Shirikisho la kandanda Tanzania limeongeza makali katika msumeno wake wa kanuni za ligi kuu kwa wachezaji na klabu ili kuleta nidhamu mchezoni pamoja na kuboresha soka la Tanzania kuelekea katika ushindani zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela amesema moja ya matayarisho ya ligi kuu msimu ujao ni kuwepo na kanuni bora za ligi ili iwe bora.
Amesema ili kuhakikisha klabu pamoja na wachezaji wanawajibika TFF itatengeneza vitambulisho maalum kwa ajili ya wachezaji wote wa ligi kuu na hawataruhusiwa kucheza kama hawatokuwa navyo.
Amesema mchezaji atakayeshangilia goli kupitiliza na kupoteza muda au kuonyesha ishara ya kashfa au matusi kwa mashabiki wa timu pinzani, mchezaji huyo atafungiwa kucheza michezo mitatu pamoja na faini ya shilingi laki tano.
Mwakalebela amezungumzia swala la klabu kuingia mitini mchezoni baada ya kuhudhuria kikao cha maandalizi itatozwa faini ya shilingi milioni tano pamoja na kushushwa daraja, wakati timu ambayo haitafika kituoni itapoteza mchezo na kutozwa faini ya shilingi milioni tatu huku ikishushwa madaraja mawili.
Mbali na TFF kuongeza makali ya msumeno katika kanuni za ligi kuu Tanzania bara ambazo sasa zitatumika misimu yote na si mwaka mmoja mmoja kama ilivyokuwa awali, Mwakalebela amesema klabu zitaneemeka kwa kuongezewa mgawawo wa mapato ya mlangoni toka asilimia 25 hadi asilimia 30.
Aidha wawakilishi wa michuano ya kombe la shirikisho na ligi ya mabingwa sasa watakuwa wakicheza mchezo wa Ngao ya Hisani, ambapo kwa mwaka huu mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Agosti 16.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment