KUPITIA
Gazeti la Mwanaspoti ambalo kwa mujibu wa takwimu za mauzo nchini ni
wazi kwamba halina mpinzani, msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond
Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Wema Sepetu
anayosema itafungwa hivi karibuni.Msanii
huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na
Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano.
Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo
maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.
“Ndoa
ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo
yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata
ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.“Unajua
nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani
wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka
tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje
kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa
tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni,
unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata
Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu
vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na
husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.”
Taarifa
kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema
Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’
alisema: “Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti
hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu
nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa
haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari,
mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,”
alisema.
Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.
“Hata
hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati mwingine
inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza,” aliongeza.
Kuhusu
taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema: “Hatuna tatizo
watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na hatuwezi
kujibishana.
“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu.
No comments :
Post a Comment