Banda
la Mtandao wa mashirika yapatayo 30 ya kupambana na matumizi ya kupita
kiasi ya pombe nchini (Tanzania Network Against Alcohol Abuse) kwenye
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.(Picha na Zainul
Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
imeshauriwa kutunga sera madhubuti ya udhibiti wa pombe katika jamii
ili pamoja na mambo mengine kuhakikisha vijana wanalindwa dhidi ya
bidhaa hiyo kwenye soko.
Akizungumza
na Moblog Tanzania jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo kikuu
wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana, Msemaji wa Mtandao
wa kupambana matumizi ya pombe kupita kiasi (Tanzania Network Against
Alcohol Abuse) Bw, Mathias Kimiro amesema kwamba kuna umuhimu wa
serikali kutunga sera mpya ya pombe ili kuzuia madhara kwa vijana na
taifa kwa ujumla.
“Kwa
kawaida matumizi ya pombe kupita kiasi ina madhara makubwa katika afya
ya mtumiaji lakini vile vile ina madhara kwenye familia kupitia kaya
moja moja na kusababisha mateso kwa familia hasa watoto,” amesema Bw
Kimiro
Amesema
kwamba umuhimu wa kuwa na sera madhubuti ya kudhibiti pombe katika
jamii ni kuangalia upya ni kwa kiwango ngani matangazo ya pombe
yanavyohamasisha unywaji kupita kiasi kwenye jamii. Bw
Kimiro aliongeza kwamba mashirika yasiyo ya kiserikali yataendelea
kuwakumbusha mamlaka zinazohusika umuhimu wa kuwa na sera ya kudhibiti
pombe katika jamii pamoja na kuangalia madhara ya matangazo kwa wasomaji
wa mabango.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makangarale Youth Theatre, ambao ni taasisi chini ya
Tanzania Network Against Alcohol Abuse (TAAnet), Bw. Ismael Mnikite
akifafanua jambo kwa Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni,
Vijana na Michezo, Bibi Venerose Mtenga wakati wa maadhimisho hayo.
No comments :
Post a Comment