Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, July 31, 2009

ZAIN YAFUNGA NDOA NA DAWASCO


Ofisa Biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Zain Bw.Chiruyi Walingo akipeana mkono na Ofisa Biashara wa Shirika la maji safi na maji taka(DAWASCO) Bw.Raymond Mndolwa Dar es Salaam jana baada ya uzinduzi wa ulipaji wa Ankara za maji kwa wateja wa Zain kupitia huduma ya Zap.(Picha na Rajabu Mhamila)

FM ACADEMIA KUZINDUA DVD YA LIVE SHOW ZAO


Rais wa bendi ya Fm Academia Nyoshi Elsadat akiimba wakati wa utambulisho wa uzinduzi wa DVD ya Live, Utamu wa Vanila,jana inayotarajiwa kuzinduriwa Dar es salaam leo kushoto ni Ofisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkonono ya Zaini Celin Njuju, ambao ni wadhamini.(Picha na Rajabu Mhamila)

Thursday, July 30, 2009

Miss Temeke ndani ya TBL

Warembo wa shindano la Miss Temeke walipotembelea kampuni ya bia Tanzania TBL, hapa wanapewa maelezo na mpishi mkuu wa TBL

Wednesday, July 29, 2009

YANGA ? DUH !!! KUMEKUCHA


Yanga wajifua ufukweni
Mazoezi ya Yanga ufukweni si mchezo. Hali ndiyo kama hii ya kubebana mindo mmoja.

Sunday, July 26, 2009

UBINGWA SIMBA KABLA YA LIGI KUMALIZIKA - PHIRI


Wachezaji wa timu ya soka ya Simba wakiwa mazoezini Chukwani mjini Zanzibar kujiandaa na Ligi Kuu Bara.
Haya ni maandalizi ya klabu ya Simba iliyojichimbia visiwani Zanzibar kabla ya ligi kuu Tanzania bara!
KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Simba, Patrick Phiri amesisitiza msimamo wake kwamba timu yake inatisha mwaka huu, na kuna uwezekano wa timu hiyo kuweza kutwaa ubingwa wa hata kabla ya ya ligi kumalizika.

Kocha huyo raia wa Zambia amesema kutokana na maandalizi yanavyokwenda, watani wao wa jadi Yanga, ambao msimu uliopita waliwatambia kwa kuwafunga mara moja na kutoka nao sare mara moja, safari hii watarajie kipigo kutoka kwa timu yake.

Kocha huyo aliyekuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi Chukwani mjini hapa ambapo timu hiyo imeweka kambi, ameusifu uongozi wa Simba ulivyojipanga vizuri katika maandilizi na hivyo kurahisisha ratiba yake ya mazoezi.

Phiri alifahamisha kuwa, tangu timu ilipowasili hapa Jula 19, hakuna tatizo lililojitokeza kwa vile pahala walipofikia pameandaliwa vizuri ambapo wachezaji na
uongozi uliopo hapa wamepafurahia.

"Maandalizi ni mazuri, hakuna malalamiko kutoka kwangu wala kwa wachezaji, sana sana
uongozi umenipa deni kubwa la kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Bara mwaka huu, "
alisema Phiri.

Alisema, anajua jinsi mashabiki wa Simba walivyokuwa na kiu ya kuiona timu yao inatwaa ubingwa, nawaahidi kiu hiyo itamalizika na ubingwa huo utapatikana tena kwa kuwafunga watani wetu wa jadi," alisema.

Alisema, Simba ilikuwa nzuri tangu msimu uliopita lakini ilifanya vibaya, kutokana na kukosa stamina pamoja na ufundi, lakini msimu huu inatisha kwa sababu kamati ya usajili imefanya kazi nzuri.

"Hadi hivi sasa siwezi kusema mchezaji gani yupo mbele zaidi kwa mazoezi, wote wanajituma sana, na kama utawachunguza vizuri huwezi kumjua yupi mgeni na yupi mwenyeji kwa kweli wananipa raha sana," alisema.

YANGA - HATUENDI MWANZA NG`O!!! KAMBI YAWEKWA YANGA HOUSE

Hili ni jengo la Yanga (YANGA HOUSE)likkiwa katika ukarabati mkubwa wa kuhakikisha linakuwa la kibiashara na kupunguza gharama za klabu kuweka kambi.
Katika harakati za kujiandaa na ligi kuu ya msimu ujao Uongozi wa klabu ya Yanga umesema hauna sababu yoyote ya kwenda sehemu nyingine kuweka kambi kwani tayari jengo lao limeshakamilika kwa asilimia tisini na tano.
Iman Mahugira Madega ni mwenyekiti wa timu hiyo yenye maskani yake jangwani Jijini Dar es salaam amesema taarifa za kambi ya klabu hiyo kwenda Mwanza si za kweli na sasa wataweka kambi katika jengo la klabu hiyo na wanafanya kila jitihada pamoja na uwanja ukamilke haraka ili uweze kutumika katika michezo yao ya ligi kuu.
Madega ameongeza kuwa mpaka sasa zaidi ya shilingi bilioni moja nukta mbili zimekwishatumika ambapo kuna vyumba vya kulala ishirini na tisa ambapo kila chumba watalala wachezaji wawili wawili pamoja na sehemu ya kuogelea swimming pool na sehemu za kupumzikia.
Akizungumzia kuhusu katibu ,mhasibu na msemaji wa kuajiriwa amesema suala hilo lipo kwenye mchakato wa kutafuta watendaji hao kwani wanafahamu kuwa hawataweza kushiriki ligi kuu bila ya kutekeleza agizo hilo la Tff.

TV TUMAINI KUCHANGISHA FEDHA KWA SMS!!!

Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,Methodius Kilaini,akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia Tv Tumaini, ili kuiwezesha kurusha matangazo yake kwa njia ya satalaiti,iliyofanyika Dar es salaam mwishoni mwa wiki kushoto ni mjumbe wa kamati ya uendeshaji wa Televisheni hiyo Bw.Joseph Temu.(Picha na Rajabu Mhamila)

Akizindua Harambee hiyo mwenyekiti wa bodi ya TTV Padri Paulo Makundi amewataka wananchi kuchangia Televisheni hiyo kwa kutuma ujumbe wa maandishi wenye neno Tumaini kwenda 15543.
Amesema Gharama za ujumbe huo utakuwa ni shilingi 500, amesema zinahitajika milioni 400 kukamilisha kujiunga kwenye mtandao wa Setilaiti.

Friday, July 24, 2009

TFF YAONGEZA MAKALI KATIKA MSUMENO WA KANUNI ZA LIGI KUU!!!

Shirikisho la kandanda Tanzania limeongeza makali katika msumeno wake wa kanuni za ligi kuu kwa wachezaji na klabu ili kuleta nidhamu mchezoni pamoja na kuboresha soka la Tanzania kuelekea katika ushindani zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela amesema moja ya matayarisho ya ligi kuu msimu ujao ni kuwepo na kanuni bora za ligi ili iwe bora.

Amesema ili kuhakikisha klabu pamoja na wachezaji wanawajibika TFF itatengeneza vitambulisho maalum kwa ajili ya wachezaji wote wa ligi kuu na hawataruhusiwa kucheza kama hawatokuwa navyo.

