Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, March 6, 2014

LG yazindua jokofu lenye kutunza baridi kwa muda mrefu.

LG yazindua jokofu lenye kutunza baridi kwa muda mrefu.




Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Hotpoint Tanzania BW. Mayur Parikh wa pili kushoto na meneja masoko wa kanda wa kampuni hiyo BW, Shakti Vellu wakizindua Jokovu lenye kutunza baridi la kampuni ya LG picha na www.burudan.blogspot.com
Feb 14, 2014: Kampuni ya vifaa vya Umeme ya LG leo imezindua jokofu la kisasa zaidi yenye uwezo wa kutunza ubaridi kwa muda wa masaa saba upande wa jokofu ya kawaida na masaa kumi kwa upande wa friza hata pindi umeme unapokuwa umekatika.
Bidhaa hii mpya imezinduliwa mahususi kutokana na tatizo lililo kithiri la katizo la umeme ambalo hukumba maeneo mengi ya nchi na kusababisha vifaa vya umeme kukosa matumizi kwa muda mrefu.
Aidha tatizo hili la kukatika kwa umeme mara kwa mara kumepelekea makapuni kama LG kutanua wigo wao katika kutafuta suluhu na hivyo kubuni  teknolojia zenye usasa uliopindukia katika ubunifu wa vifaa vitavyo himili nyakati umeme unapokosekana. Ni katika ubunifu huo ndipo LG ikatengeneza jokofu hili jipya lisilogandisha barafu kwenye “friza” linaloweza kutunza ubaridi katika sehemu ya ‘friji” kwa zaidi ya masaa saba hasa pale umeme unapokatika kwa kipindi kirefu.
Akiongea siku ya uzinduzi Appliances Product Manager LG East Africa, Oktae Kim alisema uzinduzi huu umelenga katika ubunifu mkubwa unaohusiana na mahitaji ya mteja na jinsi ya kuyatatua. Hivyo basi tunajitahidi kubuni bidhaa ambazo zina kidhi mahitaji ya wateja wetu.
Teknolojia iliyotumika inahusianisha valve kwenye jokofu ambayo hufunguka pale ambapo kunapokosekana na umeme. Valve hii inasambaza ubaridi kwenye vifaa vingine vilivyoundwa maalumu kutunda ubaridi na pindi umeme ukatikapo vipaa hivi huanza kutoa ubaridi kwa muda wa saa saba.
Bwana Kim amesema: “Evercool  inapooza mara tatu zaidi  kwa kutumia evaporator tatu. Evaporator kuu inatumia umeme na mbili zinafanya kazi bila kutumia umeme. Kwa hiyo sasa unaweza kufaidi vinywaji baridi na kuepuka kuharibika kwa chakula chako kwenye jokofu mara umeme unapokatika”.
LG ina visahani vya kugandishia barafu ambavyo vina uwezo wa kugandisha barafu kwa haraka ya zaid ya asilimia 20. Imetengenezwa kwa umahiri na maeneo ya kutosha kwa ndani na hivyo kukuwezesha kupata sehemu ya kutosha ndani wakati wa kuweka vitu. Sasa unaweza kutunza mboga na matunda vizuri bila kuogopa vitu kuharibika kutokana na mrudikano wa vitu nahivyo kusababisha unyevunyevu unaopelekea kuharibu vyakula. Na wakati wa kipindi cha joto kali, jokofu hili la milango miwili litakushangaza kwa kutunza chakula kwa hali ya juu.
Pia  mwanga wa LED unang’aa zaidi, unadumu kwa muda mrefu na unatumia umeme mdogo. Na mtu atakayenunua jokofu hili hahitaji kutafuta ‘Stabilizer” kwani jokofu hili linaweza kufanya kazi vizuri hata wakati umeme unapokuwa mdogo.
Bw. Kim aliongezea kwakusema :compressor za LG ni Imara na tunakupa guarantee ya mwaka mzima” Pia aliongeza kuwa wanajitahidi kuhakikisha wanaendelea kuzalisha bidhaa za kisasa na zinazoendana na mahitaji halisi ya watu.

No comments :

Post a Comment