Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, June 13, 2012

Maximo kuja Yanga bado Kitendawili




Ndoto za Klabu ya Yanga yenye Maskani yake mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam za kumtwaa kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tabnzania “Taifa Stars” Mbrazili, Marcio Maximo huenda zikayeyuka kufuatia kocha huyo kuwa na mkataba Nchini Brazili.

Katika salamu zake kwa wana Yanga na watanzania kwa Ujumla Maximo amesema sio rahisi rahisi tu yeye kuja kuifundisha Yanga kwani bado wapo katika mazungumzo.

“Ni kweli nimepokea Mkataba kutoka Yanga, lakini bado tupo katika majadiliano kwasababu bado nina mkataba hapa, hivyo sio rahisi kuchukua maamuzi ya haraka”, alisema Maximo.

Aidha Maximo amesema anajisikia furaha sana na maamuzi ya Clabu ya Yanga kumhitaji yeye kukinoa kikosi hicho, lakini mbali na Yanga kumhitaji anasema pia timu kadhaa za afrika zimemhitaji zikiwepo mbili za taifa.

Amezitaja timu zinazomhitaji ni pamoja na St George ya Ethiopia pamoja na timu za taifa za Rwanda na Zimbabwe.

Aidha Kocha huyo aliyeleta ari ya watanzania kuipenda timu yao ya Taifa na soka la nyumbani kwa kauli zake za matumini “ Pamoja Tutashinda” amesema anaendelea kuifikiria Yanga maana uongozi umeonesgha nia ya kutaka kuiboresha timu.

Mapema wiki hii, Viongozi wa Yanga walidai kuwa Kocha huyo Mbrazil angewasili nchini jana tayari kwa kuinona timu hiyo iliyo poteza ubingwa kwa kichapo cha magoli 5-0 kutoka kwa mahasimu wao wakubwa Yanga na Kichapo kutoka kwa wapinzani wao wa karibu Azam kilichopelekea Yanga kuambulia nafasi ya 3 na kufungiwa kwa baadhi ya wachezaji wake. zaidi tembeleahttp://mrokim.blogspot.com/2012/06/maximo-kuja-yanga-bado-kitendawili.html

No comments :

Post a Comment