Amesema mchezaji atakayeshangilia goli kupitiliza na kupoteza muda au kuonyesha ishara ya kashfa au matusi kwa mashabiki wa timu pinzani, mchezaji huyo atafungiwa kucheza michezo mitatu pamoja na faini ya shilingi laki tano.

Mwakalebela amezungumzia swala la klabu kuingia mitini mchezoni baada ya kuhudhuria kikao cha maandalizi itatozwa faini ya shilingi milioni tano pamoja na kushushwa daraja, wakati timu ambayo haitafika kituoni itapoteza mchezo na kutozwa faini ya shilingi milioni tatu huku ikishushwa madaraja mawili.

Mbali na TFF kuongeza makali ya msumeno katika kanuni za ligi kuu Tanzania bara ambazo sasa zitatumika misimu yote na si mwaka mmoja mmoja kama ilivyokuwa awali, Mwakalebela amesema klabu zitaneemeka kwa kuongezewa mgawawo wa mapato ya mlangoni toka asilimia 25 hadi asilimia 30.

Aidha wawakilishi wa michuano ya kombe la shirikisho na ligi ya mabingwa sasa watakuwa wakicheza mchezo wa Ngao ya Hisani, ambapo kwa mwaka huu mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Agosti 16.

WASHINDI SABA WA KISMAT SMS WAPATIKANA

Mfanyakazi wa Kampuni ya Selcom Bi.Judith Mtui (kushoto) akibonyeza kitufe cha kompyuta kwa ajiri ya kutafuta washindi saba wa Kismat SMS bahati nasibu ya Taifa, anaeshughudia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini Bw.Abdallah Ahmed na Meneja masoko wa Kampuni ya Selcom,Juma Mgori, ambao ni waendeshaji wa Bahati nasibu hiyo.(Picha na Rajabu Mhamila)

AURORA YA KABIDHI BASI KWA ALBINO FC

Mkurugenzi wa Kampuni ya Aurora, Ally Suleiman (kushoto) akimkabidhi ufunguo wa basi mwenyekiti wa Timu ya Albino, Abdulazizi Abdallah Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri nalo kwenda dodoma kucheza mechi na wabunge.(Picha na Rajabu Mhamila)

Wednesday, July 22, 2009

JAPHERT KASEBA KUZIPIGA NA FRANCIS CHEKA OKTOBA 3

Mabondia, Francis Cheka (kushoto) na Japhert Kaseba, wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao unaotarajia kufanyika Oktoba 3.(Picha na Rajabu Mhamnila)Japhet Kaseba ambaye ni bingwa wa Dunia K-ONE mchezo wa ngumi na mateke Kick Boxing amesema amefikia maamuzi ya kurejea katika Boxing baada ya kuona bondia Francis Cheka hana mpinzani wa kupigana naye.

Francis Cheka ni Bingwa wa Dunia anayetambuliwa na International Circut Boxing (ICB, alitwaa ubingwa huo baada ya kumshinda Bondia mkongwe nchini Tanzania Rashi Matumla Snake Boy.

Tuesday, July 21, 2009

STARS KUCHEZA NA VIGOGO WA AFRIKA

TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inatarajia kujipima nguvu na moja kati ya timu zilizofanikiwa kutinga katika hatua ya pili ya kuwania kufuvu kucheza Kombe la Dunia 2010 na Kombe la Mataifa Afrika.

Mchezo huo ambao Stars itakuwa ugenini umepangwa kufanyika katika tarehe inayotambuliwa na FIFA ambayo ni Agosti 12.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbrazil Marcio Maximo alisema wameomba kucheza na moja kati ya timu hizo ambazo ni ngumu ili kujipima uwezo wao.

Alisema mchezo huo utakuwa ni kipimo kizuri kwao katika kujenga kikosi hicho ndio maana wameomba kucheza na timu yenye uwezo mkubwa Afrika.

"Tumeomba kucheza kati ya timu hizo zilizofuvu hatua ya pili na mategemeo yetu tutapata timu mojawapo kwani tumeomba zaidi ya timu tano ambazo zipo juu kiuwezo katika hizo zilizofuvu," alisema Maximo.

Alisema mategemeo makubwa kupata timu bora zaidi katika timu hizo 20 ambazo zimefuvu bila kuangalia kama kuna baadhi tayari waliwahi kucheza nazo.

Maximo alisema anatarajia kutangaza kikosi hicho Julai 30 huku kukiwa na wachezaji wa Tanzania wanaocheza soka nje ya nchi pamoja na wachezaji wa ndani.

Alisema kikosi hicho kinatarajia kuanza kambi Agosti 3 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania katika chati ya FIFA.

Nchi za Afrika ambazo zimeingia katika hatua ya pili ya kutafuta tiketi ya kucheza kombe la Dunia na michuano ya Afrika ni Gaboni, Togo, Moroko, Kameruni, Tunisia, Nijeria, Kenya
Msumbiji, Aljeria, Misri, Zambia, Rwanda, Ghana, Mali, Benin, Sudan, Kodivaa, Burkina Faso, Guinea na Malawi.

Katika chati ya viwango vay FIFA, Tanzania kwa sasa ipo katika nafasi ya 97 baada ya kuifunga mabingwa wa Oceanic, New Zealand mabao 2-1 katika mchezo uliocheza mapema Juni.
Na Erasto Stanslaus

FIFA yakubali kuisaidia Tanzania katika kuendeleza soka


Raisi wa shirikisho la kandanad akifafanua jambo kwa Ashford Mamelody na waandishi wa habari.

Shirikisho la kandanda TAnzania TFF hapo jana limetiliana saini na shirikisho la kandanda Duniani FIFA ikiwa ni mpango wa kuisaidia Tanzania katika nyanja 11 za maendeleo ya Soka.

Akizungumza na waandishi wa habari Raisi wa TFF Leodga Chilla Tenga amesema wameafikiana kuisaidia Tanzania katika kuendeleza soka la vijana, soka la wanawake, waamuzi, na soka la ufukweni.

Tenga amesema pia wamekubali kutusaidia kuimarisha mipango ya kibiashara baina ya TFF na wadau wake pamoja na kitengo cha masoko.

Amesema kuanzia tarehe 17 hadi 19 walikuwa na mkutano na afisa maendeleo wa shirikisho la soka Duniani ukanda wa kusini mwa Afrika Ashford Batlang Mamelodi.
Picha na Rajabu Mhamila

SIKU YANGA WALIPOFULIA KWA AFRICAN LYON FC

Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia moja ya mabao yao ya kusawazisha wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya African Lyon juzi Kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam,katika mchezo huo Yanga ilifungwa mabao 3-2.Mchezaji wa Yanga Vicent Barnabas akichuana na Azizi Sibo wa African Lyon wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya African Lyon juzi Kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam,katika mchezo huo Yanga ilifungwa mabao 3-2.
Kiungo wa timu ya Yanga Godfray Bonny akimpiga chenga kipa wa timu ya African Lyon John Mbugwa wakati wa mchezo wa kirafiki Kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam juzi,katika mchezo huo Yanga ilifungwa mabao 3-2.

