshi na  wa pili Kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila na kushoto wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Nassoro  Hamidi. (Picha na Anna Nkinda-Maelezo)
 Mama Salma Kikwete , akipata maelekezo kutoka kwa mwanafunzi wa Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), Edwin  Nduguru(kushoto) jinsi deep stick inavyofanya kazi ya kupima kiwango cha oil kilichopo katika injini ya gari alipotembelea karakana ya ufundi wa magari wa chuo hicho jana. Wanaoshuhudia tukio hilo ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah  Moshi (kulia) , Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Nassoro  Hamidi (kushoto).
Mama Salma Kikwete  (aliyevaa kitenge ) akiongea jambo  na  Meneja wa  British  Gesi Tanzania ambao ndiyo wafadhili  wa mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli, Kate Sullam (kushoto) jana  kwenye   Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA) , Lindi .Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah  Moshi. 
 Mama Salma Kikwete  akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana  kwenye Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA)  Lindi . Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah  Moshi na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila.
 Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete  akikata utepe  ikiwa ni ishara kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana  kwenye Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA)  Lindi . Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA,  Mhandisi Zebadiah  Moshi na Kushoto wa tatu  ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila, kushoto ni Afisa Uhusiano wa chuo hicho Dora Tesha.
 Picha ya pamoja  na baadhi ya viongozi   na wanafunzi  wa  Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), Lindi.
 Mwanafunzi wa  wa  Chuo cha  Mafunzo ya  Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA), Lindi akimwonesha    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  (aliyevaa kitenge)  jana  kifaa cha kukata vyuma   katika karakana ya uungaji  vyuma.
Mwanafunzi wa  wa  Chuo cha  Mafunzo ya  Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), Lindi akimwonesha    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  (aliyevaa kitenge)  jana  kifaa cha  ufundi wa magari katika karakana ya ufundi wa magari.

No comments :

Post a Comment