Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, August 3, 2014

Chiku Gallawa mgeni rasmi Handeni Kwetu Foundation



MKUU wa Mkoa wa  Tanga, Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika uzinduzi wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation, utakaofanyika Jumanne ya Agosti 5, katika Ukumbi wa Vijana Social Hall,  Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo la uzinduzi wa taasisi hiyo limepangwa kuanza saa 10 za jioni ambapo wamealikwa wageni mbalimbali kwa ajili ya kuitambulisha kabla ya kuanza kazi zake rasmi nchini Tanzania.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa taasisi hiyo, Kambi Mbwana, alisema kuwa wameona wamualike RC Gallawa kuwa mgeni rasmi
kwakuwa ni miongoni mwa viongozi makini na wenye kiu ya maendeleo hapa nchini.

Alisema kuwa kitendo cha kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa Tanga, kinaonyesha namna gani viongozi wa serikali wanashirikiana na wadau wote kwa ajili ya kufanikisha mipango ya kimaendeleo.

“Tanzania imejaliwa kuwa na viongozi makini mno, hivyo taasisi imemualika Mheshimiwa Gallawa kuwa mgeni wake rasmi ili ashirikiane na wageni waalikwa kuitambulisha taasisi.

“Tunaamini kwa pamoja tutafanikisha kuitambulisha taasisi kwa
wadau wote, hususan Watanzania kwa kupitia Handeni Kwetu Foundation,
ukizingatia kuwa imesajiliwa kufanya kazi zake nchini nzima,” alisema.


Kwa mujibu wa Mbwana, sera na mikakati ya taasisi hiyo itaanikwa
katika utambulisho huo utakaokuwa na malengo mahususi ya kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha masuala ya utawala bora.

No comments :

Post a Comment