MISS ILALA YAIVA

WAREMBO KATIKA POZI
Baadhi ya warembo wanaotarajia kuwania kitongoji cha Miss Ilala wakiwa katika pozi wakati wa utamburisho wa warembo hawo mbere ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara Habari Mahelezo Dar es salaam jana.(Picha na Rajabu Mhamila)

Monday, July 20, 2009

TWANGA PEPETA KURUDISHWA LEADERS KATIKA BONANZA

Bendi ya muziki nchini Tanzania Twanga Pepeta International jumapili inatarajia kurudi katika viwanja vya Leaders club kwa mara ya kwanza baada ya kusimamishwa kwa muda usiyojulikana.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Iddi Azan kuhoji Bungeni kwanini viwanja hivyo vilisimamishwa ghafla kutumika katika michezo na burudani.

Waziri wa nchi utumishi wa umma Hawa Ghasia amejibu kwamba viwanja hivyo vitaendelea na Bonanza hadi hapo watakapoamua kufanyia ukarabati.

Aidha mmiliki ya Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka pamoja na Mkurugenzi wa bendi ya Msondo Ngoma Muhidin Gurumo ambao wamekuwa wakitoa burudani katika viwanja hivyo vya Leaders wamemshukuru Mh Hawa Ghasia kwa kuwaruhusu kuendelea.

Na Rajabu Mhamila (Super D)

MISS KINONDONI KATIKA MDAHALO/WAHARIRI

Warembo wanaowania taji la kanda ya Kinondoni (Reds Miss Kinodnoni) na wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari siku ya Jumamosi walishiriki katika mdahalo wa unahusu ngono zembe uliyofanyika katika hoteli ya Giraf Ocean View nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mdahalo huo uliongozwa na Denis Busulwa Sebo kila upande ulipata nafasi ya kuchangia mada pamoja na kuuliza maswali na kujibu.
Pamoja na kuzungumzia ngono zembe, lakini mada kuu ilikuwa je nguo fupip zinachangia ngono zembe? wahariri na waandishi waliunga mkono huku warembo wakipinga.
katika mdahalo huo uliyotumia saa moja ulishuhudia wahariri wakiwabwaga kwa hoja lakini walipata upinzani mkubwa kutokana na kujieleza kwao vizuri.

wakati huo huo warembo wawili wataopata ajira katika hoteli ya Giraffe mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo.

HAPO VIPI WANA MSONDO ???


Mnenguaji wa bendi ya MSONDO NGOMA Nacho Mpendu (Mama Nzawisa) akifanya vitu vyake wakati wa onyesho lao lililofanyika katika viwanja vya TCC Chang`ombe siku ya Jumamosi
Picha na Rajabu Mhamila (Super D Mnyamwezi)

BONANZA TCC CHANG`OMBE "HAPO VIPI WANA MSONDO"

Romario

Mwimbaji wa bendi ya msondo music Romani Mng'ande 'Romario' akiwajibika wakati wa onesho la bendi hiyo mwishoni mwa wiki .(Picha na Rajabu Mhamila aka Super D Mnyamwezi)

"ROMARIO" WA MSONDO NGOMA AKIFANYA VITU VYAKE


Msanii wa kundi la Msondo music band Romani Mng'ande 'Romario' akiimba sambamba na mcheza shoo wa bendi hiyo Amina Saidi 'QUEEN EMMY' wakati wa onesho lao lililofanyika mwishoni mwa wiki .(Picha na Rajabu Mhamila)

Sunday, July 19, 2009

MJUE EMANUEL ADEBAYOR "Si goi goi kama unavyodhani"


Alizaliwa tarehe 26 Februari 1984 mjini Lome, Togo
2002-03: ikiwa ni msimu wake wa kwanza kujitokeza akiwa na klabu ya Metz aliisadia klabu hiyo kupanda daraja nchini Ufaransa huku akiwa amefunga jumla magoli 13.
Mwaka 2003: alijiunga na Monaco kwa dau la pauni milioni 2.
2003-04: alimaliza msimu akiwa na amefunga jumla msimu akiwa amefunga jumla ya mgoli nane. na kuisaidia klabu ya Monaco kutinga fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, na Monaco ilifungwa na Porto katika mchezo wa fainali.
2004-05: alimaliza msimu akiwa amefunga magoli tisa.
2005: August – alitajwa kutaka kujiumnga na klabu ya West Ham, siku ya miwhso ya usajili alikamilisha usajili.
mwezi October – alifanikiwa kufunga goli katiak mchezo dhidi ya Congo ambapo timu ya taifa ya Togoilifanikiwa kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia mwka 2006.
AKimaliza michuano hiyo ya kufuzu akiwa ndiyo kinara wa magoli wa Afrika akiwa na jumla ya magoli 11.
2006: January 13 – alijiunga na klabu ya Arsenal kwa dau la Pauni milioni 3.
January – alihusika katika mgogoro na kocha wa timu ya taifa ya Togo kabla ya mchezo wa ufunguzi dhidi ya Misri katika michuano ya mataifa ya Afrika.
Adebayor alitishia kujitoa katika michuano hiyo lakini baadae aliamua kubaki ingawa hawakufanya vizuri.
February 4 – alifunga goli katika mchezo wa kwanaza akijitikeza katika ligi kuu ya Engaland baada ya Arsenal kushinda 2-0 dhidi ya Birmingham.
June – alikabidhiwa mikoba ya ukapteni wa timu ya taifa ya Togo katika fainali za kombe la Dunia zilizofanyika nchini Ujerumani, ambapo walitolewa katika hatua ya makundi.
2007: February 25 – alikuwa ni moja ya wachezaji watatu waliyotolewa nje kwa kadi nyekundu ambapo Arsenal ilifungwa 2-1 na Chelsea katika mchezo wa fainali ya michuano ya Carling Cup mchezo ambao ulichezwa katika dimba la Millennium.
2007-08: Ni msimu ambao aliufurahia zaidi na kula matunda ya soka la kulipwa huku akifunga jumla ya magoli 30 katika michezo 48 aliyojitokeza ikiwa ni pamoja na kichapo kilichotolewa kwa Tottenham na Newcastle.
Alimaliza akishika nafasi ya tatu katika tuzo za mwaka kw wachezaji wa kulipwa ikiwa ni pamoja na katika timu ya mwaka ya wachezaji wa kulipwa.

2008: January 23 – aliwaomba msamaha mashabiki kwa kutoleana lugha chafu na mchezaji mwenzake Nicklas Bendtner katika mchezo ambao walifungwa magoli 5-1 katika mchezo wa pili wa michuano ya Carling Cup ikiwa ni hatua ya nusu fainali ambapo walichapwa na Tottenham.
August 1 – ilithibitishwa amekubali kusaini mkataba mpya na klabu ya Arsenal licha ya kuripotiwa kuwaniwa na klabu ya AC Milan na Barcelona.
2009: February 10 – alituzwa kuwa mwanasoka bora wa Afrika wa mwaka 2008 kwa mara ya pili katika sherehe zilizofanyika Lagos, Nigeria.
July 18 – alifanikiwa kufaulu vipimo vya affya na kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Manchester City.

Mjini Magharibi watwaa ubingwa wa michuano ya Copa Coca Cola U -17

TIMU ya Mijini Magharibi jana iliibuka bingwa wa mpya wa michuano ya Vijana chini ya miaka 17 'Copa Coca Cola' baada ya kuichapa Tabora bao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchezo huo uliochezwa katika dakika 120 baada ya dakika 90 kwisha kwa sare ya mabao 1-1, hivyo mwamuzi wa mchezo huo kuongeza dakika 30 za nyongeza.

