NEEMA imezidi kuiangukia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kuingia mkataba wa miaka minane na kampuni ya +One ya Marekani ambayo itakuwa ainatoa vifaa vya michezo kwa timu za Taifa za Tanzania.
Mkataba huo utakaogharimu dola za Kimarekani 4,500,000, utazihusu timu za Taifa ya wakubwa Taifa Stars, timu ya wanawake ya Twiga Stars, na timu za vijana chini ya miaka 23, 20 na 17.
TFF tayari ilikuwa na mkataba na kampuni ya Bia ya Serengeti pamoja na Benki ya NMB ambazo zote kwa pamoja walikuwa wanazisaidia timu hizo kila mmoja eneo lake.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela alisema mkataba huo umeanza kutekelezwa kuanzia Juni 20 na utafika kikomo baada ya miaka minane.
Alisema mkataba huo utakuwa katika maeneo manne tofauti ambayo ni kutoa vifaa vya michezo kwa timu ya Taifa na maendeleo ya michezo kwa vijana, msaada wa pesa taslimu kwa timu hizo zinapofanya vizuri pamoja na kudhamini mashindano yatakayoshirikisha Tanzania na nchi jirani.
Alisema kupitia mkataba huo TFF itanufaika kupata vifaa bora vya michezo kwa kipindi hicho huku ikitoa nafasi kwa klabu na vyama vya mikoa kununua vifaa hivyo kwa bei ya chini.
"Baada ya mchakato wa miaka mitatu hatimaye tumesaini mkataba huo na kampuni hiyo kampuni hiyo ambayo utakuwa na faida kubwa katika maendeleo ya soka nchini katika nyanja mbalimbali," alisema Mwakalebela.
Alisema kwa mujibu wa mkataba huo, +One itatoa jezi za mashindano seti 900, mazoezi seti 900, soksi za mashindano seti 1200, za mazoezi seti 1200, suti za michezo za mashindano seti 900, suti za mazoezi wakati wa mvua za mashindano seti 400, za mazoezi seti 400 pamoja na vifaa vingine vya michezo.
Alisema idadi hiyo ya vifaa itakuwa inatolewa kila mwaka ambapo gharama ya vifaa hivyo kwa mwaka ni dola za Kimarekani 450,000 wakati kwa kipindi chote cha mkataba ni dola 3,600,000.
Alisema mbali na vifaa hivyo pia timu hizo zitakuwa na mgao wa pesa taslimu zitakapofanya vizuri katika mshindano mbali ambayo timu hizo zitashiriki hasa katika mashindano ya ngazi za Afrika na Dunia.
"Timu hizo zote zitakuwa na mgao tofauti kutoka kwa kampuni hiyo pale timu hizo zinzpofanya vizuri katika michuano hiyo ili kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo kuongeza juhudi katika mashindano hayo," alisema Mwakalebela.
Alisema kupitia mkataba huo Tanzania itaandaa mashindano ambayo yatakayoshirikisha timu nne ikiwemo Taifa Stars na nchi nyingine za jirani ambapo michuano hiyo itafanyika kila mwaka na kwa kuanzia wataanza mwaka huu.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment