Katika kauli iliyotoleawa na kampuni ya Airtel Tanzania kupitia Meneja Biashara Kanda Ziwa Ally Maswanya alisema”Airtel imedhamiria kusaidia shule kwa kutoa vifaa vya mbalimbali ikiwepo vya kufundishia ili kuahakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Tunatambua elimu ndiyo ufunguo wa mafanikio hivyo basi tunashirikiana na wizara ya elimu katika kuinua kiwango cha elimu sio Mwanza tu bali Tanzania kwa ujumla. Airtel itaendelea kusaidia mashule kwa kutoa vitabu na madawati ikiwa ni sehemu ya shughuli zetu za kusaidia jamii, nia yetu ni kuwafikia shule nyingi zaidi katika mikoa yote ya Tanzania alioongeza.
Akiongea wakati wa shughuli ya kugawa vitabu iliyofanyika Kanyaye Secondary katika wilaya ya ilemela, meneja wa shughuli za kijamii, Tunu Towo Kavishe alisema, tunaelewa uhaba wa madawati na vifaa vya kufundishia na tunaongeza nguvu zetu kusaidia sekta ya elimu, Airtel Tanzania inatoa fulsa sawa kwa shule zote katika mikoa yote nchini na kuhakikisha misaada tunayotoa inawafikia wanafunzi nchini kote. Leo Airtel inatoa msaada wa madawati 50 kwa shule ya sekondari Kanyaye.
“Tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini na kuhakikisha kinaongezeka, hasa kupitia upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Tangu tulipoanza mpango wetu wa kusaidia vitabu kwa shule mbali mbali za sekondari hapa nchini, takribani miaka saba iliyopita, tumeshazifikia zaidi ya shule za sekondari tofauti zipatazo 800 nchini na leo tunathibitisha dhamira yetu ya kusaidia mashule kwa kutoa madawati kanyaze secondari”, alisema Kavishe
Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu hapa nchini.
No comments :
Post a Comment