Kutokana na matokeo hayo Mjini Magahribi wamejinyakulia kitita sh. milioni 4.5 wakati nafasi ya pili imekwenda kwa Taborea wataoboka na sh. milioni tatu wakati timu ya Morogoro itapata sh milioni mbili baada ya kushika nafasi ta tatu baada ya kuinyuka Kigoma kwa bao 1-0.

Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani katika dakika zote za mchezo lakini Majini Magharibi ndio walionekana kutawala mpira kwa muda mrefu.

Pamoja Mjini Magharibi kutawala mchezo huo lakini iliwabidi kusubili hadi kipindi cha pili kupata bao hilo dakika ya 67 mfungajji akiwa Ibrahimu Rajabu kwa shuti kali la mbali lililomshinda kipa wa Tabora.

Baada ya Tabora kufungwa bao hilo waliongeza kasi ya mchezo na kufanikiwa kupata bao kusawazisha dakika ya 90 mfungaji akiwa Lameck Simon na kufanya mchezo huo kuongezwa dakika za nyongeza.

Mjini Magharibi walipata bao la pili dakika ya 93 mfungaji akiwa Mohamed Abdulrahim baada ya kupasua ngome ya Tabora na kuachia shuti kali.

Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mrisho Kikwete na alikabidha kombe kwa mshindo wa michuano hiyo.

Saturday, July 18, 2009

YANGA WAJIFUA!!!

Wachezaji wa klabu Yanga wakijifua katika uwanja wa Uhuru tayari kwa michuano ya ijayo ya ligi kuu Tanzania bara msimu ujao, wakiwa na kocha wao Mserbia Prof. Dusan Condic

ETHIOPIA YATOLEWA JELA NA FIFA BAADA YA UCHAGUZI

Shirikisho la kandanda la nchini Ethiopia EFF limeridhiwa na shirikisho la kandanda Duniani FIFA baada ya kufanya uchaguzi uliyofanyika mapema leo na kuweka uongozi mpya.
Ujumbe wa watu wa tatu toka FIFA umesema umeridhishwa na matokeo ya uchaguzi huo.
Mgogoro uliyokuwepo ndani ya EFF ulipelekea Ethiopia kuondolewa katika michuano ya kusaka nafasi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia nchini Afrika Kusini na mataifa ya Afrika nchini Angola mwaka 2010 mwezi Julai mwaka jana.
Sahlu Gebrewold Gebremariam amechaguliwa kuwa raisi wa EFF, akichukua nafasi ya Dr Ashebir Woldegiorgis, ambaye alijiuzulu mwezi May.
Sahlu alikuwa mgombea pekee katika nafasi ya uraisi katika uchaguzi uliyofanyika leo, baada ya wagombea wengine kujitoa siku ya Ijumaa.
Amesema dhamira yake kubwa ni kuhakikisha anafufua soka la Ethiopia.

MNAOMPONDA "OWEN" MPOOO ???

Mchezaji Michael Owen amefanikiwa kufunga goli katika mchezo wake wa kwanza akiwa na Manchester United huku akifunga goli la ushindi katika mchezo dhidi ya kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Malaysia na kuichapa 3-2 katika mchezo uliyochezwa Kuala Lumpur.
Wayne Rooney na Nani ndiyo walikuwa wa kwanza kupta magoli ya ushindi kwa mabingwa hao wa England, huku mchezaji Amri Yahyah akifunga magoli mawili ya Malaysia kabla ya Owen kuingia akitokea benchi na kufunga goli la ushindi.
Hata hivyo baada ya kutokea matukio ya ugaidi huko Jakarta kumeilazimisha klabu ya Manchester United kuahirisha safari ya kwenda Indonesia na kujikuta ikiathiri ziara yao ya nchi za mashariki ya mbali.
Ingawa Rooney alitolewa nje kutibiwa baada ya kuumizwa na mlinzi wa klabu ya Malaysia.
Rooney aliweza kurejea uwanjani na kufanikiwa kuipangua ngome ya ulinzi ya Malaysian na pasi iliyopigwa na Dimitar Berbatov ambayo iliwaparaza mabeki na kumkuta Rooney aliuweka mpira wavuni.
Dakika 20 baadae mshambuliaji wa kimataiaf wa Ureno Nani alifunga goli la pili na matokeo kuwa 2-0 kabla ya Malysia kusawazisha.

Friday, July 17, 2009

Morogoro washika nafasi ya tatu Copa coca cola U17

Mshambuliaji wa timu ya Mkoa wa Kigoma, Katunka Amani (kulia) na Isihaka Athumani wa Morogoro wakiwania mpira wakati wa mechi ya kusaka mshindi wa tatu wa michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Morogoro ilishinda bao 1-0.

TIMU ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya ya Mkoa wa Morogoro imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya vijana yanayoelekea ukingoni baada ya kuichapa Kigoma mabao 1-0.

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru na kushuhudiwa na umati wa mashabiki wa mpira wa miguu, walishuhudia Kigoma wakikosa mabao mengi dakika za mwanzo.

Morogoro ambao walitolewa na Tabora katika mechi ya nusu fainali, walijiaptia bao pekee dakika ya 20, lililofungwa na Hamis Salehe kwa mpira wa kona uliokwenda moja kwa moja wavuni.

Baada ya kufungwa bao hilo, Kigoma walijaribu kufanya mashambulizi langoni mwa Morogoro, lakini washambuliaji wake, Baruan Akilimali na Matata Seif walishindwa kukwamisha mpira wavuni dakika za 70 na 78.

Kutokana na ushindi huo, Morogoro walizawadiwa fedha sh. milioni mbili kutoka kwa waandaji wa mashindano hayo ya vijana.

Jumamosi, timu ya Mjini Mgharibi ambao walionesha soka safi katika mechi zao za nyuma, wataumana na Tabora katika mchezo wa fainali utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

TAASISI YA KUINUA VIPAJI YA "MAMBO" YAFANYA MAMBO KWA VIJANA


Baadhi ya wanamichezo waliyojitokeza katika taasisi ya kuinua vipaji vya mpira wa kikapu ya MAMBO wakiwa na vyeti vyao baada ya kushiriki mazoezi katika miezi miwili

NA RAJABU MHAMILA

KOVA CUP KUANZA JUMAMOSI


Mwanamichezo Ibrahimu Raza kushoto akikabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi laki mbili na nusu kwa mkuu wa upelelezi wmkoa wa Ilala, Duwani Nyanda kw ajili ya kushiriki mashindano ya kombe la kamanda Kova yanayotarajiwa kuanza Jumamosi hii jijini Dar es Salaam. katikati ni katibu wa ytimu ya mpira wa miguu ya Polisi kati Paul Mwanikungu.

NA RAJABU MHAMILA

EXTRA YAJIPANGA UPYA KUTEKA JIJI



Waimbaji wa Bendi ya Extra Bongo wakiimba wakati wa mazoezi yao Mwananyamala jijini Dar es Salaam hivi karibuni kutoka kushoto, Grenson Sesekwa, Hadija Mnoga (kimobitel) na Raisi wa Bendi hiyo Ally Choki.

NA RAJABU MHAMILA

JAHAZI YATAMBULISHA WAIMBAJI WAPYA


Wanamuziki wa kundi la Jahazi Morden Taarab wakiimba wakati wa utambulisho wa waimbaji hao wapya katika kundi la Jahazi.

