Baadhi ya majengo ya mradi huo yakiendelea na ujenzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk.
Ramadhan Dau (kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi wa NSSF walipotembelea mradi wa Dege ECO Village wa
Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu akifuatilia.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau
akizungumzia kwa kifupi mradi wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa
ujulikanao 'Dege ECO Village' unaoendelea Kigamboni.
Viongozi mbalimbali wa NSSF pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa
NSSF wakiangalia video ya muonekano wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa
ujulikanao 'Dege ECO Village' unaoendelea Kigamboni, utakavyo kuwa baada
ya kukamilika.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azimio, Mohamed Ikubal (mwenye kanzu) akitoa
ufafanuzi kwa wajumbe wa Bodi ya NSSF kwenye jengo la mauzo ya nyumba za
mradi wa Dege ECO Village, eneo hilo ndilo litakalokuwa likiendesha
mauzo na taratibu zote za mradi baada ya kukamilika.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azimio, Mohamed Ikubal (mwenye kanzu)
akiwaonesha wajumbe wa Bodi ya NSSF jengo la mauzo ya nyumba za mradi wa
Dege ECO Village, eneo hilo ndilo litakalokuwa likiendesha mauzo na
taratibu zote za mradi baada ya kukamilika. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu (katikati) akizungumza na viongozi mbalimbali wa NSSF pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF walipotembelea mradi wa 'Dege ECO Village' unaoendelea Kigamboni, utakao kuwa na nyumba bora na za kisasa eneo hilo.
Viongozi mbalimbali wa NSSF pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa
NSSF wakiangalia video ya muonekano wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa
ujulikanao 'Dege ECO Village' unaoendelea Kigamboni, utakavyo kuwa baada
ya kukamilika.
WAJUMBE
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
wametembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa unaojulikana kwa jina
la Dege ECO Village unaojengwa eneo la Kigamboni nje kidogo ya Jiji la
Dar es Salaam.
Ujenzi huo
wa mji wa kisasa ambao utakuwa na nyumba za kuishi za kisasa za watu wa
kipato cha kati unajumuisha ujenzi wa nyumba zaidi ya 7,000 zikiwa na
huduma zote za kujamii eneo moja.
Akizungumzia
mradi huo mkubwa unaotekelezwa kati ya NSSF kwa ushirikiano na kampuni
ya Azimio, Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo aliwaeleza wajumbe
wa Bodi ya shirika hilo kuwa ujenzi wa makazi hayo ya kisasa kwa
wananchi wa kipato cha kati unaendelea vizuri.
Alisema
eneo hilo litakuwa na nyumba bora na za kisasa zikiwa na huduma zote za
msingi kwa jamii kama maduka, shule, hospitali, masoko, viwanja vya
michezi, kituo cha polisi, kituo cha zimamoto, eneo la ujenzi wa majengo
ya ibada, majengo ya burudani pamoja na miundombinu ya kisasa ya maji
safi na maji taka.
Alisema
ujenzi wa mradi huo wa kisasa utakapokamilika utakuwa na uwezo wa
kuchukua watu takribani elfu 30 ambao watapata makazi bora na ya kisasa
katika eneo hilo la Kigamboni.
Akifafanua
zaidi Mhandisi Msemo alisema ujenzi wa nyumba hizo utakuwa na awamu
tatu; ambapo awamu ya kwanza itakamilika mwaka 2016 ikiwa na nyumba
2,500, huku awamu ya pili ya ujenzi itakamilika 2017 ikiwa na nyumba
bora na za kisasa 2,500.
“…Awamu ya tatu tunatarajia ikamilike mwaka 2018 hii itakuwa na nyumba
2,460,” alisema Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi Msemo akifafanua zaidi
kwa waandishi wa habari juu ya mradi huo.
Aidha
akijibu baadhi ya maswali ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa NSSF,
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dk. Ramadhan Dau alisema nyumba zote
zitakazojengwa katika mradi huo zitauzwa kwa watu wenye kipato cha kati
watakaohitaji.
Alisema
zipo zitakazouzwa kwa fedha taslimu na nyingine kwa makubaliano ya
mikopo kadri ya utaratibu utakavyotolewa na shirika hilo pamoja na
mwekezaji walieshirikiana naye kutekeleza mradi huo, yaani kampuni ya
Azimio.
Alisema
bei ya nyumba moja inakadiriwa kuuzwa kuanzia dola za Kimarekani elfu 80
hadi 130, na tayari wameanza kupokea fedha na maombi kwa watakaohitaji
au kulipa kidogo kidogo kwa utaratibu utakao kubalika.
Hata hivyo
baadhi ya wajumbe wa bodi walipongeza juhudi za uongozi wa NSSF kwa
kubuni mradi huo wa kisasa ambao utawasaidia wengi na hivyo kushauri
kuna haja ya kutekelezwa na mikoa mingine.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments :
Post a Comment