Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, August 3, 2014

OLD IS GOLD NA SPICE MODERN TAARAB KUFUNIKA NDANI YA SAFARI CARNIVAL LEO



WAPENZI wa nyimbo za zamani za taarabu asilia nchini, leo wanatarajiwa kupata burudani safi na ya aina yake  kutoka kundi la Spice Modern Taarab,  ndani ya ukumbi wa  Safari Carnival uliopo Kawe, (opposite) na Clouds fm katika gate la kuingilia Escape 1.

Kwa kiingilio cha sh 5000 tu, kuanzia saa mbili usiku mpaka majogoo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, ambao ni miongoni mwa wadhamini wa onyesho hilo, amewasihi wadau kujitokeza kwa wingi kuuenzi usiku huo kwa kukumbushiana enzi.

Asia Idarous alisema onyesho hilo maarufu kwa jina la ‘Old is Gold na Spice Modern Taarab,’  tayari limeanza kujizolea umaarufu kwa wadau ambapo wanakutana kwa pamoja na kufurahia shoo hizo.
“Kwa kiingilio cha sh 5,000 tu, wadau watafurahia shoo kabambe kutoka kwa Spice Modern Taarab kwa kupata nyimbo za mwambao hasa zile zilizokuwa zikipendwa, kuanzia saa 2 usiku hadi saa 8 usiku,” alisema Asia Idarous.

Spice Modern taarab wanatamba na nyimbo mbalimbali ambapo watapiga na nyimbo zilizowahi kutamba miaka ya zamani kama ambazo zimekuwa gumzo kipindi hicho ni pamoja na ‘Pendo kitu cha hiari’, ‘Dunia ina fisadi,’ ‘Kasha’ na nyingine nyingi.

Aidha aliwataja Wadhamini wengine katika usiku huo wa taarabu asilia ni Times FM, Fabak Fashions na Safari Carnival.

No comments :

Post a Comment