TCC WASHIRIKI MICHEZO KATIKA SIKU YA FAMILIA


Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Sigara Tanzania TCC wakishiriki katika mchezo wa wavu wakati wa siku ya Familia iliyofanyika viwanja vya TCC Club.

NA RAJABU MHAMILA

TCC WASHIRIKI MICHEZO KATIKA SIKU YA FAMILIA


Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Sigara Tanzania wakishiriki katika mchezo wa kuvuta kamba mwishoni mwa wiki katika siku ya faimailia iliyoandaliwa na kampuni hiyo.

COPA COCA COLA KUFIKIA TAMATI JUMAMOSI TAREHE 18, 2009


Kampuni ya vinywaji ya Coca Cola imetangaza zawadi za washindi wa mashindano ya vijana chini ya umri ya miaka 17, Copa coca Cola yanayofikia tamati July 18 mwaka huu katika dimba la Uhuru.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Meneja wa kampuni hiyo Heriet Mutayoba amesema mashindano hayo kwa ujumla yalikuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na kupokelewa vizuri na wapenzi wa soka.

Ametaja zawadi hizo kuwa mshindi wa kwanza ataibuka na milioni nne na nusu, mshindi wa pili milion tatu huku mshindi wa tatu milion mbili pia wote watapata kikombe, medali na vyeti.

Vilevile kutakuwa na zawadi ya mchezaji bora, mfungaji bora kipa bora ambao wataibuka na kitita cha shilingi laki tano za kitanzania na timu yenye nidhamu itapata milioni moja na kikombe kwa wote.

WAJUE WASHIRIKI WA MISS ILALA 2009

WASHIRIKI REDDS MISS ILALA 2009
CONTESTANT NO 1
JINA : FATMA ATHUMAN BONGI
UMRI : 18 YRS
ELIMU : KIDATO CHA NNE
KAZI : BIASHARA
MATARAJIO : KUWA MUELIMISHA LIKA MUIGIZAJI
KIPAJI : KUIMBA
CONTESTANT NO 2
JINA : EVELYNE LUJA GAMBA
UMRI : 22YRS
ELIMU : CHUO KIKUU
KAZI : MWANAFUNZI
MATARAJIO : KUWA COMPUTER SYSTEM ANALYST
KIPAJI : KUCHEZA BADMINTON
CONTESTANT NO 3
JINA : JULIETH WILLIAM LUGEMBE
UMRI : 19YRS
ELIMU : CHUO KIKUU
KAZI : MWANAFUNZI
MATARAJIO : MBUNIFU WA KIMATAIFA WA MAVAZI
KIPAJI : MUCHEZA MUZIKI
CONTESTANT NO 4
JINA : MAGRETH PETER MOTAU
UMRI : 21YRS
ELIMU : KIDATO CHA NNE
KAZI : MSHAURI
MATARAJIO : KUWA MAMA USHAURI KWA VIJANA
KIPAJI : KUIMBA NA KUCHEZA
CONTESTANT NO 5
JINA : LILIAN NYAMIZI MIHAYO
UMRI : 20YRS
ELIMU : KIDATO CHA NNE
KAZI : OFISA MASOKO
MATARAJIO : KUWA MWANA HABARI
KIPAJI : KUIMBA
CONTESTANT NO 6
JINA : IRENE MUGONZIBWA KARUGABA
UMRI : 20YRS
ELIMU : KIDATO CHA SITA
KAZI : AFISA MASOKO
MATARAJIO : KUJIUNGA NA CHUO KIKUU SEPTEMBA
KIPAJI : KUBUNI MITINDO
CONTESTANT NO 7
JINA : NEEMA DOREEN SYLVERY KASUNGA
UMRI : 18YRS
ELIMU : KIDATO CHA NNE
KAZI : MA
MATARAJIO : KUWA MWANASHERIA MASHUHURI
KIPAJI : KUIGIZA NYIMBO
CONTESTANT NO 8
JINA : WINNIFRIDA FARES MMARI
UMRI : 19YRS
ELIMU : KIDATO CHA NNE
KAZI : MWANAMITINDO
MATARAJIO : KUWA MWANAMITINDO WA KIMATAIFA
KIPAJI : KUCHEZA MUZIKI
CONTESTANT NO 9
JINA : HUSNA OMAR AHMED
UMRI : 21YRS
ELIMU : KIDATO CHA SITA
KAZI : RESTAURANT SUPERVISOR
MATARAJIO : KUWA MWANASHERIA
KIPAJI : KUCHEZA MUZIKI
CONTESTANT NO 10
JINA : DORIS JIMMY LOUS
UMRI : 19YRS
ELIMU : KIDATO CHA SITA
KAZI : BIASHARA
MATARAJIO : KUJIUNGA NA CHUO KIKUU
KIPAJI : KUIGIZA
CONTESTANT NO 11
JINA : GLORY WILLIAM MWANDWANI
UMRI : 21YRS
ELIMU : KIDATO CHA SITA
KAZI : MWANAFUNZI IT BRITISH COUNCIL
MATARAJIO : KUMILIKI KAMPUNI
KIPAJI : KUCHEZA MUZIKI
CONTESTANT NO 12
JINA : PENDO ANANDUMI LEMA
UMRI : 22 YRS
ELIMU : KIDATO CHA NNE
KAZI : MWANAFUNZI UDSM COMPUTING CENTRE
MATARAJIO : KUWA MWANASIASA
KIPAJI KUIMBA
CONTESTANT NO 13
JINA : ANNE MOSES MKANDAWILE
UMRI : 18YRS
ELIMU : KIDATO CHA SITA
KAZI : MODEL
MATARAJIO : SUPER MODEL
KIPAJI : KUCHEZA FOOTBALL
CONTESTANT NO 14
JINA : KHADIJA KENETH MUHECHA
UMRI : 22YRS
ELIMU : DIPLOMA
KAZI : MWANAFUNZI
MATARAJIO : KUWA HUMAN RESORCE MANAGER
KIPAJI : KUCHEZA MUZIKI
CONTESTANT NO15
JINA : SYLIVIA FRANK SHALLY
UMRI : 19 YRS
ELIMU : KIDATO CHA SITA
KAZI : PLANNING MANAGER
MATARAJIO : MFANYABIASHARA
KIPAJI : UIMBAJI
CONTESTANT NO 16
JINA : GLADNNESS JOHN SHAO
UMRI : 19YRS
ELIMU : CHUO KIKUU
KAZI : MWANAFUNZI
MATARAJIO : KUWA MWANDISHI WA HABARI
KIPAJI : KUCHEZA BASKETBALL
CONTESTANT NO 17
JINA : ZENA RASHID MBASHA
UMRI : 22YRS
ELIMU : KIDATO CHA NNE
KAZI : KATIBU MUHTASI
MATARAJIO : KUJIENDELEZA NA KUWA DAKTARI
KIPAJI : KUCHEZA MUZIKI

NA RAJABU MHAMILA - SUPER D

Thursday, July 16, 2009

Wanawake wa Afrika wadhihirisha umwamba Uholanzi

Timu ya taifa ya wanawake ya Afrika Kusini Banyana Banyana!!!

