PAMBANO LA NGUMI LA KUKUMBUKWA
Donovan "Razor" Ruddock Vs Lennox Claudius Lewis HILI
lilikuwa ni moja ya mapambano yaliyowavuta mashabiki wengi wa ngumi
duniani, na hasa kutokana na umahiri wa mabondia wote wawili.Ilikuwa
ni katika mji wa Halloween, Oktoba 31, 1992 katika ukumbi wa Earls
Court jijini London, Uingereza ambako mabondia hao walikutana. Kwa
upande wa Lennox Lewis, ilikuwa ni kipimo cha uhakika kwani hilo
lilikuwa pambano lake la kwanza kukutana na bondia wa 'ukweli' Donovan
"Razor" Ruddock aliyeogopwa kwa ngumi nzito na zenye nguvu.Ruddock
alikuwa ni mpiganaji wa kiwango cha juu duniani, wenyewe wanasema
'world class fighter'. Awali alikuwa amemuhenyesha sana Mike Tyson
katika mapambano yao yote mawili, lakini pia Ruddock alikuwa amemchana
chana bingwa wa zamani Michael Dokes.Lakini
umuhimu mwingine wa pambano hilo lilikuwa ni la kumtafuta atakayewania
ubingwa dunia wa WBC kwa kupambana na Riddick Bowe aliyekuwa mtetezi wa
mkanda huo. Je,
Lewis atakuwa bingwa wa dunia kutoka Uingereza baada ya miaka 100 tangu
afanye hivyo Henry Cooper na Bob Fitzsimmons ambaye alikuwa wa mwisho
kubeba ubingwa wa dunia akiwa Muingereza? Ndilo swali lililokuwa
likiulizwa na mashabiki wengi wa ngumi hasa wa Uingereza.Hakuna
aliyedhani kuwa pambano hilo lingekuwa jepesi, Lewis alikuwa ni
bondia anayeheshimika kwa kuwa bingwa wa medali ya dhahabu (Olympic Gold
Medalist) lakini pia hadi katika pambano hilo alikuwa hajapoteza hata
moja.Alishawadunda
mabondia kama Tyrell Biggs, Mike Weaver na Gary Mason, lakini
hakuwahi kupata pambano dhidi ya bondia anayesifika na kuogopwa kwa
nguvu na uzito wa ngumi kama Razor, kwa hakika huu ulikuwa mtihani
mkubwa kwa Lewis.*PambanoIlishitusha,
wengi hawakuamini lakini ndivyo ilivyokuwa, pambano hilo likawa jepesi
ajabu kwa Lewis ! Hakuna aliyeweza kutabiri kama Lewis angeshinda
pambano hilo kwa ulaini kiasi kile lakini kocha wake wa zamani, Pepé
Correa alidai kwamba alitabiri ushindi wa mapema kwa Lewis.1. Raundi ya kwanza: Mabondia
wote wanaitwa kusalimiana katikati ya ulingo, wanakutana na kutizamana
uso kwa uso, Ruddock anamwangalia Lewis kwa macho ya ukali na vitisho,
lakini Lewis anakuwa mpole kama pande la barafu. Nakukumbusha
tu kuwa Lewis kabla ya kuchukua uraia wa Uingereza alikuwa na uraia wa
Canada. Ruddock naye ni mzaliwa wa Canada, wote walikuwa kwenye timu ya
ngumi ya taifa ya ridhaa na walikuwa wanajuana vizuri. Lewis ana uraia
wa Uingereza na Canada.Baada
ya kusalimiana katikati ya ulingo, kila mmoja anarudi kwenye kona yake
huru (neutral corner) kisha kengele inalia kuashiria raundi ya kwanza.
Ruddock anakuwa wa kwanza kutoka kwenye kona yake na kumfuata kwa nguvu
Lewis.Mabondia wote
wanashambuliana kwa tahadhari, wanaonekana wakiwa na nguvu za miili na
wakiwa katika hali nzuri, hiyo inafanya wachambuzi wa ngumi kuamini
kwamba pambano hilo litakwenda raundi nyingi.Lakini
wakati raundi ya kwanza inaelekea ukingoni, linatokea tukio la
kustajaabisha! Ruddock, anafanya kosa la mwaka, anapiga ngumi ya
kudonoa ya kushoto (left jab) katika chembe ya kifua cha Lewis, na
wakati mkono wake ukiwa umenyooka, anakuwa ameacha uwazi kwenye taya
lake la kulia.Lewis
anaioa nafasi hiyo, anaona namna taya la Ruddock lilivyobaki 'uchi'
(wazi), hana muda wa kupoteza, anakaza msuli wa mkono wake wa kulia na
kushusha fataki kali linalokamata shabaha sawia!Ngumi
ile ya kulia (right ), inatua kwenye taya la Ruddock (vitendo hivyo
vyote vinatokea haraka sana katika muda wa sekunde mbili u )Ngumi
ile inamwingia Ruddock vizuri miguu yake inakosa nguvu na anabinuka na
kuanguka chini kama furushi la dagaa wa Mwanza! Kwanza umati unashangaa
kisha unashangilia kwa mshangao! Wanashangaa nguvu ile ya ngumi Lewis
alikoipata!Lakini
wakati Ruddock anajizoa pale chini, kengele ya kuashiria kumalizika kwa
raundi ya kwanza inalia na hivyo mwanamume anaokolewa na kengele katika
raundi ya kwanza, anakwenda kwenye kona yake na ulevi wa sumbwi lile.Kocha
wa Ruddock, Floyd Patterson, anamwambia bondia wake kutulia na kumjenga
kisaikolojia kwa ajili ya raundi ya pili, lakini kwa hakika ngumi ile
aliyodundwa Ruddock imemuumiza vibaya hakuwa ngumi ya mzaha, lilikuwa ni
kombora.2. Raundi ya Pili:Raundi
ya pili inapoanza, Lewis anakuwa na tahadhari zaidi, pengine
anakumbuka umahiri wa Ruddock ambaye katika mpambano yake alishwahi
kupigwa na kudondoka chini lakini akaja kushinda.Razor
anaendelea na mashambulizi katika raundi hii, anaachia 'right' kali ya
kulia na inatua kichwani kwa Lennox ambaye anajikaza na kujibu
shambulizi hilo.Lennox
anajibu kwa mchanganyiko wa ngumi (combination), kumbuka mkono wa
kushoto wa Lewis ni kama risasi, unafyatuka kwa haraka na Rudock
anashindwa kuziona 'jabs' kadhaa zinazodondokea usoni mwake na kisha
ngumi nyingine ya kulia inafuatia na kutua kwenye kichwa chake, Ruddock
anakwenda chini kama mlevi wa kangara kwa mara ya pili katika pambano
hilo.Ruddock anahesabiwa na kunyanyuka lakini akiyumba kwa ulevi na mwamuzi anaporuhusu pambano liendelee,Lewis anachomoka spidi lakini kwa tahadhari ya kwenda kummaliza Ruddock.
No comments :
Post a Comment