Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Mizengo
Pinda(kushoto) wakati wa semina ya kuhusu kanuni za bunge hilo leo mjini
Dodoma.
Na Magreth
Kinabo,Dodoma
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuhutubia Bunge
Maalum Machi 21, mwaka huu mjini Dodoma.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa bunge
hilo, Yahya Khamis Hamad wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa waandishi wa habari wa
ofisi za Bunge mjini Dodoma.
“Kwa mujibu wa kanuni ya 75 (1), Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge Maalum siku ya Ijumaa Machi 21 ,mwaka
2014 saa 10:jioni, ambapo wageni waalikwa wote watatakiwa kuwa wameingia na
kuketi katika maeneo watakayoelekezwa
saa 9:00 alasiri,” alisema Katibu huyo.
Aidha Katibu huyo alisema ratiba ya shughuli hiyo
itaanza na kikao cha Bunge saa 9:10 na baadae kikao hicho kitaanza saa 9:20 kwa
ajili ya kumpokea Rais .
Aliongeza
kuwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge, Rais Kikwete atapokewa na
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Naibu Katibu wa Bunge Maalum, ambapo
baadae ataelekea katika jukwaa maalum kwa ajili ya kupokea salamu za heshima na
kukagua Gwaride Maalum ambalo limeandaliwa na jeshi la polisi.
Baada ya shughuli zote kufanyika katika viwanja vya
Bunge kumalizika, utaratibu umewekwa kwa
viongozi kuingia Bungeni kwa maandamano maalum.
Viongozi watakaohusika katika maandamano hayo ni
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar
,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Rais wa Zanzibar na hatimaye Rais
Kikwete ambaye atafuatana na Mwenyekiti wa bunge hilo.
Katibu huyo aliwataja viongozi wegine walioalikwa
kuwa ni viongozi wa kitaifa na watendaji wakuu kutoka pande zote Muungano, viongozi
wa kitaifa wastaafu,ambao ni marais wastaafu kutoka pande zote za muungano,
mawaziri wakuu wastaafu, waziri kiongozimstaafu na maspika wastaafu.
Viongozi wengine ni mama Maria Nyerere, Mama Shadia
Karume na Mwenyekiti na wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba.
Wageni wengine walioalikwa katika utaratibu huo ni
taasisi za dini, zisizozakiserikali, tansia
ya habari, vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu, taasisi za
elimu, vyama vya watu wenye ulemavu, wafanyakazi,wafugaji,wavuvi, wakulima na
wawakilishi kutoka sekta binafsi.
Kwa mujibu wa
ratiba ya shughuli hiyo Rais Kikwete anatarajiwa kuhutubia bunge hilo kwa muda
wa saa moja. Hivyo shughuli hizo zitakamilika majira ya saa 12:00jioni.
No comments :
Post a Comment