Timu ya taifa ya wanawake ya Afrika Kusini imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Switzerland katika mchezo wa fainali uliyoshirikisha mataifa manne nchini Uholanzi.
Mchezaji soka bora wa kike wa Mwaka wa Afrika Noko Matlou, Mamphashe Popela na Janine Van Wyk walifunga magoli na kuipa ushindi Afrika Kusini.
Meneja wa kikosi hicho Fran Hilton-Smith amesema anajisikia fahari sana vijana kuibuka na ushindi.
Naye kocha Augustine Makalane amesema ni kikosi ambacho bado anakijenga lakini wamefanya vizuri kutokana na kile ambacho wamejifunza mara ya mwisho walipokuwa Cyprus.
Banyana Banyana walianza michuano hiyo vibaya, kwa kuchapwa 5-0 na China katika mchezo wa ufunguzi.
kapteni wa kikosi hicho Kylie Anne Lowe amesema kwamba pipingo walichokipata dhidi ya China kiliongeza chachu ya kufanya vizuri kwa kikosi hicho ambacho kilikuwa hakina uzoefu wa michuano ya kimataifa.
Katika mchezo wa pili iliibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Uholanzi, huku magoli yakifungwa na Lebogang Thobejane na Popela.
Wa Afrika Kusini waliyopo Uholanzi waliunganisha pamoja na kuishangilia Banyana Banyana, na kudai hizo ni salamu za michuano ya Dunia 2010.

BONDIA ASHRAFU AYATAKA MATAJI YA AWADHI TAMIMU UZITO WA JUU

Bondia Awadhi Tamimu kushoto akipambana na bondia wa Nchini Urusi aliyemtaja kwa jina la Bokt kulia.

Bingwa wa ngumi za kulipwa ashrafu Suleimani imetamba kumdunda mpinzani wake Awadh Tamim katika pambano la kuwania ubigwa wa Afrika wa mchezo huo mchezo utakaofanyika July 18 katika ukimbi wa DDC Mlimani jijini Dar es Salaam.

Akichonga na kipindi michezo ya Radio Times FM Ashrafu amesema amejiandaa vizuri katika pambano hilo ambalo litaonyesha historia yake katika mchezo huo.

Ashrafu amesema kwamba ana hofu na mchezaji huyo na uhakika wa kupiga upo kutokana na maandalizi makali anayoyafanya.

Ashrafu amefikia uamuzi wa kuzichapa na Awadhi Tamimu baada ya Bodnia huyo kamua kuacha wazi mikanda yake ya Ubingwa wa Tanzania na Afrika Mashariki kufuatia kukosa mpinzani hapa nchini.

Awadhi Tamimu amesema kwa muda mrefu amekuwa na kiu ya kuwa bingwa wa Afrika na kusaka mataji makubwa ya Dunia katika uzito wa juu, lakini amekuwa akikosa mpinzani hapa nchini, hivyo amefikia maamuzi ya kuacha wazi mikanda hiyo ili awanie ubingwa wa Afrika.

Promota wa pambano hilo Shomari Kimbau amesema Bingwa wa Pambano hilo kati ya Awadhi Tamimu na Ashrafu Suleiman ndiyo atawania ubingwa wa Afrika.

Wednesday, July 15, 2009

SIMBA SASA YAPUMUA !


Kocha Phiri mwenye suti na tai katikati ya mashabiki wa SIMBA!

KOCHA Mkuu wa klabu ya Simba, Mzambia Patrick Phiri amewasili nchini siku ya Jumatano jioni na kupewa mapokezi makubwa na wanachama huku akisindikizwa na vikundi vya ngoma vya klabu hiyo maarufu Mpira Pesa.

Kocha huyo baada ya kuwasili, alipanda basi dogo la klabu hiyo, huku akiambatana na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Field Masho Hassan Dalali na Meneja wa timu, Innocent Njovu bila ya mchezaji yoyote kama ilivyodaiwa awali na uongozi wa klabu hiyo.

Hiyo imekuwa ni faraja kubwa kwa Simba ambao walijawa na hofu ya kocha huyo kuingia mitini kama ilivyowahi kutokea siku za nyuma wakati timu hiyo ilipokuwa ikikabiliwa na michuano.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini kwa ndege ya Shirikika la Ndege la Zambia majira ya saa 10 jioni, Phiri alisema, ameyapokea mapokezi hayo kwa mshtuko mkubwa kwani hakutegemea kupokewa hivyo.

Amesema kuchelewa kwake kufika nchini si kwamba alifanya makusudi, bali ni matatizo yaliyokuwa yakimkabili kwao na ilikuwa ukizingatia ilimharibia mipango yake.

Tabora uso kwa uso na Mji Magharibi fainali ya Copa Coca Cola


TIMU ya Mkoa wa Tabora imekata tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 baada ya kuifunga Morogoro bao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Tabora walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia kwa mshambuliaji wake, Said Khalfani aliyefunga kwa shuti kali baada ya kupokea pasi kutoka Lameck Simoni.

Moro walisawazisha bao hilo dakika 47, kupitia kwa Kulwa Salanga kwa shuti kali akiwa ndani ya eneo la hatari na mpira kutinga wavuni.

Bao hilo liliwaongezea nguvu Tabora na kuongeza mashambulizi langoni mwa wapinzani wao, dakika ya 76, Issa Swedy aliifungia timu yake bao la pili kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Hussein Moshi.

Kwa matokeo hayo, Tabora itakutana na Mjini Magharibi katika mchezo wa fainali itakayochezwa Uwanja wa Uhuru, Jumamosi huku Morogoro wakikutana na Kigoma kutafuta mshindi wa tatu.

Manyema FC yawasilisha majina ya usajili

Timu ya soka ya Manyema FC ya jijini Dar es Salaam leo imewasilisha majina ya wachezaji waliowasajili kuchezea ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Akiongea na viwanjani Mkrugenzi Mtendaji wa Manyema FC Ally Mmanga amesema wachezaji wote waliowasajili msimu huu ni wa ndani ya nchi na si nje ya nnchi.

Amesema wamesajili jumla ya wachezaji 28 huku akismea wachezaji 16 ni wa zamani na wachezaji 12 ni wachezaji wapya.

Amewataja baadhi ya wachezaji kuwa ni pamoja na goligipa Odo Nombo Mulemba toka Kagera, Amoa Kefa Zulu, Abrahamu Masunga, Musa Kipao na Steve Mkuchika.

Mmanga amesema swala la Katibu wa kuajiriwa bado wanalifanyia kazi na litakapokuwa tayari wataliweka hadharani.

Kuhusu maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara msimu ujao, amesema tarehe 1 mwezi wa nane wataweka kambi nje ya Dar es Salaam.

Mjini Magharibi watinga fainali Copa Coca Cola


Timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 toka mjini Magharibi Zanzibar imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Copa Coca Cola baada ya kuwafunga vijana wa Kigoma 2-0.

Magoli ya Mji Magharibi yalifungwa na mchezaji Juma Mbwana katika dakika ya 18 ya mchezo wakati goli la pili lilipatakana katika dakika ya 85 kupitia kwa mchezaji Ibrahim Rajabu.

Katika mchezo huo mchezaji wa timu ya vijana wa kigoma Shaaban Abasi alizawadiwa kadi nyekundu.

Timu ya vijana wa Mji Magahribi sasa wanamsubiri mshindi wa mchezo wa pili wa nusu fainalli kati ya Tabora na Morogoro.

