Banda la Mbeya yetu Blog
Mtoa
Maelezo kutoka Tone Multimedia Group kupitia Mtandao wao wa Mbeya yetu
Blog Fredy Anthony Njeje wa kwanza kulia akitoa maelezo ya kina kwa
Mkuu wa Mkoa wa katavi Mh.Dr Rajab Lutengwe jinsi mtandao wa Mbeya
yetu unavyofanya kazi pia unavyosaidia upatikanaji wa habari kwa urahisi
kabisa. Pia kuekeza sababu za Kushiriki katika mashindano ya nane nane
ikiwa ni pamoja na Kutoa elimu juu ya mitandao ya kijamii na faida zake
hasa upande wa Blogs na matumizi sahihi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Dr Rajab Lutengwe akiwapongeza Tone Multimedia Group kwa kuanzisha Mtandao wa Blogs za Mikoa na Mbeya yetu Blog ikiwemo ndani yake kwa ubunifu mkubwa na kazi kubwa wanayoifanya ili kufikisha taarifa kwa kila mkoa na Mtandao wake na kusisitiza kuwa ni vizuri kuendelea na moyo huo huo ili kuendelea kuhabarisha jamii kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Dr Rajabu Lutengwe wa tatu kutoka kushoto akitoa ushauri kwa Blog ya katavi yetu baada ya kuweka Mnyama Tembo awekwe mnyama Kiboko kwa sababu ndiye alama kubwa ya utalii katika Mbuga ya Wanyama ya Katavi.
Fredy Anthony Njeje akiendelea kumpa maelezo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr. Rajab Lutengwe juu ya kazi zengine ambazo kampuni ya Tone Multimedia Group inazifanya ikiwa ni pamoja na Radio ya Mtandaoni Tone Radio, Mtandao Maalum ambao unawahusu wanafunzi Matukio na wanavyuo, Huduma Mpya ya kupata habari kwa njia ya Simu kwa watu wenye Whatsapp Tone Mobile News, Mtandao wa watanzania waishio nje ya nchi pamoja na kazi zote za ambazo kampuni inazifanya. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwandishi wa Mbeya yetu Venance Matinya.
Mwandishi
Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango wa kwanza upande wa kushoto
akiendelea kutia maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea katika banda
la Mbeya yetu blog.
************
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dr. Rajab Lutengwe, ameusifia mtandao wa kijamii wa
Mbeya Yetu Unaomilikiwa na Tone Multimedia Group kwa kuonesha mabadaliko
ya kwenda na wakati katika teknolojia ya mawasiliano na habari teknolojia ya kisasa.
Dr. Lutengwe
ametoa pongezi hizo hivi wakati akitoa tathmini yake mara baada ya
kutembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho ya wakulima maarufu kama Nane nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Alisema
kuwa mtandao huu umeonesha chachu ya mabadaliko katika sekta ya
mawasiliano kwa kukuza na kutangaza uchumi wa ndani na nje ya nchi kwa
kurusha matukio mbalimbali yanayoendelea katika maonesho hayo.
“Nimewapenda sana wale vijana wa mtandao wa Mbeya Yetu kwa
kazi yao ya kurusha matukio yanayoendelea kwenye viwanja hivi, huko
tunakoelekea hivi sasa katika kukuza biashara ya mazao yetu ni lazima
tutangaze kupitia ‘Google’ Mbeya yetu imeonesha njia sahihihi ya
kukabiliana na soko la uchumi na kama wataenedelea na kasi ile watafika
mbali” alisema.
Alisema
kwa kutumia mitandao ya kijamii taarifa mbalimbali zinazohusu sekta ya
kilimo zinawafikia wananchi wengi kwa mara moja na kuwa ni muhimu kwa
halmshauri za wilaya kuanzisha Tovuti na Blogu ili kuendana na wakati.
No comments :
Post a Comment