Fainali ya michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 itachezwa siku ya Jumamosi ya tarehe 18 mwezi huu.

Tuesday, July 14, 2009

VYAMA VYA MIKOA SASA KUTOA MAONI TFF DHIDI YA ZFA

Raisi wa shirikisho la kandanda Tanzania TFF Leodga Chilla Tenga amevitaka vyama vya soka vya mikoa kutoa maoni dhidi ya ushirikiano wa TFF na ZFA.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na afisa habari wa TFF Florian Kaijage imesema kwamba Tenga amefikia hatua ya kukusanya maoni kwa viongozi wa mikoa ili kutoa fursa ya kupata uwezekano wa kulimaliza tatizo hilo ambalo sasa linaonekana kukua zaidi.

Raisi wa TFF juma lililopita alizungumza na waandishi wa habari kuelezea kwa kina namna ambavyo TFF imekuwa ikitoa ushirikiano wa karibu na ZFA katika maswala mbali ya maendeleo ya soka.

Tenga aliwataka viongozi wa chama cha soka cha Zanzibar kuwa wa kweli na kuacha kuongea mambo ambayo wanafahamu ukweli wake.

Kwa takribani majuma kadhaa sasa ZFA wamekuwa wakilalamika katika vyombo vya habari kwmaba TFF ndiyo kikwazo katika kufanikisha wao kuwa wanachama wa shirikisho la kandanda Duniani FIFA jambo ambalo TFF imekanusha.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Tenga kwenda kwa vyama vya mikoa imesema TFF itakuwa na kikao na chama cha soka visiwani Zanzibar ZFA tarehe 21 Julai 2009 na moja ya ajenda itakayojadiliwa ni pamoja ushirikishwaji ZFA/Zanzibar katika masuala ya FIFA.

Monday, July 13, 2009

UJIO WA PHIRI SIMBA BADO KITENDAWILI

Kitendawili cha kocha mkuu wa Simba Ptrick Phiri lini atarejea Tanzania baada ya kukwama Zambia alipokwenda katika mapumziko bado kigumu.

Akizungumza na Viwanjani.blogspot meneja wa timu ya Simba Innocent Njovu amesema kocha Phiri anaweza kuwasili mwishoni wiki hii.

Kauli hii inapingana na ile iliyotolewa jana na uongozi wa klabu ya Simba kwamba kocha huyo anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania siku ya Jumanne.

"Kocha Phiri tunamtegemea kuwasili Tanzania tayari kwa maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara mwishoni mwa juma hili" amesema Njovu

Njovu amesema kufuatia kuchelewa kwa Phiri kumepelekea timu kusita kuingia kambini sasa kwa juma la pili tangu iarifiwe itaanza kambi hapo Julai mosi.

"timu haiwezi kuingia kambini hadi kocha mkuu atakapowasili nchini" amesema Njovu na kudai "kwa sasa timu inafanya mazoezi ya kawaida ikiwa chini ya kocha msaidizi"

Patrick Phiri kocha mkuu wa klabu ya Simba alikwa nchini Zambia baada ya kufiwa na kaka yake, lakini baadae gazeti moja la Zambia likaandika kocha huyo wa wekundu wa Msimbazi ameshindwa kesi ya madai ya umiliki wa nyumba yake jambo lilidaiwa kumchelewesha.

BALLACK "HUU NI MSIMU WA CHELSEA MAN U WAMEFULIA"


Mchezaji wa klabu ya Chelsea Michael Ballack anaamini kwmaba mabingwa wa England Manchester United, watadhoofika msimu ujao baada ya kuondoka kwa mchawi wao wa magoli na kutabiri kwmaba utakuwa ni msimu wa Chelsea.
Ujio wa kocha mpya Carlo Ancelotti katika dimba la Stamford Bridge kumefufua tumaini jipya la kwa mashabiki wa Chelsea na huenda ukawa msimu wa mafanikio ya ubingwa tangu mara ya mwisho wa twao mwaka 2006.
Kiungo mchezeshaji huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani anaamini watafanya vizuri zaidi ya Manchester United ambayo imempoteza Cristiano Ronaldo na Carlos Tevez katika dirisha la usajili.
Amesema lengo lao kila msimu huwa ni kutwaa ubingwa na wanaamini watatwa ubingwa msimu huu.
Amekiri kuwa msimu uliyopita walianza vema lakini Man United walicheza katika kiwango cha juu zaidi yao.
Na kukiri kwamba mashetani hao wekundu wa Old Traford wamekuwa kikwazo kikubwa kutwaa ubingwa msimu wa 2007 na 2008.

FURGOSN ASEMA HATAKI TENA KUSAJILI

Klabu ya Manchester United imeweka wazi kwamba haitanunu tena mchezaji katika kipindi hiki cha usajili.

Rai hiyo imetolewa na kocha wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson akisema wamefikia kikomo cha biashara hivyo watu wanapaswa kusahau nani na nani walikuwa wakiwafuatilia na kuweka bayana kwamba mchezaji Michael Owen atakuwa akivaa jezi nambari saba.

Amesema wakati soko linapokuwa limepamba moto, wao huwa hawako tayari kufanya makkubaliano.

Wadau wengi wa soka walitaraji kuona dau la Pauni milioni 80 toka katika mauzo ya Cristiano Ronaldo ambaye ametua Real Madrid lakini imeonekana kwamba zimetumika robo tatu tu baada ya Owen, Antonio Valencia, Gabriel Obertan wakitumia jumla ya dau la pauni milioni 20.
Mzee Furgason amesema Valencia na Obertan wote ni wachezaji wenye umri mdogo, lakini ni wanauwezo mkubwa wa kusakata kandanda.

Ameongeza kuwa wako na mzee mmoja akimaanisha Owen. lakini amedai anauzoefu wa kutosha na anaamini atafunga magoli.

SAFARI YA BONDIA AWADHI TAMIMU KUWANIA UBINGWA WA AFRIKA YAINGIA MDUDU

Maandalizi ya pambano la ngumi za kulipwa la kuwania ubigwa Afrika kwa Awadh Tamim dhidi ya bondia Ashrafu Suleiman pambano litakalopigwa katika ukumbi wa DDC mlimani jijini Dar es Salaam yamekamilika.

Akiongea na kipindi cha michezoi cha Radio Times FM mwandaaji wa pambano hilo Shomari Kimbau amesema kwamba pambano hilo linatakuwa upinzania wa hali ya juu kutokana na maandalizi kabambe yanayofanywa na mabondia hao.

Amesema sababu kubwa ya pambano hilo ni baada ya Awadhi Tamimu kutangaza kuacha wazi mikanda yake ya Ubingwa wa Tanzania na Afrika Mashariki na kuweka nia ya kuwania ubingwa wa Afrika lakini bondia Ashrafu Suleimani akataka wapambane ili kumuonesha kwamba kunamabondia wanauwezo.

Awadhi Tamimu alifikia maamuzi hayo ya kuachia mikanda hiyo wazi baada ya kukosa mpinzani, hivyo Ashrafu amesema anataka kumuonyesha kwamba anaweza.

Kimbau amesema Bingwa atakayepatikana katika pambano hilo ndiyo atakayecheza pambano la kuwania ubingwa wa Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa Tanzania katika uzito wa juu.

NEWCASTLE INAKUFA KISAMAKI

Golikipa wa klabu ya Newcastle Steve harper amedai klabu hiyo inakufa taratibu, kifo cha maumivu huku mmiliki Mike Ashley akijaribu kuiuza klabu hiyo bila mafanikio.

Wanunuzi kadhaa wamekuwa wakitangaza nia yao ya kutaka kuinunua kabla ya kushuka daraja na baada ya kushuka daraja lakini wamekuwa hawafikii makubaliano na hatimaye kupotea kusiko julikana.

hatua hiyo imemuacha Alan Shearer njia panda asijue lini atasaini mkataba wa kuinoa timu hiyo, huku wachezaji nao wakiwa katika giza totoro lisilo hata lepe la mwanga la kuwaonyesha njia.

Harper akizungumza kwa uchungu amesema inauma sana inapofika wakati mtu unakuwa hujui nini cha kufanya, huku wachezaji nao wakijua bosi wao maji yamemfika shingoni, licha ya kuwa na ndoto za Alinacha kwamba siku moja watajenga nyumba angani na kuwa matawi ya juu.

Amesema kila moja, mashabiki, wachezaji, uongozi wanataka kuijenga upya klabu hiyo lakini hali ndiyo inazidi kuwa ngumu kila kukicha.

WAOGELEAJI 6 KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA ITALIA

Chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania kinatarajia kuondoka Julai 18 kwenda nchini Italia kwa ajili ya mashindano ya Dunia ya mchezo huo yatakayoanza Julai 21 mwaka huu.

Akizungumza na kipindi cha michezo na burudani Rais wa chama hicho Deogratius Vicent ametanabaisha kuwa safari hiyo itajumuisha watu sita yaani wachezaji wanne na viongozi wawili.

Vicent ameongeza kuwa lengo lao ni kwenda na wachezaji 12 lakini kutokana na matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wao basi hawana budi kwenda na idadi hiyo pungufu.

Hata hivyo amewaombna wadau wote wanaoupenda mchezo huo kujitokeza kwa wingi katika kuwapiga tafu ili waende kuiwakilisha vema Tanzania.

Sunday, July 12, 2009

TFF yataka rangi za timu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limezitaka klabu zote zitakazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao kuweka wazi viwanja watakavyotumia na kuwasilisha rangi za jezi watakazotumia kwa michezo ya nyumbani na ugenini.

Msimu uliopita kulikuwa na mabadiliko kwa baadhi ya viwanja ambapo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kulikuwa na timu za Yanga, Simba, Moro United, JKT Ruvu ya Pwani na Azam FC zote ziliutumia uwanja huo.

Akizungumza Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Fredrick Mwakalebela alisema, walizitumia klabu zote za ligi kuu, taarifa ya kuzitaka ziweke wazi viwanja watakavyotumia kwa ajili ya msimu ujao, pamoja na kuwasilisha rangi za jezi watakazozitumia.

''Unajua muda uliobaki ni mchache kabla ya ligi kuanza, hivyo jana (juzi) tuliziandikia klabu mambo mbalimbali yakufanya kabla ya ligi kuanza, lazima watuambie mapema watatumia jezi za rangi gani watakapokuwa ugenini na nyumbani pamoja na viwanja watavyotumia,'' alisema Mwakabela.

Alisema ni lazima vitu hivyo vipelekwe mapema, ili na wao wapate muda wa kupanga ratiba ya ligi hiyo, kwani klabu zikishindwa kutoa taarifa mapema, watashindwa kupanga ratiba kwa kuwa hawatajua ni viwanja vingapi vitatumika kwa ligi hiyo.

Mwakalebela alisema mbali na hayo, pia wamezitaka klabu hizo kuwasilisha logo (nembo) za wadhamini wao, ili wajue ni jinsi gani watakavyowaelekeza mahali zitakapokaa kwenye jezi ukizingatia kuwa, ni lazima nembo ya mdhamini mkuu ambayo ni Kampuni Vodacom iwe mbele.

Akizungumzia suala la kiungo wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' na Simba, Henry Joseph kama Shirikisho la Mpira wa Miguu la Norway limemwombea uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya kuichezea Kongsvister ya nchini humo, alisema mpaka sasa hawajapokea barua yoyote kutoka huko.

TFF wazidi kula shavu

NEEMA imezidi kuiangukia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kuingia mkataba wa miaka minane na kampuni ya +One ya Marekani ambayo itakuwa ainatoa vifaa vya michezo kwa timu za Taifa za Tanzania.

Mkataba huo utakaogharimu dola za Kimarekani 4,500,000, utazihusu timu za Taifa ya wakubwa Taifa Stars, timu ya wanawake ya Twiga Stars, na timu za vijana chini ya miaka 23, 20 na 17.

TFF tayari ilikuwa na mkataba na kampuni ya Bia ya Serengeti pamoja na Benki ya NMB ambazo zote kwa pamoja walikuwa wanazisaidia timu hizo kila mmoja eneo lake.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela alisema mkataba huo umeanza kutekelezwa kuanzia Juni 20 na utafika kikomo baada ya miaka minane.

Alisema mkataba huo utakuwa katika maeneo manne tofauti ambayo ni kutoa vifaa vya michezo kwa timu ya Taifa na maendeleo ya michezo kwa vijana, msaada wa pesa taslimu kwa timu hizo zinapofanya vizuri pamoja na kudhamini mashindano yatakayoshirikisha Tanzania na nchi jirani.

Alisema kupitia mkataba huo TFF itanufaika kupata vifaa bora vya michezo kwa kipindi hicho huku ikitoa nafasi kwa klabu na vyama vya mikoa kununua vifaa hivyo kwa bei ya chini.

"Baada ya mchakato wa miaka mitatu hatimaye tumesaini mkataba huo na kampuni hiyo kampuni hiyo ambayo utakuwa na faida kubwa katika maendeleo ya soka nchini katika nyanja mbalimbali," alisema Mwakalebela.

Alisema kwa mujibu wa mkataba huo, +One itatoa jezi za mashindano seti 900, mazoezi seti 900, soksi za mashindano seti 1200, za mazoezi seti 1200, suti za michezo za mashindano seti 900, suti za mazoezi wakati wa mvua za mashindano seti 400, za mazoezi seti 400 pamoja na vifaa vingine vya michezo.

Alisema idadi hiyo ya vifaa itakuwa inatolewa kila mwaka ambapo gharama ya vifaa hivyo kwa mwaka ni dola za Kimarekani 450,000 wakati kwa kipindi chote cha mkataba ni dola 3,600,000.

Alisema mbali na vifaa hivyo pia timu hizo zitakuwa na mgao wa pesa taslimu zitakapofanya vizuri katika mshindano mbali ambayo timu hizo zitashiriki hasa katika mashindano ya ngazi za Afrika na Dunia.

"Timu hizo zote zitakuwa na mgao tofauti kutoka kwa kampuni hiyo pale timu hizo zinzpofanya vizuri katika michuano hiyo ili kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo kuongeza juhudi katika mashindano hayo," alisema Mwakalebela.

Alisema kupitia mkataba huo Tanzania itaandaa mashindano ambayo yatakayoshirikisha timu nne ikiwemo Taifa Stars na nchi nyingine za jirani ambapo michuano hiyo itafanyika kila mwaka na kwa kuanzia wataanza mwaka huu.